Uingereza kama demokrasia imepitiliza sasa. Keir Starmer njoo Africa utafurahi

So if ungepewa nafasi ya kuanzisha Mfumo ungeleta mfumo upi !?
 
So if ungepewa nafasi ya kuanzisha Mfumo ungeleta mfumo upi !?
Mkuu naona kama unafikiri mimi naikataa demokrasia. SIVYO. Kwangu mimi utawala wa kidemokrasia ni mfumo bora kuliko yote.

Nilichoeleza ni matatizo ya demokrasia yanayohitaji kufanyiwa kazi nyakati zote (bila kupuuzia) ili kuhakikisha huo mfumo unafanya kazi kama ilivyokusudiwa. Waasisi wa mfumo huo huko Ugiriki waliziona hizo changamoto na kuzijadili kwa kina.

Taifa linapoua mfumo thabiti wa elimu. Kisha kuendekeza rushwa, ufisadi na propaganda uchwara na wananchi nao kuamua kukaa kimya au kushabikia watu waovu na kuendekeza uchawa, demokrasia hufifia na kufa nchini. Hapo ndio mwanzo wa uimla, udikteta, kudorora kwa uchumi na madhila kadhaa katika jamii.

Sasa hivi hali hizo zinajitokeza huko Marekani na Ulaya - ambao siku zote hujitambulisha kama vinara wa demokrasia. Maisha yanazidi kuwa magumu na dunia nzima inaathirika sababu ya chaguzi mbovu na maamuzi mabovu ya wananchi wa nchi hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…