HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Tukiondoa Nukes, ni silaha gari haipo Ukraine kwa upande wa Russia?Hayo makombora UK walikuwa nayo kwenye maghala maana yalitumika kwenye uvamizi wa Iraq mwaka 2003.
Yamekaa ghalani zaidi ya miaka 25 hivyo wayatoa yakalipuliwe huko Ukraine.
Lengo ni kuyatumia hayo ili kupisha makombora ya kisasa zaidi ambayo sasa hivi yapo kwenye "production line".
Russia imesema itachukua hatua za kukabiliana na hatua hiyo na itachokifanya ni kupelekea uwanja wa vita silaha za kisasa zaidi ya hizo ili kuonyesha kwamba nao wana silaha "more advanced".
Tukumbuke kwamba Russia nayo imekuwa ikitumia silaha za zamani sana ili kusafisha maghala yake na sasa hivi wakiona hawana jinsi wataleta silaha za kisasa zaidi na huenda hapo ndipo vita itapomalizika.
Ukraine yazidi kuharibiwa na wanajeshi wake nao wazidi kuuawa vitani kila kikicha.