Uingereza miaka kumi lakini bado Maimuna

Uingereza miaka kumi lakini bado Maimuna

Ni tatizo la kujisahau na kutojichanganya na wenyeji kisawasawa, kwamba ukiwa nyumbani lugha ni kiswahili na huendi hata kwenye park kucheza na watu wenyeji na kujifunza maneno mbalimbali.

Unapotaka kujifunza lugha ya kigeni inabidi ufanye jitihada kujifunza matamshi na kuyafanyia mazoezi sisi tunashindwa hasa kwenye grammar, kwamba mtu kuwa na uwezo wa kusema sentensi, maneno na mafungu ya maneno. Grammar inatawaliwa na sheria zake na mtu ukizifuata sheria hizi unaweza angalau kuzungumza kiingereza na ukaeleweka, ukasoma magazeti na majarida mbalimbali na kuangalia news.

Kwahio hata kama utaishi miaka 20 na kuendelea ilhali hufahamu namna ya kutamka maneno ya kiingereza na kuweza kujieleza kwa ufasaha basi wewe utaendelea kuzungumza kiingereza chenye kukosewa matamshi na maneno.

Ila kuna shule mbalimbali za kufundisha lugha hii ya kiingereza ingawa kwa asie mwenyeji inakuwa ngumu kuzifuatilia. Lakini Uingereza pekee ndipo penye mchangayiko wa lugha mbalimbali lakini kiingereza kikiwa lugha rasmi.

Kuna lugha za kigeni ambazo zimekubaliwa kutumika katika baadhi ya wilaya na miji mingine kama kisomali na Urdu ambayo ni lugha inayozungumzwa Pakistan.

Ila lazima tukumbushane ukiishi nchi za watu huna budi kuzungumza lugha yao na sio kubishana kwa makelele kwenye mabasi kwa lugha zenu kama wenzetu wanigeria na kutoa masauti makubwa, jambo linalowaudhi sana wenyeji.

Asante sana mkuu yaani wewe ndo umenipa pa kuanzia najua na wenye hili tatizo wakifuatilia itawasaidia sana. Kweli JF kuna magreat thinkerz
 
Mkuu, kwanza pole kwa mkanganyiko ulioupata katika swala hilo ambalo hata mimi pia zamani lilikuwa linanisumbua. Kwa kifupi sana ukwel ni kuwa kuna baadhi ya maeneo ambapo watanzania ni wengi mfano Reading, sasa kuna tabia wengine huwa hawapendi kujichanganya na yawezekana kuna sababu nyingi za wao kutojichanganya yaani mara nyingi wanaongea kiswahili na hata mtindo wao wa maisha ni kama wa Tanzania kabisa na mtu anajisikia kuwa Tanzania zaidi badala ya kuwa uingireza kwa hali hiyo ni rahisi sana kupita mitaani esp.Reading kukuta watu weusi wanaongea kiswahili. Pia hii haimaanishi hawawezi kusikia ama kuelewa wengine wanaelewa lakini kukiongea ndo shida.

Asante sana mkuu maana umenipa pa kuanzia
 
Wewe kichwa maji kweli yaani mtoto kuongea kiingereza ana akili sana ? Mbona madogo wengi wanaongea kiswahili.

Yaani hata mimi huyu naye kaniacha kweli na imebidi nimpite maana nimekosa lakukomenti nikajua mtakuja kama nyie kunisaidia
 
Sasa utajuaje Kiingereza ilhali hata kiswahili chakupa tabu..MAIMUNA maana yake ni nini? Ni MAIMUNA au MAAMUMA.!!?
Anayekwenda Uingereza ili imsaidie ajue kiingereza nae ni bure tu, kila kitu kinawezekana tu ukitilia mkazo..sisi wengine tumeishi hapa hapa TZ lakini kiingereza tukiongea kinaeleweka based on grammar and syntax. Kuna namna mbili ya kufahamu lugha ya kigeni
1. Ishi katika mazingira yao ukijifunza hyo lugha.
2. Soma sana vitabu vyenye lugha hiyo..kwa lugha nyingine inabdi uwe na muongozo wenye lgha yako.

Nilichojifunza mm ni kuwa sisi ni wavivu sana kwenye kusoma vitabu iwe kiswahili au kiingereza.

Mkuu unajitapa umeishi hapa bongo wakati hata MAIMUNA hujui na unafikiri unanisahihisha mimi? Ngoja nikusaidie kwenye miaka ya mwanzoni mwa 90 ilianzishwa shule ya kiingereza kama sikosei wakaitangaza kwenye radio na tangazo lao lilibeba jina la yule asiyejua Kiiingereza anaitwa MAIMUNA basi kuanzia hapo ilikuwa kama Kiinglish hakipandi unaitwa Maimuna. Ni kama leo ilivyo Kayumba. Usikejeli kama hujui labda enzi hizo hamkua na redio kwenu au kijijini kwenu zilikuwa zinakamata idhaa za nchi jirani tu.
 
Wakuu naomba mnisaidie hivi unaweza ukaishi UK kwa miaka zaidi ya mitano na ukawa haujui Kiingereza? Maana jana kuna jamaa yangu anaishi UK-Liverpool amekuja likizo sasa nikakaa naye akatokea jamaa yangu mwingine nikamtambulisha sababu jamaa kasikia mjeba amejitundika huko muongo mmoja si akaangusha kwa Lugha yao mshikaji kujibu nikagundua loh!

Shida yangu sio kuona nini bali nashindwa kuelewa kama huko kwa wenzetu kuna mchanganyiko wa lugha. Nisaidieni maana kuna dada mmoja aliniambia akimaliza MBA yake hapa nchini anatafuta course UK angalau ya miezi sita ili ajibrashi hicho kilugha.

Msaada jamani hasa mlioko huko na mnipe ushauri je ni nchi au mji gani anaweza enda ambao hamna mchanganyiko wa lugha?
Kiingereza kwa UK huwezi kukwepa sijui unanunua vitu wapi, au labda huongei na watu? kwasababu hata wachina wanaongea kiingerezqa sasa kwa matanzania sidhani naona kama umetunga tu.
 
Ukiwa na Masistas digiliii na bado hujui kuwa kuishi uingereza sio ndio kujua kiingereza basi wewe ni juha namba moja. Kiingereza unaweza kujua hata bila kwenda Uingereza. Kilaza ni wewe usiyeelewa hata kwa mifano.

Nimekwambia kukaa karibu na bahari pekee hakukufanyi uwe mvuvi bora, unless uwe umeshiriki uvuvi wenyewe. Hakuna jiji litakalokufanya ujue kiingereza wewe kapuku, kiingereza utakimudu kwa kukiongea mara kwa mara. Unaweza kujifunza kinyamwezi bila kwenda Tabora, foolish coconut.

Kaa usubiri majuha wenzio wakujibu majibu tofauti na haya ya kwangu. Ipo siku utadhani ukivaa nguo za Messi utajua kucheza mpira huku miguu yako yote ya kushoto kama ulivyo ubongo wako

Mkuu kutokana na mfumo wa elimu yetu mbona hilo sio la kushangaza? Maana hata malecturer wanalecture kwa kiswahili na tukifanya presentation ndio hivyo tena full of broken gramar na tenses. Sasa nategemea kuwa meneja unafikiri report nitakuwa naziandika kibroken? Au kufanya official presentations unafikiri nitaendelea kuvunjavunja lugha nieleweke?

Ndo maana nilijua nikijichanganya na wahaya nitajua kihaya au na wamatumbi nitaongea kimatumbi. Alafu wengi hamuelewi sisi wakusoma kwenye lugha tuleteeni spelling hatukosei maana ndivyo tunavyovisoma na kupractice sana. Nataka fluent oral language je nitaipataje ili niongeze confidence na ufanisi?
 
Matatizo haya yapo kote duniani. Wapo wageni wengi hapa Tz ambao wameishi miaka mingi hapa lkn hawajui Kiswahili vizuri.

Nikweli hasa wahindi, na hii naona nisababu ya maendeleo yao ndo maana hawajichanganyi lakini haiwaathiri coz they need just little thing from Swahili speakers, sasa hawa ndugu zetu na dhikidhiki zao unafikiri sababu ndo hiyo? Au woga na wengine ukilaza wao wakujua maana vile vizee wanavyovichamba kule kwani vinajua lugha gani?
 
Mkuu, ni Maimuna na si Maamuma.

Lilikuwa ni Tangazo la shule ya Lugha kama sikosei miaka ya 80 mwishoni na dada akapokea simu (secretary) na alipoulizwa kama Boss yupo kwa Kiingereza, yeye akawa anajibu MAIMUNA.

Kutoka hapo ikawa kama hujui Kiingereza unaitwa Maimuna na ukichakachua cheti cha shule wanakuita KIHIYO.

Yaani ndo umenikumbusha vizuri mkuu asante, na mzee wako akiwa kibopa serikalini unaitwa mtoto wa Kingunge ingawa hii mpaka leo ipo, dah kweli tumetoka karibu lakini matukio yanatufanya tuone mbali sana
 
Kiingereza kwa UK huwezi kukwepa sijui unanunua vitu wapi, au labda huongei na watu? kwasababu hata wachina wanaongea kiingerezqa sasa kwa matanzania sidhani naona kama umetunga tu.

Natamani hata nimtaje jina mkuu ili unielewe ila ndo hivyo heshima mbele, naomba niamini nikweli hata mimi nimeshangaa na zaidi sio mjaji wa home maana kabla ya sasa alishakuja miaka mitatu nje na anaishi Liverpool
 
Nimebahatika kupitapita Uingereza mara nyingi sana, Watanzania wengi walioenda huko miaka 10-15 nyuma ambao hawajakwenda kwa malengo ya kusoma, wamekwenda huko na wamelemaa kwa uvivu, kuna niliowakuta wamejiripua kama Warwanda, Wakongo, Wasomali na wanapokea fedha za ukimbizi ambazo kwa maisha ya Uingereza ni kidogo sana lakini kwa maisha waliyotoka nayo bongo wanaziona ni nyingi.

Wengi wao hawajibidiishi kusoma na kutafuta maisha bora zaidi, wengine nimewakuta wamejisingizia uchizi au ulemavu ili wapate fedha za ziada za ulemavu.

Na pia nimekutana na watu ambao nawafahamu wapo Uingereza kwa miaka mingi sana (zaidi ya 25), hawa utakuta wengi wao wamesoma, wanaishi maisha ya mazuri zaidi, wanakaa sehemu ambazo ni nzuri kidogo, wengi wao wanaishi kwenye nyumba zao wenyewe na wame "integrate" vizuri sana na Waingereza na hawa nimeona kuwa wameji seclude kiaina fulani, na hawataki kuingiliana na waswahili waliojiripuwa.

Pia kuna kakikundi fulani ka watoto wa wanene huku Tanzania ambao wako huko kwa kusoma, wao hawa wengi wao wanakula raha tu, kwani wao wanangoja posho zao (ni zaidi ya mshiko wa wale waliojiripua) wao hawa ni watu wa kutumbuwa. Vijipashkuna vingi vilivyojiripuwa huwa vinawalenga hawa wa kundi hili, kwani wanajuwa hawa wanamshiko.

Kundi lingine nililokutana nalo la Watanzania wenye asili ya Kiasia, hawa wanafanya kazi kwa bidii na wako wenye biashara zao, wengine ni matajiri kwa kiasi fulani.

Wapo "wapemba" waliojiripua na baadhi yao sasa wana biashara huko tayari, hawa wamenifurahisha ni wachapa kazi sana na wanasoma kuliko jamaa zetu wa bara.

Ni mtazamo wangu tu wa kupita huko mara kwa mara.
 
Nimebahatika kupitapita Uingereza mara nyingi sana, Watanzania wengi walioenda huko miaka 10-15 nyuma ambao hawajakwenda kwa malengo ya kusoma, wamekwenda huko na wamelemaa kwa uvivu, kuna niliowakuta wamejiripua kama Warwanda, Wakongo, Wasomali na wanapokea fedha za ukimbizi ambazo kwa maisha ya Uingereza ni kidogo sana lakini kwa maisha waliyotoka nayo bongo wanaziona ni nyingi.

Wengi wao hawajibidiishi kusoma na kutafuta maisha bora zaidi, wengine nimewakuta wamejisingizia uchizi au ulemavu ili wapate fedha za ziada za ulemavu.

Na pia nimekutana na watu ambao nawafahamu wapo Uingereza kwa miaka mingi sana (zaidi ya 25), hawa utakuta wengi wao wamesoma, wanaishi maisha ya mazuri zaidi, wanakaa sehemu ambazo ni nzuri kidogo, wengi wao wanaishi kwenye nyumba zao wenyewe na wame "integrate" vizuri sana na Waingereza na hawa nimeona kuwa wameji seclude kiaina fulani, na hawataki Quintilian na waswahili waliojiripuwa.

Pia kuna kakikundi fulani ka watoto wa wanene huku Tanzania ambao wako huko kwa kusoma, wao hawa wengi wao wanakula raha tu, kwani wao wanangoja posho zao (ni zaidi ya mshiko wa wale waliojiripua) wao hawa ni watu wa kutumbuwa. Vijipashkuna vingi vilivyojiripuwa huwa vinawalenga hawa wa kundi hili, kwani wanajuwa hawa wanamshiko.

Kundi lingine nililokutana nalo la Watanzania wenye asili ya Kiasia, hawa wanafanya kazi kwa bidii na wako wenye biashara zao, wengine ni matajiri kwa kiasi fulani.

Wapo "wapemba" waliojiripua na baadhi yao sasa wana biashara hulo tayari, hawa wamenifurahisha ni wachapa kazi sana na wanasoma kuliko jamaa zetu wa bara.

Ni mtazamo wangu tu wa kupita huko mara kwa mara.

Mkuu hii nayo uliyonipa naiita ni side B ya waishio mamtoni, ndo maana wengine wanarudi na suruali za jeans original lakini la maana hawana, heheeee tate nane mgoshiiii
 
Ni kweli bwana mm nimekulia kijijini huko ndani kabisa..redio ilikuwa kwa Mwenyekiti tu na mpaka ikaliwe ndio yazungumza. Maimuna na Maamuma vyote vitamaanisha kitu kimoja kulingana na kwamba ni wapi linatumika.Kiswahili sanifu hakuna neno maimuna bali kuna maamuma..ikimaanisha mtu asiyejua/fahamu kitu/jambo fulani. Nashukuru kwa maneno yako.
Mkuu unajitapa umeishi hapa bongo wakati hata MAIMUNA hujui na unafikiri unanisahihisha mimi? Ngoja nikusaidie kwenye miaka ya mwanzoni mwa 90 ilianzishwa shule ya kiingereza kama sikosei wakaitangaza kwenye radio na tangazo lao lilibeba jina la yule asiyejua Kiiingereza anaitwa MAIMUNA basi kuanzia hapo ilikuwa kama Kiinglish hakipandi unaitwa Maimuna. Ni kama leo ilivyo Kayumba. Usikejeli kama hujui labda enzi hizo hamkua na redio kwenu au kijijini kwenu zilikuwa zinakamata idhaa za nchi jirani tu.
 
Ni kweli bwana mm nimekulia kijijini huko ndani kabisa..redio ilikuwa kwa Mwenyekiti tu na mpaka ikaliwe ndio yazungumza. Maimuna na Maamuma vyote vitamaanisha kitu kimoja kulingana na kwamba ni wapi linatumika.Kiswahili sanifu hakuna neno maimuna bali kuna maamuma..ikimaanisha mtu asiyejua/fahamu kitu/jambo fulani. Nashukuru kwa maneno yako.

Mkuu usinichanganyie mada hata hapa kwenye Kiinglish simaanishi Vocabulary bali ni tenses and grammar tu. Ni kusema "si ukujege na huku" lol!!!!!!

Mshikaji alituchanganyia madawa kama gongo ya Kigogo Mbuyuni
 
Kiingereza kwa UK huwezi kukwepa sijui unanunua vitu wapi, au labda huongei na watu? kwasababu hata wachina wanaongea kiingerezqa sasa kwa matanzania sidhani naona kama umetunga tu.
We huwajui hao wanao zungumziwa hapa.
Hata mimi nimeshawaona wakija leave.
Mi mwenyewe english yangu ya kuunga
ila nilijikuta namzidi kwa kiasi fulani yani.
Halafu wanajaribu kuficha udhaifu wao huo
kwa kuongea haraka with a fake british accent
 
Mbona nilikuwa Berlin na Uholanzi na watoto hawajui Kiingereza?

Nilifika hadi juu kule Sweden, watoto wakanipa Hej hej? Na mie nikawaaga Hej Do!!!

Au hao siyo Wazungu? Ufaransa ndiyo kabisa na hasa hawa Nigga In Paris.....
nilidhani wazungu ni waingereza!
Kumbe hadi wasweden!
 
Nikweli hasa wahindi, na hii naona nisababu ya maendeleo yao ndo maana hawajichanganyi lakini haiwaathiri coz they need just little thing from Swahili speakers, sasa hawa ndugu zetu na dhikidhiki zao unafikiri sababu ndo hiyo? Au woga na wengine ukilaza wao wakujua maana vile vizee wanavyovichamba kule kwani vinajua lugha gani?
Nadhani ni k/sbb ya kutopenda kujichanganya kwa sbb mbalimbali, km wafanyavyo baadhi ya wahindi hapa Tz, na km ulivyoitaja sbb mojawapo.Vilevile, ni k/sbb ya hofu/kutojiamini na kukosa msukumo wa ndani (self motivation).
 
Kaazi kweli kweli. wakati unaongea lugha yoyote usiogope kuonekana mshamba,usijali sijui grammar au syntax au conjunction- wewe vunja tu -huo sio mtihani kwamba baada ya maongezi utapewa below. Hatimaye unajikuta unatema lugha hiyo kama wenyewe.
 
Nimebahatika kupitapita Uingereza mara nyingi sana, Watanzania wengi walioenda huko miaka 10-15 nyuma ambao hawajakwenda kwa malengo ya kusoma, wamekwenda huko na wamelemaa kwa uvivu, kuna niliowakuta wamejiripua kama Warwanda, Wakongo, Wasomali na wanapokea fedha za ukimbizi ambazo kwa maisha ya Uingereza ni kidogo sana lakini kwa maisha waliyotoka nayo bongo wanaziona ni nyingi.

Wengi wao hawajibidiishi kusoma na kutafuta maisha bora zaidi, wengine nimewakuta wamejisingizia uchizi au ulemavu ili wapate fedha za ziada za ulemavu.

Na pia nimekutana na watu ambao nawafahamu wapo Uingereza kwa miaka mingi sana (zaidi ya 25), hawa utakuta wengi wao wamesoma, wanaishi maisha ya mazuri zaidi, wanakaa sehemu ambazo ni nzuri kidogo, wengi wao wanaishi kwenye nyumba zao wenyewe na wame "integrate" vizuri sana na Waingereza na hawa nimeona kuwa wameji seclude kiaina fulani, na hawataki Quintilian na waswahili waliojiripuwa.

Pia kuna kakikundi fulani ka watoto wa wanene huku Tanzania ambao wako huko kwa kusoma, wao hawa wengi wao wanakula raha tu, kwani wao wanangoja posho zao (ni zaidi ya mshiko wa wale waliojiripua) wao hawa ni watu wa kutumbuwa. Vijipashkuna vingi vilivyojiripuwa huwa vinawalenga hawa wa kundi hili, kwani wanajuwa hawa wanamshiko.

Kundi lingine nililokutana nalo la Watanzania wenye asili ya Kiasia, hawa wanafanya kazi kwa bidii na wako wenye biashara zao, wengine ni matajiri kwa kiasi fulani.

Wapo "wapemba" waliojiripua na baadhi yao sasa wana biashara hulo tayari, hawa wamenifurahisha ni wachapa kazi sana na wanasoma kuliko jamaa zetu wa bara.

Ni mtazamo wangu tu wa kupita huko mara kwa mara.

Maajabu leo una point yakuongea. Keep it up!!
 
We huwajui hao wanao zungumziwa hapa.
Hata mimi nimeshawaona wakija leave.
Mi mwenyewe english yangu ya kuunga
ila nilijikuta namzidi kwa kiasi fulani yani.
Halafu wanajaribu kuficha udhaifu wao huo
kwa kuongea haraka with a fake british accent

Mwe! hapo kazi ipo
 
Maajabu leo una point yakuongea. Keep it up!!

Huwa hunisomi vizuri tu, ungepata faida kubwa sana ungechukuwa wasaa wako kidogo kunisoma, na ambapo hujapaelewa ungechukuwa fursa ya kuniuliza, ungejifunza mengi sana.
 
Back
Top Bottom