- Thread starter
- #21
Ni tatizo la kujisahau na kutojichanganya na wenyeji kisawasawa, kwamba ukiwa nyumbani lugha ni kiswahili na huendi hata kwenye park kucheza na watu wenyeji na kujifunza maneno mbalimbali.
Unapotaka kujifunza lugha ya kigeni inabidi ufanye jitihada kujifunza matamshi na kuyafanyia mazoezi sisi tunashindwa hasa kwenye grammar, kwamba mtu kuwa na uwezo wa kusema sentensi, maneno na mafungu ya maneno. Grammar inatawaliwa na sheria zake na mtu ukizifuata sheria hizi unaweza angalau kuzungumza kiingereza na ukaeleweka, ukasoma magazeti na majarida mbalimbali na kuangalia news.
Kwahio hata kama utaishi miaka 20 na kuendelea ilhali hufahamu namna ya kutamka maneno ya kiingereza na kuweza kujieleza kwa ufasaha basi wewe utaendelea kuzungumza kiingereza chenye kukosewa matamshi na maneno.
Ila kuna shule mbalimbali za kufundisha lugha hii ya kiingereza ingawa kwa asie mwenyeji inakuwa ngumu kuzifuatilia. Lakini Uingereza pekee ndipo penye mchangayiko wa lugha mbalimbali lakini kiingereza kikiwa lugha rasmi.
Kuna lugha za kigeni ambazo zimekubaliwa kutumika katika baadhi ya wilaya na miji mingine kama kisomali na Urdu ambayo ni lugha inayozungumzwa Pakistan.
Ila lazima tukumbushane ukiishi nchi za watu huna budi kuzungumza lugha yao na sio kubishana kwa makelele kwenye mabasi kwa lugha zenu kama wenzetu wanigeria na kutoa masauti makubwa, jambo linalowaudhi sana wenyeji.
Asante sana mkuu yaani wewe ndo umenipa pa kuanzia najua na wenye hili tatizo wakifuatilia itawasaidia sana. Kweli JF kuna magreat thinkerz