Uingereza: Waziri Mkuu apigwa faini na Polisi kwa kutofunga mkanda wa Kiti akiwa ndani ya gari

Uingereza: Waziri Mkuu apigwa faini na Polisi kwa kutofunga mkanda wa Kiti akiwa ndani ya gari

Huku mjeda juzi anamwambia Traffic PAKA wwe,alafu wewe nakucheki Traffic akabaki kuuliza mi paka mi paka??
 
Propaganda hizo hata huko pia haiwezekani labda kama wanataka kufanya show kama hivyo ili kuwadanganya watu, Malkia Elizabeth hajawahi kufunga mkanda na wala hakuwahi na leseni ya udereva na alikuwa anaedesha gari!
Nani kakuambia haya ?...acha uongo
 
Nani kakuambia haya ?...acha uongo

Malkia wa Uingereza hata passport hakuwa nayo na alikuwa JUU ya Sheria za Uingereza hata mtoto wake Mfalme yuko JUU ya Sheria za Uingereza hashitashiki popote nchini Uingereza!
 
Malkia wa Uingereza hata passport hakuwa nayo na alikuwa JUU ya Sheria za Uingereza hata mtoto wake Mfalme yuko JUU ya Sheria za Uingereza hashitashiki popote nchini Uingereza!
Hilo kwa kiongozi wa taifa sio la kushangaza.
 
Nimeamua tu kuwaza kwa sauti kuwa ingekuwa hapa nchini kwetu ingewezekana? wenzetu wako serious na mambo yao na ndio maana huwa wanafanikiwaga mambo yao someni habari hapo chini.

===

Sunak.JPG

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amepigwa faini kwa kutofunga mkanda kwenye gari lililokuwa likitembea wakati akirekodi video kwa ajili ya mitandao ya kijamii.

Polisi wa Lancashire wamesema kuwa wamempa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 42, adhabu ya kulipa faini isiyobadilika masharti.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kwamba Sunak amekubali kuwa hilo lilikuwa kosa na ameomba radhi na kuongeza kuwa atalipa faini hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Kijana kalewa madaraka mapema hivi?

Shida ya vinasaba vya uafrika ina muandama, muafrika akipata matako ulia pata...

Yeye pamoja na uhindi(ukanjibai) na wazazi walio tokea afrika mashariki lakini bado hivi vitabia vina mpeleka puta

Hizi kashfa ndogo lakini baadae zina weza kuja kumsumbua na kumuondolea sifa ya kuwa kiongozi mkuu ktk taifa kubwa

Wenzie waliondoka kwa vikashfa vidogo...

Mawaziri walio pita ktk nafasi aliyonayo

Kuna waziri wa ulinzi mwanamama pale ujerumani kaachia kiti juzi kwa vikashfa vidogo sana ambavyo ukukwetu tuna chukulia poa

Ila kwa wenzetu ni kuonesha uwajibikaji
 
Huko ndiko kuna utawala wa sheria, huku hata rais akijamba watu watashangilia
Kujamba ni kosa? Kati ya mifano yote ya hovyo inayofanywa na watawala, umeona jambo la kiasili la mwili ndio kosa?! WaTz akili zetu, sijui.
 
Kujamba ni kosa? Kati ya mifano yote ya hovyo inayofanywa na watawala, umeona jambo la kiasili la mwili ndio kosa?! WaTz akili zetu, sijui.
Nadhani alikusudia huko kushangiliwa na watu ndio noma
 
Nadhani alikusudia ili kuuonyesha umma kwamba SHERIA NI MSUMENO.
Namaanisha ya kwamba nchini UK hata unapopanda taxi, dereva kabla ya kuwasha gari huakikisha umefunga mkanda.
 
Kujamba ni kosa? Kati ya mifano yote ya hovyo inayofanywa na watawala, umeona jambo la kiasili la mwili ndio kosa?! WaTz akili zetu, sijui.
Jifunze kitu inaitwa rhetoric
 
Napenda kuchukua nafasi hii kukumbusha tu wakuu.

Kufunga mkanda katika gari ni kitu muhimu sana, na kutaweza kusaidia kupunguza madhara makubwa katika ajali.

Ajali ikitokea haijui wewe Waziri Mkuu wala kapuku.

Haijali una hela au masikini.
 
Back
Top Bottom