Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Suella Braveman ambae alikuwa akiongoza wizara ya mambo ya ndani amejiuzulu leo jioni baada ya kukiuka kanuni za usalama wa habari mitandaoni kwa kutumia anuani binafsi ya barua pepe badala ya anuani maalum ya serikali.
Waziri huyo anadaiwa kutumia anuani binafsi kutuma taarifa nyeti katika mitandao ya serikali jambo ambalo linaweza kupoteza taarifa hizo kwa wale wasokusudiwa.
Bi Suella alituma ujumbe wa barua pepe uloonyesha mswaada uloongelea sera ya uhamiaji kupitia simu yake ya mkononi jambo lilokikuka kiufundi suala zima la usalama wa mitandao ya serikali.
Lakini katika kinaochoonekana kwa bi Suella kutokubali uongozi wa waziri mkuu Liz Truss, katika barua yake ya kujiuzulu amedai kutokuwa na imani na serikali na mwelekeo wake na pia serikali kutokufanya yake ambayo iliyaahidi kwa wapiga kura.
Pia katika barua hiyo bi Suella amedai kuwa serikali bado imeshindwa kushughulikia suala la uhamiaji ulozidi kipimo ambapo idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakiingia nchini humo kinyume cha sheria na kushindwa kuzuia mitumbwi inotumiwa na wahamiaji hao kuingia nchini humio kupitia mkondo ujulikanao kama "English Channel".
Katika barua yake alomjibu bi Suella, waziri mkuu Liz Truss amekubali kujiuzulu huko na kusisitiza umuhimu wa viongozi wa serikali kutii maadili ya uongozi na kulinda siri za baraza la mawaziri.
Serikali ya Uingereza bado ipo matatani ambapo waziri mkuu Liz Truss amekuwa akabiliwa na madai ya kutakiwa kujiuzulu jambo ambalo amekuwa akipingana nalo kwa wiki zaidi ya mbili sasa.
Hali kadhalika ndani ya chama cha wafahidhina kumekuwepo mipasuko na mikanganyiko ambapo wapo wanachama wanotaka Liz Truss ajiuzulu na wapo pia wanotaka bwana Boris Johnson arejeshwe ili kukiokoa chama hicho dhidi ya mashambulizi kutoka vyama vya upinzani vikiongozwa na chama cha Labour.
Hata hivyo kitendo cha bi Suella Braveman bado kimeendelea kuleta masuali mengi juu ya uwezo wa baadhi ya viongozi katika chama cha wahafidhina hususan wale ambao badi umri wao ni mdogo kisiasa.
Hadi sasa Bi Liz Truss amewateua katika baraza lake la mawaziri wale ambao walikuwa wakimuunga mkono mhasimu wake bwana Rishi Sunak ambae walichuana katika kinyang'anyiro cha kuongoza chama cha wahafidhina. Siku chache zilopita, Bi Liz Truss alimteua bwana Jeremy Hunt kuwa waziri wa fedha na leo jioni amemteua bwana Grant Shapps kuwa waziri wa mambo ya ndani.
Bi shaka mambo haya yaendelea kuwapa wakati mgumu wapiga kura wa nchi hiyo ambao mpaka sasa wakabiliwa na baridi kali ijayo kuanzia mwezi ujao wa November na kupanda kwa kasi kwa gharama za maisha.