Uingereza yaichimba mkwara Kremlin

Tanker kitu Gani huoni kipigo

alichokula Iran pamoja na true promise imeyeyuka
Wewe mtoto mdogo naona likizo imeanza unaiba simu za wakubwa.
Hata unachoongea hukijui.
Kichapo gani unasemea wewe!?
Unazungumzia lile shambulio la ndege 100 lilofeli kiasi hata picha hazionekani za madhara!?
Kama bwana wako UK ana uwezo aende akakomboe meli yake ya mafuta iliyotekwa na Iran 2019.
Aya peleka simu kwa dada yako haraka sana.
 
Huyo jamaa siju deputy wa defense force ni Mwijaku wa kizungu
 
Uchumi ni sehemu ndogo ya vita. Ingekuwa uchumi unashinda vita Russia asingeshindwa pale Afghanistan, US asingekimbia pale Vietnam, US asingeshindwa pale Afghanistan. Hata Ukraine asingemsumbua Russia
 
Uchumi ni sehemu ndogo ya vita. Ingekuwa uchumi unashinda vita Russia asingeshindwa pale Afghanistan, US asingekimbia pale Vietnam, US asingeshindwa pale Afghanistan. Hata Ukraine asingemsumbua Russia
Sawa jenerali
 
Kwanza uwe unaacha aya ukiandika. Kisha wewe na wasiojua wenzio mzingatie kwamba Soviet Union iliingia mkataba wa kutopigana na Ujerumani (Molotov-Ribbentrop Pact) wa mwaka 1939 kuepusha kupigana ndani ya miaka 10 inayofuatia.

Soviet Union au Urusi kama underdog akashirikiana na Ujerumani kuivamia Poland. Wakaigawana, mwaka huo Ujerumani ikavamia Belgium na ndipo Uingereza ikatangaza vita dhidi ya Ujerumani. Ujerumani ilikuwa inaiogopa sana Uingereza ila ikalazimika iingie vitani. Walipigana miaka mitano ila huo udogo wa Uingereza mnaosema hakuna mwanajeshi wa Ujerumani hata mmoja alitia mguu Uingereza. Hiyo ndio Britain usiyoijua.

Uingereza ikaingia front kupigana kuikomboa Ufaransa na Belgium, baadae Marekani akaja. Miaka hiyo Urusi ikaivamia Finland ikateseka kushinda vita, Ujerumani baada ya kuona Warusi ni wachovu ikawavamia ili iwashinde faster faster maana Waingereza hawapigiki. Then majeshi ya Ujerumani yakaingia Urusi hadi kidogo kuichukua Moscow walifika within 20km, sio mtego wa Urusi ni uwezo mbovu. Warusi zaidi ya 20 million walikufa unasemaje ni mtego.

Allies wakiongozwa na Marekani wakatoa msaada mkubwa sana wa ndegevita, chakula, mafuta, vifaru, malori kwa Soviets kupigana ili wasishindwe na Ujerumani. Wakati huo wao wakipigana Western front. Bila msaada wa allies Urusi alikuwa mnyonge mbele ya Ujerumani ile.

Urusi ilivamiwa na Ujerumani hivyo ilibidi ipigane haukuwa msaada ilikuwa lazima, Uingereza hata haikuvamiwa na iliombwa na Ujerumani haitaki shida ila ikaingia nayo vitani. Urusi ni coward aliyekumbatia wahuni kwenye Molotov-Ribbentrop Pact ili wasimpige, na wakampiga akaja saidiwa na wenye nia njema.
 
Marekani ilikuwa koloni la Muingereza ila muingereza kwa sasa hawezi kubattle na mmarekani hata kwa dawa..zama zinabadirika sana ,watu wasikalili
 
Watoto wa mwaka 2000s hao,hawajui unyama wa Uingereza kwenye medani ya Vita na fitna.
Na hawajui kuwa sio, Napoleon Bonaparte wa Ufaransa,wala Àlexander The Great wa Russia wala Hitler wa Ujerumani aliyediriki kupigana vita na Uingereza na akashinda. Kama Putin anataka kuuramba moto, ajaribu!
 
PUMBA. Hapa hatuongelei mambo ya miaka 100 iliyopita. Miaka hiyo ata Israel alikuwa anatumia siku moja kfika Beirut baada yakuvuka boda ya Lebanon. Lakini sasa hivi miezi 2 wame stuck hapo boda. Acheni kukariri
 
hii unwritten constitution UK, wako zigzag sana kwa zaidi ya miaka 12 sasa hawana utulivu katika utawala, hawana nguvu ya ushawishi tena duniani na wala hawaaminiki tena.
Laana ya kujitoa EU inawaumbua sana.

Kwa hali ilivyo sasa UK anaweza akachapwa makofi hata na Israel tu.

Nadhani UK, hawana tofauti sana katika nguvu za kiuchumi na kijeshi na nchi nyingi za Africa kwa sasa 🐒
 
Wewe unajua kubonyeza button tu. Kazi ipo kuliweka ilo kombola kwenye luncher yake unatakiwa huko nyuma kuwe hakujaharibika
Shoga anakaa kwenye logistics na mipango special forces wapo watafanya kazi hizo....
Mfano shoga akabuni aina mpya ya silaha then wakatumia mawazo hayo kuitengeneza hapo unaonaje?
Au hata akawa mpishi ....au medical personel
 
UK zaman sio sasa hawezi kwenda head to head hata na Turkey mna mawazo ya enzi za kikoloni
Usiseme hivyo mkongwe ni mkongwe anasiri za nchi nyingi dunian anapesa na uchumi wa kuhimili vita nyie mnamuona kimya ila vita kashazichapa sana dunia na kuitawala
 
Nilisoma mahali taarifa ya huyo jamaa, niliishia tu kucheka! Maana unaona kabisa anaitishia nyau Urusi.
Sasa mkuu, hiyo ni taarifa ya General wa Uk ambaye ana Abc za jeshi lake na uwezo wake, wewe unacheka una profile gani kwenye mambo ya jeshi?

Watanzania ni kawaida kwa muimba kwaya kumchallenge daktari kwenye sekta ya Afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…