Uingereza yaichimba mkwara Kremlin

Uingereza yaichimba mkwara Kremlin

Nimejikuta nacheka mno mpaka machozi baada ya kusoma kauli ya UK Deputy Chief of Defence Staff Rob Magowan isemayo
"Uingereza ipo tiyari kuingia vitani na Urusi usiku wa leo endapo kama Russia itaivamia Ulaya Mashariki.

View attachment 3159183
“Britain is ready to engage Russia tonight if Russian troops invade Eastern Europe” .

What a joke 😂😂
Unacheka sababu wewe ni mnywa kahawa tu hujui chochote kuhusu jeshi la Uk wala la Russia zaidi ya kupata porojo za mitandaoni.
 
Wanajeshi wa UK hawachelewi kuandama kumshinikisha huyu jeneral ajiuzulu..

Hakuna hata nchi chini ya hii sayari inayo weza kupambana Russia kwenye ulingo wa viti..

Vita ni mbaya sana tuachen ushabiki maandaz.
Ukrainians are doing it
 
Huna akil hivi unaijua UK wewe kwenye ulimwengu wavita
Kwenye top 10 ya mataifa yenye nguvu kijeshi UK inazidiwa hata na South Korea. Ni moja ya mataifa yenye nguvu ila kwa Russia, UK ni mdogo sana. Russia kijeshi inalinganishwa na USA.
 
Uingereza ni kitaifa kidogo lakini kina historia ya kushinda vita nyingi sana mpaka kutengeneza empire kubwa.

Uingereza mwishoni mwa vita ya pili ya dunia ilishawahi kuandaa mpango wa kuipiga Urusi (USSR), mpango ulioitwa operation unthinkable (google). Hata hivyo waliusitisha baada ya chama cha labor kuingia madarakani!
 
Huna akil hivi unaijua UK wewe kwenye ulimwengu wavita
Was***ge tu Hao hawana jipya Kwa sasa Putin Kesha waambia wafunge Midomo kama ni wanaume kweli wamvamie kama ambavyo walivyo Fanya Kwa Saddam na Gadaffi tuone ,

Wamemjaza upepo zelensky kuwa watamuunga na jumuia ya NATO mwenzao anapigwa mpaka Leo hii wamebaki kumtazama Tu what a foolish kama kweli hawa waogopi Russia wakati Russia anaivamia Ukraine kwanini wasingefanya haraka haraka kumuunganisha zelensky ktk huo umoja wa NATO ili Russia Atakavyo ipiga Ukraine wapate kumchangia ni nini wanacho kuogopa haswaa!?
 
Hata mongolia imeshawahi kuitawala asia na baadhi ya nchi ulaya.

Ottoman empire imeshawahi kutawala eneo kubwa tu kibabe.

Hata roma imeshawahi kutawala dunia.

Acha kutuletea historia uingereza hana chochote cha kumfanya mrusi.

Kadiri unavyopigana vita ndivyo unavyozidi kuwa imara na madhubuti na unapata uzoefu mrusi ana uzoefu na vita.

Wabishi wote wa dunia mrusi kawanyonya kamasi kuanzia napolean bonaparte mpaka adolf hitler.
Mwambie Huyo 🤣🤣🤣🤣

Hao wame karili maisha muingereza now days hata akisimama peke yake na Iran lazima jasho la kwapa limtoke inshort uingereza anajua kuwa nyuma yake ana backup ya USA ndio maana huwa USA anapotoa kauli yoyote na yeye anajifanya kufuata mkumbo ila kiuhalisia Hana uwezo wakupigana na Russia kwanza hata katika zile top 5 za nchi zenye uwezo wa Mkubwa wa kivita kwa sasa hayupo aache mbwembwe
 
Kisiwa chenyewe cha UK kipo kama Zanzibar. Bomu moja tu kutoka russia Kisiwa chote kinakuwa kifusi.
 
Mimi kama Mrusi mweusi sina wasiwasi, jana Putin alisema kuna watu wana wasiwasi hawapaswi kuwa nao.

Na wasiwasi umenitoka baada ya chuma kimoja tu cha Oreshnik kudondoka dunia nzima imesimama, hawa watu walijiandaa vyema na wanachokifanya.
mrembo nifah lini umekuwa mrusi?
 
Mimi kama Mrusi mweusi sina wasiwasi, jana Putin alisema kuna watu wana wasiwasi hawapaswi kuwa nao.

Na wasiwasi umenitoka baada ya chuma kimoja tu cha Oreshnik kudondoka dunia nzima imesimama, hawa watu walijiandaa vyema na wanachokifanya.
Urusi ndo nchi pekee ninayoweza kusimama mbele kuipigania vitani,...WWW3 tukutane Russia
 
Mahaba pembeni
Watu bado wana akili za ile Britain ya ma meli .karne hii UK hawezi battle na Russia head to head kwa military technology huu ndio ukwel mchungu .
Iyo special operation anayo endesha Russia ku demilitarized ukraine ange amua kufanya kama anavyo fanya Israel kule gaza na Lebanon Ukraine yote ingekua magofu zamani sana .

Sio UK,France wala German anae weza moto wa Russia ndio maana wana unga mkono wote kuji jaza minguvu sio mchezo
 
Russia ndio ilikua core ya soviet baad ya kuvunjika walibaki na vitu vingi sana kijeshi .technologia .siraha zingine ndo izo zime enda kutupwa kama chuma chakavu apo ukraine
Kwamba Russia ndo kaweza ku retain nguvu za me za kijeshi tangu WW 2?
 
Weee weeeh weeeee mama mkanye mwanao katika mistake kubwa Putin atafanya ni kuibeep Uk. Ivi Putin ataanzajeee anzage kuivamia uk, nchi ina malkia kama hajuii nguvu ya malkia basi ajaribu.
 
Weee weeeh weeeee mama mkanye mwanao katika mistake kubwa Putin atafanya ni kuibeep Uk. Ivi Putin ataanzajeee anzage kuivamia uk, nchi ina malkia kama hajuii nguvu ya malkia basi ajaribu.
Malkia ana nguvu gani, labda ile
 
Kama uchumi unapigana basi Japani angewapiga wengi. Vita ni science, waarabu wana mihela lakini uwanja wa vita sio wao
Vita ni pesa uchumi wa Urusi unaingia mara 2 kwa uchumi wa Britain, acheni kuota ndoto, huyu General wa UK sio mpumbavu kama hapo kijiweni mtogole eti hajui Urusi ina uwezo gani akachimba mkwara tu km kimbwa koko cha hapo jalalani kwenu! Mashabiki wa vita mnadhani ni yanga na simba hii

Kwanza uwe unaacha aya ukiandika. Kisha wewe na wasiojua wenzio mzingatie kwamba Soviet Union iliingia mkataba wa kutopigana na Ujerumani (Molotov-Ribbentrop Pact) wa mwaka 1939 kuepusha kupigana ndani ya miaka 10 inayofuatia.

Soviet Union au Urusi kama underdog akashirikiana na Ujerumani kuivamia Poland. Wakaigawana, mwaka huo Ujerumani ikavamia Belgium na ndipo Uingereza ikatangaza vita dhidi ya Ujerumani. Ujerumani ilikuwa inaiogopa sana Uingereza ila ikalazimika iingie vitani. Walipigana miaka mitano ila huo udogo wa Uingereza mnaosema hakuna mwanajeshi wa Ujerumani hata mmoja alitia mguu Uingereza. Hiyo ndio Britain usiyoijua.

Uingereza ikaingia front kupigana kuikomboa Ufaransa na Belgium, baadae Marekani akaja. Miaka hiyo Urusi ikaivamia Finland ikateseka kushinda vita, Ujerumani baada ya kuona Warusi ni wachovu ikawavamia ili iwashinde faster faster maana Waingereza hawapigiki. Then majeshi ya Ujerumani yakaingia Urusi hadi kidogo kuichukua Moscow walifika within 20km, sio mtego wa Urusi ni uwezo mbovu. Warusi zaidi ya 20 million walikufa unasemaje ni mtego.

Allies wakiongozwa na Marekani wakatoa msaada mkubwa sana wa ndegevita, chakula, mafuta, vifaru, malori kwa Soviets kupigana ili wasishindwe na Ujerumani. Wakati huo wao wakipigana Western front. Bila msaada wa allies Urusi alikuwa mnyonge mbele ya Ujerumani ile.

Urusi ilivamiwa na Ujerumani hivyo ilibidi ipigane haukuwa msaada ilikuwa lazima, Uingereza hata haikuvamiwa na iliombwa na Ujerumani haitaki shida ila ikaingia nayo vitani. Urusi ni coward aliyekumbatia wahuni kwenye Molotov-Ribbentrop Pact ili wasimpige, na wakampiga akaja saidiwa na wenye nia njema.
Wewe hujui chochote unaropoka historia ya wapui hiyo? Sio kweli usidanganye watu
 
Kama uchumi unapigana basi Japani angewapiga wengi. Vita ni science, waarabu wana mihela lakini uwanja wa vita sio wao



Wewe hujui chochote unaropoka historia ya wapui hiyo? Sio kweli usidanganye watu
Sawa jenerali wa kwa mpalange we unajua sna vita kuliko General wa Britain, yaishe
 
Back
Top Bottom