Kwanza uwe unaacha aya ukiandika. Kisha wewe na wasiojua wenzio mzingatie kwamba Soviet Union iliingia mkataba wa kutopigana na Ujerumani (Molotov-Ribbentrop Pact) wa mwaka 1939 kuepusha kupigana ndani ya miaka 10 inayofuatia.
Soviet Union au Urusi kama underdog akashirikiana na Ujerumani kuivamia Poland. Wakaigawana, mwaka huo Ujerumani ikavamia Belgium na ndipo Uingereza ikatangaza vita dhidi ya Ujerumani. Ujerumani ilikuwa inaiogopa sana Uingereza ila ikalazimika iingie vitani. Walipigana miaka mitano ila huo udogo wa Uingereza mnaosema hakuna mwanajeshi wa Ujerumani hata mmoja alitia mguu Uingereza. Hiyo ndio Britain usiyoijua.
Uingereza ikaingia front kupigana kuikomboa Ufaransa na Belgium, baadae Marekani akaja. Miaka hiyo Urusi ikaivamia Finland ikateseka kushinda vita, Ujerumani baada ya kuona Warusi ni wachovu ikawavamia ili iwashinde faster faster maana Waingereza hawapigiki. Then majeshi ya Ujerumani yakaingia Urusi hadi kidogo kuichukua Moscow walifika within 20km, sio mtego wa Urusi ni uwezo mbovu. Warusi zaidi ya 20 million walikufa unasemaje ni mtego.
Allies wakiongozwa na Marekani wakatoa msaada mkubwa sana wa ndegevita, chakula, mafuta, vifaru, malori kwa Soviets kupigana ili wasishindwe na Ujerumani. Wakati huo wao wakipigana Western front. Bila msaada wa allies Urusi alikuwa mnyonge mbele ya Ujerumani ile.
Urusi ilivamiwa na Ujerumani hivyo ilibidi ipigane haukuwa msaada ilikuwa lazima, Uingereza hata haikuvamiwa na iliombwa na Ujerumani haitaki shida ila ikaingia nayo vitani. Urusi ni coward aliyekumbatia wahuni kwenye Molotov-Ribbentrop Pact ili wasimpige, na wakampiga akaja saidiwa na wenye nia njema.