Wabongo bana. Kambi ni ya mafunzo na mazoezi ya makurutu wa British Army(BATUK) wakishirikiana na KDF, sio kambi ya kivita. Maeneo ambayo wamekubaliwa kutia kambi ni mali ya Kenya Airforce, Nanyuki, na wanalipia! Vibali vya kufanya shughuli zote hizi wanapewa na GOK sio wao ndio wanajiamulia. Hivi ni vitu vya kawaida sana duniani, kutoka Ufilipino, Taiwan, S.Korea hadi Djibouti. Nyie tu ndio mnashangazwa na vitu vya kawaida kama hivi, aisee ujamaa uliwalemaza akili kweli kweli. Acheni ushamba majirani. [emoji1][emoji1][emoji1] Sidhani duniani kuna mtu ambaye anaogopa mzungu zaidi ya mtz. Yaani mkiwaona tu wanajeshi wenye sura nyeupe zaidi ya mia hapo tayari mnaanza kulia tumevamiwaaa! [emoji23] Ndio maana baada ya lile shambulizi la kigaidi la Dusit mlifungua nyuzi zaidi ya hamsini humu mkimsifia mzungu mmoja tu! Eti ni Commando kama wale wa filamu za action. Badilikeni bana.