Uislam na Ukristo siyo maadili ya Mtanzania na Mwafrika, ni moja ya nyenzo ya mmomonyoko wa maadili

Uislam na Ukristo siyo maadili ya Mtanzania na Mwafrika, ni moja ya nyenzo ya mmomonyoko wa maadili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UISLAM NA UKRISTO SIÔ MAADILI YA MTANZANIA NA MUAFRIKA NI MOJA YA NYENZO YA MMOMONYOKO WA MAADILI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kîla jamii inamaadili yake. Maadili yanatokana na ûtamaduni wa jamii Husika. Kîla jamii inautamaduni wake.

Maadili ni mafundisho yanayotolewa kwèñye jamii yenye kuonyesha Tàbia Njema na tàbia Mbaya na kutaka Watu wafuate mambo Mema. Maadili ya jamii Moja huweza kutofautiana na maadili ya jamii zingine. Ingawaje Yapo maadili àmbayo yanafanana.

Kukiuka Maadili ya jamii yako ndîo huitwa MMOMONYOKO WA MAADILI.

Muafrika anamaadili yake kutokana na tamaduni Zake.
Wazungu wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Waarabu wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.
Wachina, wahindi n.k wôte wanamaadili Yao kutokana na tamaduni zào.

Kîla jamii ina Mila na desturi nzuri na Potofu. Mila na desturi au tuite maadili huwa potofu Kwa sababu mbalimbali lakini sababu kûbwa ni Wakati(Zama) na sababu ya pili utofauti Kimila.

Mfano, kile kinachoonekana NI maadili Mema Kwa jamii Moja siô ajabu kikawa NI maadili potofu Kwa jamii ñyiñgine Mathalani, Ndoa za mitala NI maadili Mema Kwa jamii nyingi za kiafrika na Mashariki ya kati lakini Kwa jamii ya kizungu siô maadili

Ukeketaji ni maadili Mema Kwa Baadhi ya jamii za kiafrika lakini Kwa wazungu NI Mila Potofu.

Mahari ni maadili Mema Kwa jamii nyingi Duniani ikiwemo jamii za kiafrika lakini Kwa jamii nyingi za kizungu NI maadili potofu.

Upotofu na usahihi mara nyingi hutokana na mabadiliko ya kizama(kinyakati) na tofauti za kiutamaduni.

Ukristo na Uislam siô maadili ya Mtanzania na Muafrika Kwa ujumla.

Huwaga nashangaa nikisikia Mtu akiwaita Wengine Hawana maadili Wakati Muda huohuo MTU huyo NI muislam au Mkristo. Muafrika mwenye maadili hawezi kuwa Muislam au Mkristo. Kuwa Muislam au Mkristo ni kukosa maadili ya kiafrika na pia ni mmomonyoko wa maadili.

Kukaidi, kukiuka, kutofuata maadili yako ya asili na kufuata maadili ya jamii ñyiñgine hiyo ndîo tofsiri halisi ya MMOMONYOKO WA MAADILI.

Maadili humong'onyolewa na vitu vingi lakini kikubwa zaidi ni Muingiliano WA tamaduni zaidi ya Moja Kwa kile kiitwacho utandawazi.

Huwezi Acha ûtamaduni wako na kuita tamaduni za Wengine ni maadili. Kitendo cha kuacha tuu na kusaliti ûtamaduni wako ni mmomonyoko wa maadili tosha.

Kabla ya Wageni kuja, waafrika walikuwa na maadili Yao Mema tuu. Hii haimaanishi hapakuwa na Mila mbaya na potofu.

Nilishasema kîla jamii inamila Zake nzuri na Mbaya. Mila mbaya kama uchawi, Kutoa Watoto kafara, unyanyasaji WA kijinsia, n.k zilikuwepo Karibu jamii zote hata jamii za kizungu zilikuwa na Mila hizô.

Jamii za kiafrika zilikuwa zinaabudu katika Mungu Mmoja kupitia mizimu ya mababu kama ilivyo Kwa Waislam na Wakristo ambao huamini katika Mungu Mmoja katika mitume na Manabii.

Kabla ya ujio WA uislam na ukristo waafrika walikuwa na maadili kuliko Zama hizi baàda ya ujio wa Dini hizi.

Ûkienda kwèñye jamii Ambazo hazina Ukristo au Uislam zina maadili ukilinganisha na jamii Zenye Ukristo na Uislam. Nenda Umasaini ndanindani, nenda Kwa Wahadzabe na watindiga Huko utajionea mwenyewe

Maadili ya kwèli hayafundishwi Kanisani au Misikitini. Maadili hufundishwa nyumbani.
Maadili yanauhusiano na asili ya Mtu na mîungu Yao.

Baadhi ya mafundisho ya kikristo na kiislam yanaweza kuwa mazuri Kwa kiwango cha juu lakini haimaanishi NI mafundisho Bora kuliko yale mafundisho ya asili Yenu, Wazazi wako, Babu zako Ambao wewe ndîo umetokea.

Maadili pia hufanyiwa matengenezo (reformations) ili yaendane na wakati Husika. Hata maadili ya kiislam na Kikristo yamefanyiwa marekebisho mengi tuu kufikia Hapo yalipo.

Maadili NI utambulisho yaani ûtamaduni. Mtu kutokuwa na maadili ya Kwao inamaanisha Hana utambulisho na Hana maadili na amemomonyoko kimaadili.

Yàani kikawaida Huwezi kuwa Muafrika Ukawa Mkristo au muislam alafu ukajiita unamaadili labda Kama hujui mantiki ya maadili yenyewe.

Unaweza Ukawa mwema na Mtu Bora Kwa kufuata tamaduni za kwetu zile zilizobora. Lakini zile zilizombaya ukaziacha.

Kûna wale watakaokuja na hoja ya Teknolojia.
Kwamba Kwa nini tunatumia Teknolojia za kigeni.
Mfano Simu au Magari n.k.
Tunaweza Kutengeneza Simu Kulingana na ubunifu wa tamaduni zetu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
Kwa Sasa Dar es salaam
 
🔹 Kitu ambacho wafia dini wasiotumia UBONGO ni kuwa dini za Kiislamu na Kikristu zilichipukia sehemu yenye utamadini sawa ( far east)

🔹 Kwa kuwa ilianzia sehemu Moja, maandiko mengi ya vitabu wanavyo viita ni maneno / vitabu vya Mungu , vimejaa Mila na destiri na tamaduni za kale za kiarabu na kiyahudi na kwa kuwa wanaoitwa manabii wote ni WA eneo hilo hilo basi Maisha Yao ya kibinaadamu yanatafsiriwa kimakosa kuwa ni maelekezo ya Mungu

🔹 Watu wameacha tamaduni zao na kuwa watumwa wa Mila za kigeni kuanzia,Mavazi ,vyakula, lugha, Nafasi ya mwanamke, MATAMBIKO ya kuchinja nk.

🔹 Kama mtu ana UBONGO wa angalau Mb Moja angejiuliza hivi kama Uislam na ukristu ungeanzia Kanda ya Kaskazini tungevaa kanzu, tungekula tende, tungesali Kilatini au kiarabu, tungesema MKATE ndio chakula Cha kwenye ibada?

🔹 Naamini dini hizo zingeanzia Kanda ya Kaskazini vazi rasmi la ibada lingekuwa mgorore wa kimasai, kinywaji bacho kingeandikwa kwenye vitabu kama ilivyo divai lingekuwa mbege ya Wachaga au dengelua ya kipare, Chakula bacho kingeandikwa badala ya MKATE ingekuwa ndizi za wachagga au makande ya wapare

🔹 Kwenye nyumba za ibada tusingekuwa tunakaa chini kama ilivyo asili ya tamaduni za Asia yote hata wasio na dini Bali kwa tamaduni za Kaskazini sehemu ya heshima Mgeni hukaribishwa kwenye kiti na kama kiti halipo litatafutwa gogo ili mheshimiwa asikae chini

🔹 Lugha ambayo tunadanganywa kama ni lugha za Mungu na hadikii lugha zingine tofauti na kiarabu na Kilatini usingezisikia kwenye vitabu Bali ungeziona lugha za kimasai, ki barabaig , ki Iraq, kichagga au kipare
 
kabla ya Ukristo kuingia tanzania kama miaka 150 iliyopita kulikuwa na maadili gani hapa kwetu ya kujivunia kulingajisha na leo hii? niorodheshee angalau matatu tu halafu tujadili kuanzia hapo, isitoshe tanzania haifwati maadili ya Kikristo vinginevyo kusingekuwa na uonevu, umaskini, wizi na unfairness ulioshamiri kila mahali …
 
🔹 Kitu ambacho wafia dini wasiotumia UBONGO ni kuwa dini za Kiislamu na Kikristu zilichipukia sehemu yenye utamadini sawa ( far east)

🔹 Kwa kuwa ilianzia sehemu Moja, maandiko mengi ya vitabu wanavyo viita ni maneno / vitabu vya Mungu , vimejaa Mila na destiri na tamaduni za kale za kiarabu na kiyahudi na kwa kuwa wanaoitwa manabii wote ni WA eneo hilo hilo basi Maisha Yao ya kibinaadamu yanatafsiriwa kimakosa kuwa ni maelekezo ya Mungu

🔹 Watu wameacha tamaduni zao na kuwa watumwa wa Mila za kigeni kuanzia,Mavazi ,vyakula, lugha, Nafasi ya mwanamke, MATAMBIKO ya kuchinja nk.

🔹 Kama mtu ana UBONGO wa angalau Mb Moja angejiuliza hivi kama Uislam na ukristu ungeanzia Kanda ya Kaskazini tungevaa kanzu, tungekula tende, tungesali Kilatini au kiarabu, tungesema MKATE ndio chakula Cha kwenye ibada?

🔹 Naamini dini hizo zingeanzia Kanda ya Kaskazini vazi rasmi la ibada lingekuwa mgorore wa kimasai, kinywaji bacho kingeandikwa kwenye vitabu kama ilivyo divai lingekuwa mbege ya Wachaga au dengelua ya kipare, Chakula bacho kingeandikwa badala ya MKATE ingekuwa ndizi za wachagga au makande ya wapare

🔹 Kwenye nyumba za ibada tusingekuwa tunakaa chini kama ilivyo asili ya tamaduni za Asia yote hata wasio na dini Bali kwa tamaduni za Kaskazini sehemu ya heshima Mgeni hukaribishwa kwenye kiti na kama kiti halipo litatafutwa gogo ili mheshimiwa asikae chini

🔹 Lugha ambayo tunadanganywa kama ni lugha za Mungu na hadikii lugha zingine tofauti na kiarabu na Kilatini usingezisikia kwenye vitabu Bali ungeziona lugha za kimasai, ki barabaig , ki Iraq, kichagga au kipare

bila ya Ukristo leo hii usingeweza kusoma na kuandika …
 
Dini imeleta mafundisho mengi sana na ndio maana watu husema tumestaarabika maana kuna watu mpaka leo wana maadili na tabia za hovyo
Tusingefuata dini sidhani kama tungekuwa hivi
Pamoja na Dini kusema Usafi ni moja katika Imani lakini bado watu ni wachafu kupindukia
Kuna uzi unaongelea kuhusu uchafu wa mama ntilie wa Tz na ukifananisha na mama ntilie wa Rwanda kwa usafi

Sisi mbali na watu kusema wana dini fulani lakini bado kuna tatizo kubwa hata maadili ni tofauti
Kwani Vigodoro na kucheza uchi ndio maadili unayoona yanafaa
Sasa akija Padri au Shehe akakemea utamshangaa?
 
Pia dini zimeleta mambo mengine ya hovyo na ajabu ajabu, nafikiria kikubwa pia ni kwamba Waafrika walichukua kila kitu kilicho kwenye dini zilipokuja na kufikiria kila yaliyoandikwa kwenye hivi vitabu ni matukio na maisha halisi(literally).
 
Nimefutrahi sana kuwa hujapinga kuwa Ukristo siyo dini.
Siwezi pinga kitu ambacho NI sahihi
Waislam wengi duniani siyo Waarabu.
Hao ambao siô waarabu wanafuata Dini ya waarabu àmbayo muanzilishi wake ni Muhammad
Uislam una asili na Mwafrika tokea Adam.
Hiyo siô Fact ni opinion za wanadini kujifagilia.
Hapa tujadili Fact.

Tunazungumzia maadili àmbayo msingi wake Mkûu ni ûtamaduni.
Kwèñye ûtamaduni kûna aspects nyingi kama Lugha, Dini, mavazi, chàkula, n.k.

Kwèñye Dini kîla jamii inadini na mîungu wake. Na hayo NI maadili ya kîla jamii.
 
Dini imeleta mafundisho mengi sana na ndio maana watu husema tumestaarabika maana kuna watu mpaka leo wana maadili na tabia za hovyo
Tusingefuata dini sidhani kama tungekuwa hivi
Pamoja na Dini kusema Usafi ni moja katika Imani lakini bado watu ni wachafu kupindukia
Kuna uzi unaongelea kuhusu uchafu wa mama ntilie wa Tz na ukifananisha na mama ntilie wa Rwanda kwa usafi

Sisi mbali na watu kusema wana dini fulani lakini bado kuna tatizo kubwa hata maadili ni tofauti
Kwani Vigodoro na kucheza uchi ndio maadili unayoona yanafaa
Sasa akija Padri au Shehe akakemea utamshangaa?
Ukristo unasimama kwenye amri kuu mbili (ambazo ni kifupi Cha amri 10 za Mungu): Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote (Amri 1-3) na mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenywe (Amri 4-10). Sasa ni ipi kati ya hizo si Mila ya Kitanzania?
 
kabla ya Ukristo kuingia tanzania kama miaka 150 iliyopita kulikuwa na maadili gani hapa kwetu ya kujivunia kulingajisha na leo hii? niorodheshee angalau matatu tu hakafu tujadili kuanzia hapo, isitoshe tanzania haifwati maadili ya Kikristo vinginevyo kusingekuwa na uonevu, umaskini, wizi na unfairness ulioshamiri kila mahali …
1.Hakukuwa na kuoana kwa watu walio ndugu wa karibu.
2. Hakukuwa na mabishano kuhusu ushoga au mahubiri yanayohusu ushoga.
3. Hakukuwa na matapeli wanaodanganya watu wawape pesa watabarikiwa
4. Hakukuwa na mifarakano ya kidini, mfano vyakula, mavazi, vinywaji n.k
5. Ndoa zilikuwa zinadumu, hakuna kuoa na kuacha hovyo hovyo.
 
Back
Top Bottom