DINI.
SIASA.
MPIRA.
Bora hata nikalale kuliko kujihusisha na mambo hayo.
Kama Mungu ni mmoja, dini nyingi ni za nini?, na kila mtu anakwambia ya kwake ndio ya kweli(utaamini vipi)
Kama kila mtu anakwambia ya kwake ni kweli, wanaaminikaje hawa watu? Kwa nini na wewe usianzishe ya kwako peke yako ndio ukaiamini ndio njia sahihi ya kumfikia Mungu?
Mwanasiasa yupo kwa ajili ya tumbo lake na wala sio wewe. Kizuri Anachokifanya kwako, ni punje tu katika bahari anayofaidi yeye.
Mwanasiasa anapotunga sheria, anatunga kwa ajili ya kumnufaisha yeye na matajiri tu, mtu wa kawaida, sheria huwa zinatungwa kukukandamiza wewe mpumbavu.
Sheria hutungwa kuwabana wengi na mara zote wengi ni ordinary people.
Tukija kwenye mpira, mtu roho inaanzaje kukuuma unapoona wanaume wenzako wanakimbiza li rubber lililojazwa pressure, eti likiingia golini kwao roho inakuuma, are you for real.
How come uuze feelings zako kwa bure kiasi hicho? Kitu afanye mtu mwingine, wewe roho ikuume. Jifunze ku control feelings bro.