safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Habarini za kutwa nyote.
Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.
Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.
Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.
Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.
Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.
Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?
Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?
Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.
Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.
Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.
Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu
Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu
Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.
Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.
Allah anasema, "Hakuna kulazimishana katika dini".
Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.
Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.
Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k.
Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani.
Nakaribisha maswali.
Naomba kuwasilisha.
===
Kwa mijadala zaidi kuhusu suala hili na marufuku nyingine Zanzibar soma:
Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika