Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Tatizo wale waliojifunza uislam vichochoroni ndo wanaona ni makosa wengine kula mchana.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Serikali itabeba dhimma ndio. Bora mtu ale huko kwa kujificha atajijua mwenyewe na Mola wake. Kuna wtt tunawakuza wakiona mambo km hayo watajifunza nini?

Nyumbani tunawafundisha kufunga wakitoka nje waone watu wanajilia ovyo tu na kuvuta sigara na kufanya uesherati wao hadharani.

Kazini tunafanya kazi na wakristo na wanakula kwa staha tu. Hamna anaowakataza wala kuwalazimisha kufunga. Kwa sababu inajulikana haijawalizimikia. Lkn hawatoki nje wakala hadharani.

Kuhusu Wagonjwa, vikongwe, wajawazito, wanaonyonyesha, wasafiri na wenye dharura hio imeshatolewa maeleze kwenye Qur'an.
 
Unafunga ili ujitakase na kujiweka karibu na muumba wako ama unafunga kwa sababu hamna namna utafanyaje ni lazma iwe hvyo?
Nafunga ili nipate kumcha Allah.

Kama hamna namna si ningekula tu kuna shida gani
 
Kwahyo leo hii wakristo wa Italia wakiweka sheria hakuna kula hadharani wakati wa kwaresma utaona wametenda haki ?
 
Swali ni moja tu.

Utaratibu wa kukataza watu kula hadharani mmeutoa kwenye Quran, hadith au muongozo upi wa kiislamu ?
 
Misikitini hatuna nafasi ya kusema.

Acha tuseme huku ambako tunayo nafasi na ujumbe utafika tu
Km wewe unaijua kweli na unaogopa kuisema hadharani halafu unachimba shimo unaingiza shingo humo ndo unapaza sauti, basi wewe unaingia kwenye kundi la wanafiki.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
wewe sio muislam kaa kimyaaa
 
Sawa,
Ila sisi ambao hatufungi basi ni vyema kutafuta sehemu ambayo haipo hadharani

Ni ustaarabu tu

Funga yako wewe inamzuia nini mtu mwingi kula, kwanza kufunga ni ibada ambayo inapaswa kuwa siri baina yako wewe na Mungu, sasa iweje ukifunga unataka kila mtu ajue umefunga na kuzuia watu wengine kula wakati wa mfungo? Huu upuuzi na ubinafsi wa hali ya juu.
 
HONGERA KAMA UNALIJUA HILO

KABALISHE HIYO TITTLE YAKO ULOIANDIKA KWENYE HABARI/NYUZI HII
Nikupe pole sana kwa sababu mpaka leo hujui kwamba kuna kauli za waislamu zinaharamisha wasio waislamu kula mchana wa ramadhani hata kama sio hadharani.

Pole sana ndugu.
 
wewe sio muislam kaa kimyaaa
Hiii πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
 
naungana na wewe mkuu
 
Bora mtu ale huko kwa kujificha atajijua mwenyewe na Mola wake.
Hapa unakusudia mtu ale nyumbani kwake asile hadharani akaonekana na watu.
Kuna wtt tunawakuza wakiona mambo km hayo watajifunza nini?
Hii hoja inanipa shida mno kwa sababu hao Wasiofunga wakila majumbani mwao si wanaishi na watoto wa kiislamu ambao wqtakuwa wanaona hao watu wakila chakula.

Au pia wajifungie mavyumbani huko wachungulie kama hakuna watoto wanaoona wakati wanakula ?

Hiyo itakuwa ni tashaddudi ambayo hata kwenye dini haijaelezwa ni matashi ya watu.
Nyumbani tunawafundisha kufunga wakitoka nje waone watu wanajilia ovyo tu na kuvuta sigara na kufanya uesherati wao hadharani.
Mkuu nyumbani mnawafundisha watoto kusali lakini wakitoka nje wanaona watu kibao hawaendi kusali muda wa sala mbona hili haliwapotoshi watoto wa kiislamu badala yake wanasali ?

Mnachotakiwa kuwwfundisha watoto ni kuwa kuna ambao hawafungi mtawaona wanakula msiwashangae wana nyudhuru na wengine sio waislamu.

Ila nadhani mafundisho mnayowapa watoto mnawadanganya kwamba huko nje hakuna mtu ambaye anakula katika mwezi wa ramadhani ndio maana mnahofia wasije watoto wakaona watu wanakula.
Imani haifundishwi hivyo.
Lkn hawatoki nje wakala hadharani.
Migahawa inafungwa.

Je ukila ndani ya mgahawa ni hadharani mpaka ifungwe migahawa ?
Au mkuu unaelewa nini maana ya neno hadharani ?
hio imeshatolewa maeleze kwenye Qur'an.
Na kuhusu wasio waislamu kula mchana katika miji hilo halijatolewa maelekezo bali ni maelekezo ya wqtu.

Why yanasibishwe na uislamu wakati Qurani haijasema mambo hayo aisee
 
Ina maana Quran ilikuja kutengua injili?
 
Hivi ni wapi kuna watu wamezuiwa kula?

Kuna hiyo fatwa hapo ambayo inakataza kabisa asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na pia zipo sehemu migahawa imefungwa kabisa kwa kusema kwamba mchana wa ramadhani hairuhusiwi kula hadharani.

Je mgahawani ni hadharani ?
Kama ni kuhusu Zanzibar hiyo ni ishu nyengine kabisa mana Zanzibar ni nchi ya Kiislamu, 99% ya watu wao ni waislamau.
Mbona zanzibar haihimizi kila mtu atakayekutwa nje muda wa sala apigwe au apewe adhabu kwa sababu huoo ni muda wa sala ?

Unaposema 99 ni waislamu hiyo 1% hawana haki ya kula mchana wakati ilikuwa waachwe tu kwa sababu hiyo 1% haina madhara yoyote hata wakila mchana itaonekana kana kwwmba wote wamefunga tu ?

Unapokua mgeni nchi za watu heshimu sheria za watu.
Sheria lazima ziheshimiwe.

Hata tunachokisema ni kwaba uislamu haujakataza popote watu kula mchana wa ramadhani kwa wale ambao hawalazimiki kufunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…