Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Waislam wenzako wa zenji hawatakuelewa Na watakuita kafir Kwa kuwatetea makafir
Sitetei makafiri bali natetea uislamu.

Leo ukisema kwamba mtume kakataza kwenye vita tusiwaue wakristo wanaofanya ibada kanisani kwa sababu hawajajihusisha na vita basi wajinga watasema natetea wakristo ila werevu watasema natetea uislamu
 
Sasa kwenye uislam wajinga ndiyo wengi....mf Zanzibar
 
Sio wajinga kwa sababu ni uislamu bali ni wajinga kwa sababu ile ni jamii,na jamii lazima kuwe na wazuri,wabaya,wajinga na werevu.

So zanzibar kila sifa utaikuta kwa sababu ndio sifa ya jamii.

Leo kungekuwa na jamii yenye wakristo 99% kama zenji basi hizo sifa pia zingedhihiri kwao.

So sioni kama ni sahihi kwa kila sifa mbaya kuwatupia waWnji eti kwa kuwa ni waislamu,bali ndio sifa ya jamii inavyokuwa mkuu.
 
Ufahamu sahihi una sifa zipi ndugu ?

Hali gani unaizungumzia...?

Una dalili? marejeo - hoja zenye nguvu zenye kuupa uzito huu ufahamu

Unazungumziaje hali ya utekelezaji wa ulichowasilisha kwenye taifa la kiislamu na taifa lisilo la kiislamu 'mchanganyiko'? kuna tofauti au
 
Dalili yenye nguvu ni kukosekana dalili ya kukataza jambo hilo ama kuzungumziwa.

Kutokuwepo kwa marejeo ya kukataza jambo ndio marejeo yenyewe.

Mtume aliishi katika taifa la kiislamu na wala jambo hilo halikunukuliwa.

Hivyo basi katika taifa la kiislamu tuishi kama alivyoishi mtume kwamba hilo halikunakiliwa watu kuchapwa na kupigwa bakora eti kisa tu wameonekana wanakula mchana wa ramadhani.
taifa lisilo la kiislamu 'mchanganyiko'? kuna tofauti au
Kama katika taifa la kiislamu hakuna ulazima wa kuwatia makosani wanaokula mchana basi katika taifa mchanganyiko ni awla zaidi watu wasitiwe makosani.
 
Dalili yenye nguvu ni kukosekana dalili ya kukataza jambo hilo ama kuzungumziwa.

Kutokuwepo kwa marejeo ya kukataza jambo ndio marejeo yenyewe.

Mtume aliishi katika taifa la kiislamu na wala jambo hilo halikunukuliwa.

Hivyo basi katika taifa la kiislamu tuishi kama alivyoishi mtume kwamba hilo halikunakiliwa watu kuchapwa na kupigwa bakora eti kisa tu wameonekana wanakula mchana wa ramadhani.

Kama katika taifa la kiislamu hakuna ulazima wa kuwatia makosani wanaokula mchana basi katika taifa mchanganyiko ni awla zaidi watu wasitiwe makosani.
Sawa, maoni yako yanajitegemea - unajiegemezea mwenyewe? au yana-support? fatawa za maulamaa 'jithad - ijithad' - kama yapo naomba ninukulie, naamini unafahamu fika kwamba dini ya uislamu haiendeshwi kwa rai na maoni ya watu ambao ni 'wajinga = awam = ignorants au wanafunzi watafuta elimu = tullab = students of knowldege'
 
Habarini za kutwa nyote.

Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.

Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.

Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.

Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?

Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.

Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.

Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.

Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu

Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu

Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.

Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.

Allah anasema..

"Hakuna kulazimishana katika dini"

Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.

Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.

Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k

Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani

Nakaribisha maswali.

Naomba kuwasilisha.
Maislamu mengi yana roho mbaya, majinga sana ndo maana mashoga, magaidi
 
Zenji kwa akina yakhee, wangepata elimu hii nadhani wange elimika Sana.
 
Sawa, maoni yako yanajitegemea - unajiegemezea mwenyewe?
Nimesema hakuna dalili ya kuadhibu watu kula mchana wa ramadhani.

Kama ipo naomba ninukulie.
au yana-support? fatawa za maulamaa 'jithad - ijithad' - kama yapo naomba ninukulie
Maneno matupu ya maulamaa itabaki kuwa ni maoni kama yangu mimi na wewe endapo hayajaegemezwa na dalili.

Ishu sio maneno ya ulamaa ishu ni je hayo maneno(fatawa) yana dalili gani ya kutegemea.
unafahamu fika kwamba dini ya uislamu haiendeshwi kwa rai na maoni ya watu
Sio kweli,dini kwa asilimia fulani lazima iendeshwe na rai na maoni ya watu.
wajinga = awam
Mjinga ni nani kwa mujibu wa sheria ya dini ?
wanafunzi watafuta elimu
Mpaka Mtume wa allah anakufa kuna hadithi ambazo umar/abubakar hakupata kuzisikia,akiwasikia watu anawataka ushahidi chini ya usimamizi mkali.

Hii ina maana ya kwamba omar mwenyewe alikuwa anaendelea kupata mambo mapya ya dini licha ya kuwa ni mtawala.

Uwanafunzi haueshi,mpaka unakufa ni mwanafunzi.

Ukisema mtafuta elimu haruhusiwi kutoa rai katika dini maana yake watu wote wasitoe rai kwa sababu unaowaita wewe wanachuoni wote ni wanafunzi.
 
ushahidi funga ni nguzo ya uislam
Wenzio wakiwa wanatimiza hyo nguzo usiwakere.
Ww ndio maana unajiita mjinga na ni mjinga kwelikweli Kwan hao waliofunga hawana watoto majumbani kwao ambao hawajafunga? Kwahiyo wanawakera? Yaani kula nile mm kukereka ww?
 
View attachment 2173451m
Huku Smz sijui imekuaje maana hata restaurant zitafungwa kisa mfungo
Niliishi Cairo, Misri, kwa miaka mitatu wakati Mwinyi (Mzee Ruksa) alikuwa balozi wetu huko na Mwinyi, Rais wa Zanzibar wa sasa, alikuwa mtoto mdogo. Zaidi ya asilimia 90 ya wananchi huko ni Waislamu. Hiyo asilimia ndogo inayobakia ambayo siyo Waislamu tulikuwa hatubugudhiwi hata kidogo kuhusu imani yetu tofauti. Kuna migahawa mitaani sawasawa na Dar. Wakati wa Ramadhani iko wazi kutwa na baa zinabaki wazi usiku mpaka mteja wa mwisho atakapoamua kuondoka. Kuna maduka ya nguruwe yanayoendesha biashara bila bugudha yo yote. Mimi nilipelekwa kwenye maduka hayo na Mpakistani, Muislamu, ambaye alikuwa anafuata dini yake haswa. Mwenyewe hali nguruwe na kufunga anafunga. Nilikuwa pia na jirani wa kutoka Nepal, naye Muislamu. Nje ya mwezi wa Ramadhani alikuwa anakwenda kunywa mpaka usiku wa manane halafu anakwenda kusubiri taxi barabarani. Mara ya kwanza polisi wa doria wakamuona wakamuuliza anatoka wapi. Akajibu anatoka ubalozini kulikuwa na dhifa. Wakamuuliza anakaa wapi, akawatajia mtaa wetu. Wakampa lift, labda kwa kutaka kuhakikisha kwamba amesema ukweli. Hakuna ghasia kabisa. Kila mtu na lwake, mradi huvunji sheria.
Nashangaa kusikia mambo yalivyo Zanzibar, leo hii. Labda Rais aulizwe anavyoikumbuka Cairo.
 
Hali kama hiyo huwa inaongeza chuki bila sababu, lakini wakiacha kila mtu awe huru hakuna mtu atawaza ubaguzi.....Nina mdogo wangu yupo ZANZIBAR wanapata shida sana kusurvive
 
Nimesema hakuna dalili ya kuadhibu watu kula mchana wa ramadhani.

Kama ipo naomba ninukulie.

Maneno matupu ya maulamaa itabaki kuwa ni maoni kama yangu mimi na wewe endapo hayajaegemezwa na dalili.

Ishu sio maneno ya ulamaa ishu ni je hayo maneno(fatawa) yana dalili gani ya kutegemea.

Sio kweli,dini kwa asilimia fulani lazima iendeshwe na rai na maoni ya watu.

Mjinga ni nani kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Mpaka Mtume wa allah anakufa kuna hadithi ambazo umar/abubakar hakupata kuzisikia,akiwasikia watu anawataka ushahidi chini ya usimamizi mkali.

Hii ina maana ya kwamba omar mwenyewe alikuwa anaendelea kupata mambo mapya ya dini licha ya kuwa ni mtawala.

Uwanafunzi haueshi,mpaka unakufa ni mwanafunzi.

Ukisema mtafuta elimu haruhusiwi kutoa rai katika dini maana yake watu wote wasitoe rai kwa sababu unaowaita wewe wanachuoni wote ni wanafunzi.
Ulichojibu sicho nilichouliza ndugu, ni wapi kwenye maelezo yangu nimegusia suala la kuwaadhibu watu 'waislamu au wasiokuwa waislamu' wasiofunga mchana wa Ramadhani? naomba yanukuu kisha nionyeshe
 
Swali langu lililenga maoni uliyowasilisha kwenye kichwa cha habari na si vinginevyo, heading peke yake tu
 
Jawabu langu mkuu ni kwamba hakuna dalili ya kuwaadhibu au kuwazuia watu kula mchana hadharani maadamu hawajalazimishwa na sheria kufunga.
 
Ulichojibu sicho nilichouliza ndugu, ni wapi kwenye maelezo yangu nimegusia suala la kuwaadhibu watu 'waislamu au wasiokuwa waislamu' wasiofunga mchana wa Ramadhani? naomba yanukuu kisha nionyeshe
Sawa ndugu.

Naomba uliza swala lako vizuri pengine sikuelewa.
 
Back
Top Bottom