Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Kuna siku nilisikia msikitini ikisifiwa tende kwamba ni tunda bora kuliko yote hii kwa mwafrika yeyote mwenye kufikiri ni tusi kwake.
 
Hahahahha aiseeee.

Kwa nini ?
 
Mimi nimesikitika kuona Zanzibar mpaka sehemu za vyakula zinafungwa, kula mahali ambapo ni pa wazi hairuhusiwi! Inabidi zanzibar iitwe dora la kiislam na warudi kwa waOman.
 
Tuwaelimishe waachane na misimamo feki isiyowafikisha popote.

Kuna mambo ya kutilia mkazo katika jamii kama vile wanawake kutembea wamevaa vibaya wakionesha maungo yao,kudhibiti ushoga n.k
 
Ukijua kuwa hii DINI imeanzishwa na WA Roman Catholic Iko chini ya Papa hata HUWEZI KUUMIZA Kichwa.

Roman Empire.
 
Nasubiri siku hii mada ianzishwe ili nipate kujifunza katika hii ishu
 
Ukijua kuwa hii DINI imeanzishwa na WA Roman Catholic Iko chini ya Papa hata HUWEZI KUUMIZA Kichwa.

Roman Empire.
Kuna uzi sijui uko wapi unaelezea hii inshu naomba unitag kama unaujua
 
Habarini za kutwa nyote.

Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.

Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.

Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.

Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?

Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.

Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.

Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.

Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu

Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu

Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.

Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.

Allah anasema..

"Hakuna kulazimishana katika dini"

Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.

Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.

Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k

Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani

Nakaribisha maswali.

Naomba kuwasilisha.
Wejamaa ukisifiwa ndo unaona siiifaa akati vitu viko wazi kabisa nchi zote za waslamu wengi ilo swala la kula hazarani mchana no no
 
kuna tofauti ya waisilamu na uisilamu,know the difference
 
Habarini za kutwa nyote.

Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.

Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.

Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.

Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?

Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.

Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.

Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.

Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu

Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu

Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.

Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.

Allah anasema..

"Hakuna kulazimishana katika dini"

Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.

Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.

Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k

Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani

Nakaribisha maswali.

Naomba kuwasilisha.
Kudadadeki yaani hela ni zangu na kula nakula kwa raha zangu halafu aje mtu kunikamata kisa eti nakula mchana? Haki ya nani huyo mtu itabidi aombe Mungu wake, nitamkung'uta vibaya sana na kumshikisha adabu. Hapa ni Tanzania si jehanam, nani anayekatazwa kula?
 
Watu wanakatazwa kula mzee.

Nenda zanzibari huko utayashuhudia.😀
 
Zanzibar kuna uonezi tu mbona watalii wanatembea na chupa zamaji mkononi wakinywa mchana kweupe au kwa kuwa ni wazungu?
Kwa kuwa ni wazungu kaka.

Fanya wewe mswahili utanangwa
 
Back
Top Bottom