Uislamu na Ukristo ndiyo vimeleta ubaguzi wa kijinsia, Afrika haikuwabagua wanawake

Siyo dini tu mkuu huyo ana lenga mbali. Macho yote kwa beberu. Anamlaumu beberu kwa lolote. Mark my words - lolote.
Kuna tofauti ya kusema historia ilivyo na matokeo yake kwetu leo na kulia wakoloni hivi na vile. Inaonekana unatabia ya kulaumu 'mabeberu' maana umekazania hiyo point. Soma historia yako vinginevyo utakuwa unalaumu wengine kila siku kwa yanayokupata.
 
Ukisoma title ukaelewa utaona kwanini nomezungumza mfano wa Shehe.

Na ukisoma mada hadi mwisho utaona mifano mingine inayoonyesha kwanini nasema hatukuwa tunabagua wanawake.
Haya kwa watakaoelewa.
 
Haya kwa watakaoelewa.
Ngoja nikusaidie kuelewa. uwepo wa Matrineal Societies unaonyesha kuwa katika waafrika mwanamke aliweza kuwa kiongozi.

Pili ni uwepo wa gender kwenye hizo lugha. Utakuta kiarabu, kiebrania na kiingereza wanajinsia kwenye lugha zao. Vitu kama She/He/Him/her/his. Lugha za kiafrika kama kiswahili hakuna hili.
 
Katika historia ya Tanzania kuna mtu aliyeitwa Kisabengo. Kisabengo alikuwa ni mtumwa wakati ambapo Sultani wa Zanzibar anatawala Zanzibar na pwani ya Afrika mashariki. Alikuwa ni mtu mwenye nguvu sana. Baada ya muda akatoroka atumwa akiwa na watumwa wengine akiwa kiongozi wao.

Baada ya kutoroka akaanza kuwa mbabe wa kivita, akivamia na kupora maeneo ambayo leo ni mikoa ya Pwani na Morogoro. Kokote lilikosikika jina Kisabengo watu waliingiwa na hofu kuu. Baadaye akaanzisha mji. Aliuita mji huo Simbamwenni/Simbamwene. Mji aliojenga leo ndiyo Moro Town. Ulikuwa mji wa maana sana. Ulikuwa na Kuta za mawe. Minara miine ya ulinzi iliyojengwa kwa mawe na ulilindwa na maaskari wenye magobole. ulijengwa kando ya mto na ulikuwa na milango minne ya mpingo kila pande, milango yake ilipambwa vizuri sana. Mji ulikuwa moja ya vituo muhimu ya misafara kutoka bagamoyo kwenda Ujiji kituo.

Huyu Kisabengo alikuwa na binti yake ambaye alimwita Simbamweni. Alimpenda sana binti yake. Hata alipokufa alimuachia usultani wa mji ule. Kipindi H. M Stanley anapita kwenda unyanyembe aliweka kambi Simbamwene. Alistaajabu uzuri wa mji ule uliokuwa ukiongozwa na mwanamke. Askari wakakamavu wenye silaha wakimtii.

Stori hii inaonyesha jinsi Waafrika hatukua na habari za ubaguzi wa kinjinsia wala kuwadharau wanawake. Ushahidi mwingine ni lugha. Lugha yetu haina habari za She/He/Her/Him. Haibagui jinsia.

Ushahidi mwingine ni uwepo wa Matrineal Societies. Huko mikoa ya kusini urithi ulikuwa unapita kwa mwanamke, hata jamii nyingine kama wanyakyusa utakuta ni semi -matrineal. Na hii habari ya matrineal ipo sehemu nyingi africa.

Sasa zikaja dini za kutoka Mashariki ya kati na utamaduni wa watu wa eneo hilo kudogosha na kudharau mwanamke. Wakatulisha maneno kibao kibao na kutufanya hata sisi tuanze kufikiri kama wao. Hizi dini za middle east ndiyo zimefanya muafrica aanze kudharau mwanamke.
Ilikuwa karne ipiii iyo mpaka kisabengo namiliki magobore kwenye ulinziiiii
 
Africa hii hii ambako wanawake walipigwa na kukosa sauti?
Huku huku ambako wanawake hawakufanya chochote kwa maamuzi yeyote
 
Historia uliyoandikiwa ndiyo inataka kukuaminisha hivyo.
 
hujasikia shehe anasema mwanamke hafai kuwa Rais.
Hayo ni maneno yake binafsi,sio ya dini.Mwanamke katika dini zote mbili kapewa nafasi kubwa,katika uislamu Bi Khadija,Bi Aisha,Asma bint Abubakar,Maryam(mama wa Nabii Issa),Bi Asiya(Mke wa Firaun),Balkiss(alikuwa mtawala),na wengine wengi,ni mfano bora wa kupewa nafasi kubwa katika uislamu.
Ukija katika ukristo,Mariya(mama wa Yesu),na wanawake wengi tu,wamepewa nafasi kubwa kubwa.Wapo wanawake karibia mia,wametwajwa ndani ya Biblia,yupo mwanake anaitwa Abia(alikuwa mfalme(malikia) ,si chini ya miaka 25.Wapo kina Anna,Abagail na wengineo,kama sijakosea majina yao.
 
Katika historia ya Tanzania kuna mtu aliyeitwa Kisabengo. Kisabengo alikuwa ni mtumwa wakati ambapo Sultani wa Zanzibar anatawala Zanzibar na pwani ya Afrika mashariki. Alikuwa ni mtu mwenye nguvu sana. Baada ya muda akatoroka atumwa akiwa na watumwa wengine akiwa kiongozi wao.

Baada ya kutoroka akaanza kuwa mbabe wa kivita, akivamia na kupora maeneo ambayo leo ni mikoa ya Pwani na Morogoro. Kokote lilikosikika jina Kisabengo watu waliingiwa na hofu kuu. Baadaye akaanzisha mji. Aliuita mji huo Simbamwenni/Simbamwene. Mji aliojenga leo ndiyo Moro Town. Ulikuwa mji wa maana sana. Ulikuwa na Kuta za mawe. Minara miine ya ulinzi iliyojengwa kwa mawe na ulilindwa na maaskari wenye magobole. ulijengwa kando ya mto na ulikuwa na milango minne ya mpingo kila pande, milango yake ilipambwa vizuri sana. Mji ulikuwa moja ya vituo muhimu ya misafara kutoka bagamoyo kwenda Ujiji kituo.

Huyu Kisabengo alikuwa na binti yake ambaye alimwita Simbamweni. Alimpenda sana binti yake. Hata alipokufa alimuachia usultani wa mji ule. Kipindi H. M Stanley anapita kwenda unyanyembe aliweka kambi Simbamwene. Alistaajabu uzuri wa mji ule uliokuwa ukiongozwa na mwanamke. Askari wakakamavu wenye silaha wakimtii.

Stori hii inaonyesha jinsi Waafrika hatukua na habari za ubaguzi wa kinjinsia wala kuwadharau wanawake. Ushahidi mwingine ni lugha. Lugha yetu haina habari za She/He/Her/Him. Haibagui jinsia.

Ushahidi mwingine ni uwepo wa Matrineal Societies. Huko mikoa ya kusini urithi ulikuwa unapita kwa mwanamke, hata jamii nyingine kama wanyakyusa utakuta ni semi -matrineal. Na hii habari ya matrineal ipo sehemu nyingi africa.

Sasa zikaja dini za kutoka Mashariki ya kati na utamaduni wa watu wa eneo hilo kudogosha na kudharau mwanamke. Wakatulisha maneno kibao kibao na kutufanya hata sisi tuanze kufikiri kama wao. Hizi dini za middle east ndiyo zimefanya muafrica aanze kudharau mwanamke.
Mkuu nadhani jeshini hakuna dini.
Naomba kujua kwanini asilimia kubwa ya hostile missions kama rotations maporini nk wengi au wote huwa ni wanaume na si wanawake?!
 
Ni wasomali sio waarabu.
Hivi nyinyi mnaojifanya waarab koko mmesoma kweli au mnakariri tu vitu bila kujuwa.....acheni story za vijiweni. Hizi nchi zifuatazo ni za wapi > Jordan, Iraq, Syria, Oman, United Arab Emirates and Qatar?
 
Back
Top Bottom