Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wanahistoria, wachambuzi na watu wengine wengi mnaopenda kufuatilia maendeleo katika bara la Africa mnapaswa kutilia maanani madhara, hasara na legacy ya ujamaa katika kufifisha maendeleo ya nchi za Africa zilizofuatisha mfumo huo wa uchumi.
Nchi nyingi za Africa wakati zinapata uhuru miaka ya 1960 zilipata uhuru na zikarithi uchumi wa wakoloni uliokuwa ukikua.Viwanda vilivyokuwepo vilikuwa vikifanya kazi kwa ufanisi, hali ya biashara ilikuwa nzuri, sekta ya kilimo ilikuwa nzuri inayokua huku ikiweza kulisha raia wote bila kuagiza chakula nje, hifadhi ya fedha za kigeni ilikuwepo, huduma za kijamii nazo zilikuwa zikisonga mbele n.k
Punde tu baada ya kupata Uhuru miaka ya 60 baadhi ya viongozi kama Nkuramah, Leopold Senghor, Sekou Toure, Julius Nyerere, Kaunda, Milton Obote, Mengistu Haile Mariam(Ethiopia haikuwahi kuwa koloni)na wengine wakaja na sera zao za ujamaa. Japo zilitofautiana lakini zilifanana katika mambo muhimu kama "nationalization", vijiji vya ujamaa, chama kimoja, na kutoruhusu uwekezaji kutoka nje.
Kitu walichosahau au ambacho hawakuzingatia viongozi hawa ni kwamba Africa kwa asili yake ilikuwa ni bara la soko huria au la kibepari tangu karne na karne. Kabla ya ukoloni na hata baada ya wakoloni kuja. Ujamaa ulioletwa miaka ya 1960 hadi 70 ulikuwa kitu kigeni sana kwa raia wa bara hili. Uliharibu na kuvuruga mfumo mzima wa soko huria uliojengeka kwa karne nyingi.
Ujamaa ulileta rushwa, uzembe, matumizi mabaya ya rasilimali na kodi za wananchi. Uliondoa hata uhuru wa ukosoaji ambao ulikuwepo wakati wa ukoloni! Matokeo yake kadri miaka ilivyosonga mbele uchumi wa hizi nchi na nyingine nyingi za Africa ukadorora sana, ukawa mbovu, viwanda vikafa na vingine vikawa havianzishwi, biashara ikasinyaa, uhuru wa raia ukaminywa, migogoro ikachachamaa, umaskini ukazidi kutapakaa.
Ujamaa ni mfumo ovu sana uliochangia pa kubwa kuliharibu bara hili zuri. Unapaswa kulaaniwa na mtu yeyote anayetazamia siku nzuri za usoni katika bara hili.
Hii ni kwa ufupi sana.