SoC02 Ujamaa(ubuntu) na ajira ya muda ni mkombozi wa uchumi wa Vijana kuelekea kwenye uchumi wa Kitaifa na kujitegemea

Stories of Change - 2022 Competition

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
UTANGULIZI.

Ujamaa nitakaojikita nao ni (UBUNTU).

Rejea (Kamusi ya karne ya ishirini na moja 21 Toleo jipya uk wa 555)

Ubuntu ni mfumo katika jamii unaowawezesha wanajamii kuishi kwa kushirikiana katika kila jambo.

Ninaye rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu kutokana na safari yangu ya kielimu, nilipokuwa kwenye pirikapirika zangu nilipigwa na butwaa nilipomkuta kwenye duka kubwa la nguo na kunisimulia kisa chake mpaka kuwa na hilo duka ninaloliona na kunivutia, ni upendo alioupata kwa jamaa yake aliyehishi naye nakuziona ndoto zake baada ya kutembeza bahasha kwa miaka mitatu bila kuambulia kitu kulinga na kile alichokisomea.

Rafiki yangu alinidokeza shauku yake ya kuendeleza mnyororo huo pale duka lake litakapozalisha duka lingine kwani hilo ni deni la kuupanua myororo kwa watu yaani kuwafanyia hisani vijana anaowaona na bahasha mkononi kwani alipitia magumu na Machungu.

Katika kupembua kwangu alichokivuna kutokana na shughuli hii ndani ya miaka miwili ni urahisi wa kujipatia mahitaji yake ya kimsingi kama vile chakula bora, mavazi nadhifu na kile anachodunduliza katika kulinda mtaji na faida anayoitunza ili kutimiza ndoto zake.(Tanzania tunaitaji sera ya ubuntu kwa maendeleo bila ya ubaguzi wa kikanda.

Kauli ya “uchawa” isifishe mazuri ya ujamaa kwani ikikua itadumaza watu kwa kuwabwetesha huku ikimfanya mwanaujamaa kujenga roho ya umimi na kuona kile alichonacho ni chake binafsi bila ya kufikiria wahitaji ndani ya jamii.

Mfano mwingine halisi wa ubuntu ni kitendo cha jamii yangu kujichanga mfukoni ili nipate Elimu ya juu na bila ya huo ujamaa pengine ningelikosa au ningechelewa kupata haya maarifa niliyonayo hadi sasa, vilevile nimeshuudia ujenzi wa miundombinu bora ya shule kutoka kwa watangulizi kwa kujishika pamoja mifukoni na wadau wengine wa kijamaa, hii ni ishara ya ukuzaji wa maendeleo kwenye ngazi ya kijamii.


AJIRA ZA MUDA KATIKA UKUZAJI UCHUMI WA KIJANA.

Katika kupunguza makali ya maisha kwa vijana yanayotokana na lundo la ukosefu mkubwa wa ajira ninaona suruhisho lake ni suala la uwepo kazi za muda kutoka Serikalini na taasisi binafsi kuliko kusubiria zile za kudumu.

Ajira hizi za muda hazitapunguza tu umaskini wa kupitiliza kwa vijana bali zitaendeleza kulinda taaluma za vijana na uwezo wao yaani zitawapatia uzoefu kazini bila ya kuwaacha tu mtaani huku maarifa yale waliyoyapata vyuoni yakiendelea kuwachachia ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona kijana anakosa kazi kwenye taasisi au kampuni kwa kigezo cha ukosefu wa uzoefu kazi, wakati ndio tu anatoka chuoni je kwanini uzoefu wa mafunzo kwa njia ya vitendo authaminiwi, taasisi zinasahau kuwa kupitia wao au kampuni mhitimu anaongeza huo uzoefu kulingana na maarifa aliyonayo kutoka chuoni, “ kila taasisi ikitumia kigezo cha uzoefu kazini na kuwatupilia mbali vijana, huo uzoefu wataupata wapi?”. Tuamini vyuo vyetu na wakufunzi tulionao ili nao waone umuhimu wa kuwaandaa vyema vijana ili wasiende kuwatia aibu na kuharibu taswira ya chuo.

(“”Itafana kila mwaka tasisi binafsi, kampuni au serikali ikituma maombi ya moja kwa moja vyuoni huku wakiomba majina ya wahitimu wanaofanya vizuri ili kuwapatia ajira za muda ili wapate kile cha kuanzisha maisha ya kujitegemea hapo baadae””) huku wakiwafanyia usaili (upimaji) wenye na wajiridhishe na uwezo wa hao vijana na kuzuia mianya ya kuchaguliwa kwa kujuana na rushwa.

Ajira ya muda itasaidia kuwanyanyua vijana wenye mitaji midogo katika kuikuza na kuwainua pale zitakapowalenga : mfano wa ajira ambazo zimewainua baadhi ya vijana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ni Zoezi la uandikishaji na usimamizi wa wapiga kura, zoezi la uadikishaji wa anwani za makazi zilizofanyika mwaka huu 2022, sensa ya idadi ya watu na makazi nimeona shauku ya vijana.


MKAKATI MWINGINE.

Nchi ya Tanzania inapaswa kuwa na ; “NYUMBA YA MALEZI” Kwa vijana wanaotoka vyuoni kutoka kila mkoa ikiwa ni kuwaandaa vijana watakao tekeleza ubuntu, Viongozi bora kimaadili na Wazalendo pia vijana wenye nguvu ya ushawishi na wabunifu, mfano Tanzania tangu tumepata uhuru bado hatujawa na vazi rasmi la nchi wakati tunao wabunifu na watu wenye ushawishi wa kutumia utandawazi kupitia mitandao ya kijamii katika kutangaza mitindo mbalimbali kutoka nje, wabunifu kutoka kwenye nyumba ya malezi wabuni vazi la taifa kwa watoto, vijana, watu wazima na wazee na zitengenezwe nchini na zipatikane kwa gharama nafuu (ili tumalize hitaji la mavazi nadhifu). Si haya tu ndiyo yatakuwa mafanikio tu kwa vijana bali itakuza maadili mema kwani kila kijana atatamani kuwa barozi mwema wa jamii yake na kuwa mtu wa mfano kwa kizazi kilichopo na kile kijacho. (Tanzania tunaitaji sera ya Ubuntu).

Nyumba ya malezi itoe wabunifu na wasanifu wa majengo. Yaani ramani ya nyumba kwa kila familia au mtanzania wa pato la chini, kati na juu kwa gharama zote hadi kukamilika ili tumalize hitaji la (makazi bora) huku serikali ikiratibu suala la bei elekezi za vifaa vya ujenzi na unafuu wa upatikanaji wake kulingana na eneo la kijiografia. (Twaweza kuwa wanaubuntu) kulingana na hali zetu za kimaisha mbali na utofauti uliopo kiuchumi yaani Viwango/ngazi. Mfano wa nyumba hizi za malezi zitumie mifumo ya “Big brother Afrika na “Big brother nigeria” kwani zimekuwa nguzo kubwa ya kuwaandaa vijana katika kubuni mawazo chanya yenye kuchagiza maendeleo ya vijana na mataifa yao kwa ujumla na kuzitangaza nchi zao na vivutio vilivyomo.

“Ubuntu uliokomaa unaweza pia kukuza uchumi wa nchi”
Mfano halisi wa ubuntu kupitia michezo.

Hapa nchini Tanzania kuna kituo cha televisheni kilichobuni wazo la “ nani zaidi ?” kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu ndani ya wiki mbili Timu (A) ilikusanya zaidi ya milioni mia moja na timu ( B) ilikusanya zaidi ya milioni hamsini kutoka kwa wanajamii. Serikali ikibuni mawazo kama haya ya ubuntu kulingana na vyanzo vya mapato vilivyopo, nchi yetu ya haiwezi kukosa Viwanda vya mavazi ya nguo rasmi, za kawaida na zile za kimichezo.

Bado nchi yetu ya Tanzania inahitaji utekelezaji wa sera ya ubuntu kuelekea kwenye kujitegemea kwani mshikamano wa pamoja katika kuinuana utakuza maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye familia hadi kufikia kwenye ngazi ya kitaifa.


(Picha kwa msaada wa mtandao). Katika kuonyesha nguvu ya ubunifu na ushawishi.​
 
Upvote 6
Mkuu

Naona umekomalia "matusi" too much,are you getting paid?

Matusi yapo kwenye jamii,kila sekunde,why getting this emotional?

Mjadala ni verbal exchange between human beings with potential of being offensive which is allowed.

Mjadala kugeuka physical it is another dimension which is not allowed since it is not benefial to the parties involved

To begin with,matusi yangu ni yepi hasa?

Kama nimetukana matusi 2 au 3 au 10,na wewe nirudishie idadi hiyo hiyo to make yourself happy then tuendelee mbele.....
 
Matako ya Ubungu na ujamaa wa kipumbavu...
Hizi ni lugha zisizo faa kutolewa na mtu mzima mwenye kujiheshimu .
Nyerere na washenzi wenzie
Pia hii haifai.
still motherfvckers dont understand!
Nayo pia hii haifai.
- kuongea lugha za matusi sio sifa nzuri za kujisifia kwa mtu mzima anayejitambua na sio wote wanapenda kurudisha tusi kwa tusi hapana haipo hivyo . Ila wewe unayetoa lugha hizo mbaya inabidi ujitafakari kweli Kama mtu mzima heshima yako ipo wapi Kama unashindwa kuheshimu wengine? Na sio kila aina ya lugha inapaswa kutolewa kila sehemu la hasha inakupaswa wewe Kama mtu mzima kutazama na hadhira eneo husika ndio maana hauwezi kwenda kanisa, ofisi za kiserikali , maeneo ya kiserikali, kwenye makazi ya watu , shuleni, kanisani , msikitini na sehemu zozote zenye heshima na wewe kuanza kuongea lugha za kukera zilizojaa matusi hakika hautaeleweka na jamii. Hizo lugha chafu zilizo jaa matusi hutolewa na watu wasiojitambua kuwa wapo rika gani , watu wasio na elimu, walevi wa kupindukia, watumiaji wa madawa ya kulevya, wezi , majambazi na hata watu wengine wenye matatizo ya akili[ vichaa] . Sasa inakupasa kujitafakari wewe ni mtu wa namna gani na aina ya maneno machafu unayotoa na kuchukulia kuwa ni lugha za kawaida je kweli hayo maneno yana afya katika mijadala hii ya heshima Kama ya mtoa mada? 🤔
 
Hizi ni lugha zisizo faa kutolewa na mtu mzima mwenye kujiheshimu .
Mkuu...hii kazi ya kulazimisha wanadamu watu wazima kama wewe waongee lugha unazotaka wewe ni waste of your time

Toa elimu hapa,matusi au unachokichukia achana nacho acha kujifanya msahihisha wanadamu humu,unapotea
 
Too bad aiseee

I cant help you with this

Wewe chambua unachotaka achana na matusi...then jibu hivyo unavyoona ni point

Mengine achana nayo

Halafu punguza unafiki
 
Mkuu...hii kazi ya kulazimisha wanadamu watu wazima kama wewe waongee lugha unazotaka wewe ni waste of your time

Toa elimu hapa,matusi au unachokichukia achana nacho acha kujifanya msahihisha wanadamu humu,unapotea
Sawa mkuu umeshinda. kuwa na siku njema.
 


Ndugu yangu,
Rejea vizuri mada yangu ya ubuntu
"ninegusia pia kuwa Ubuntu unaweza kufanyika kulingana viwango/ngazi tulizomo" nikiwa na maana kwamba tunachohitaji ni maendeleo/Maisha mazuri ili kuepuka uduni yaani umaskini uliopitiliza. nikilenga watu wa pato la chini maendeleo yao ya julikane ni yapi nyumba bora iweje au ni ipi, mavazi bora yaweje, hata kwa ngazi ya kati hadi kufikia ngazi ya juu.

Mfano;Teknolojia ni mfano mzuri wa Ubuntu nini maana ya ubutu ; Ubuntu ni mfumo wa kijamii unaowawezesha watu (wanajamii) waishi kwa kushirikiana kwa kila jambo. Nimerejea kwenye kamusi ili usije kusema huo ni mfumo wa tarakilishi (kompyuta) na si watu na jamii.

Nitatumia mfano wa simu janja(smart phone). kukufumbua macho.

Hawa wagunduzi wa simu janja walihitaji jamii yote (dunia)iishi kwa kushirikiana kimawasiliano na utendaji kazi, wakaona kiunganishi ni mtandao kupitia simu au ngamizi (kompyuta). dunia iwe pamoja.

Waliona vitu hivi vinaweza kuwalenga watu walio na kipato cha juu huku lengo lao likiwa ni kuwaleta watu wote pamoja bila ubaguzi kwenye mawasiliano na utendajikazi.

Wakaanza kuraisisha jambo hili kwa aina za simu na viwango, lakini wote wanashiriki pamoja kupitia mtandao wa simu janja, mfano kuna simu janja ndogo ya elfu hamsini, laki moja hadi milioni. Mbali na utofauti huu mtu mwenye simu janja ya laki moja anyimwi nafasi ya kushiriki pamoja kimaoni hata baadhi ya utendaji kazi na mtu mwenyewe simu janja ya milioni.


je unajua kupitia huu umoja wa kimtandao kama sehemu ya kuleta watu pamoja wanaingiza kiasi gani pesa au wananufaika vipi kwa kile wanachokiona na kupata pengo la mahitaji na kuyaboresha.

Utani kidogo ......."Morison alipokuwa Yanga alikuwa anajinasibu kwa kusema"
"Sisi tuna watu" hii kauli ni pana.
Mwalimu J. K. Nyerere aliona mbali uenda aliangushwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi, mpe heshima yake kuiweka nchi huru inatosha. kupitia Ubuntu leo tuna uhuru alikaa na watu wakaongea kwa pamoja kisha yeye akasimama kama mwakilishi. huku nyuma akiwa na jopo la watu.

Dhana yangu ya sera ya ubuntu ni kumuonjesha hata maskini utamu wa maisha/maendeleo hata kwa ngazi yake hiyo aliyonayo. Hata mtoto wa kabwera aseme sisi tuna nyumba ya vyumba viwili lakani ina vigae, tuna umeme na kaka ataleta video(televisheni)
hapa tutakuza watoto wadadisi kuanzia vijijini hadi mijini.
 
blah blah blah

Hujui unachoongea

Huwezi kufananisha process ya kujenga specific output kama mchezo wa mpira wa miguu na SOCIALISM..hujui lolote au kama ulisoma From Three ulifeli

Please go back to Form Three usome upya ndugu
 
blah blah blah

Hujui unachoongea

Huwezi kufananisha process ya kujenga specific output kama mchezo wa mpira wa miguu na SOCIALISM..hujui lolote au kama ulisoma From Three ulifeli

Please go back to Form Three usome upya ndugu
Ndugu,
Usitake niseme wewe ulikuwa miongoni mwa watoto waliowasumbua walimu wa vidudu.
DHANA YANGU IMEJIKITA KWENYE UBUNTU
Nimekupa urejee hata kwenye kamusi

Nimetumia neno 'ujamaa"
Kwa misingi huu
1. Ukwasi wa lugha
Ningesema Ubuntu moja kwa moja ningewaacha wengi mbali kwani huu ni msamiati mpya hauko masikioni mwa watu.
Ningesema moja kwa moja ujamaa
Ungelishibisha hoja zako zilizojaa takataka.
Sema wapi kuna ukakasi nikupe sukari itakayokuponya na hili gonjwa lako.
 
Kila uchao napawaza hapa kama suruhu ya lundo la ukosefu wa ajira.

1. Watakao maliza muda wao watakuwa bado wanayo nguvu ya uzalishaji kwani watakuwa bado hawajaufikia uzee ambao unaweza kuwa tatizo kwenye utendaji kazi pale watakapoanzisha miradi mbalimbali.

2. Ita kuwa rahisi Idadi ya watu wengi kuifaidi "keki ya taifa". Kwani zitakuwa kama mbio za kijiti. "Utumishi wa kupokezana.

3. Mnyororo wa ajira utakuwa mrefu Sababu mtumishi aliyemaliza kazi yake ya muda atakapoanzisha mradi anaweza kuajiri vijana "vibarua" kuanzia wawili au zaidi.

4. Itakuza taifa la wachapakazi kwani kila mmoja atajiaandaa kuwa mtendaji kazi ata baada ya kumaliza utumishi wa muda mfupi.

5. Italeta tabasamu kwa vijana lililopotea huku wakikwepa vitu hatarishi kama vile matumizi ya dawa za kulevya, pombe nk ili kulinda haiba na taaluma zao kwani muda mfupi ujao wao watakuwa watumishi.

6. Italeta chachu ya mabadiliko kwenye njia za utendakazi kwani maarifa mapya yanayoibuka kulingana na sayansi na teknolojia yatakuwa yanatumika kuliko kuendeleza mbinu zilezile za kizamani zinazotumiwa na watumishi waliokaa muda mrefu kazini hata zisizokuwa na tija.

7. Tanzania itakuwa nchi ya kuigwa na mataifa mengine kama nchi yenye maono ya kona kila mwanchi anakuwa kwenye myororo wa kufikiwa na maendeleo kupitia ajira na kujiajiri.
Hakika ikipitishwa kuwa sera yenye kutekelezwa italeta tija kubwa sana hapa nchini isipobezwa na wenyeuchu wa kujilimbikizia mali za umma kupitia utumishi wa muda mrefu.
 
Safi Sana. Ni kweli kabisa kwa 100% hiki unachosema . Inabidi serikali na wadau mbalimbali wenye nguvu hapa nchini walipigie kelele jambo hili maana tatizo la ajira kwa vijana wengi wasomi limekuwa Kama wimbo wa taifa. Jambo la muhimu ni serikali kuchukua maamuzi magumu na kuchagua njia mbadala Kama tulizo jadili hapa na kuangalia ni kwa namna gani zinaweza kuanza Kutumika hapa nchini ili kuokoa wimbi la taalumu zinazopotea na kuozea mitaani.
 
Umenena vyema.
 
 

Attachments

  • IMG_20220806_083930_686.jpg
    1 MB · Views: 7
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…