Kwa hiyo ni kwamba Udini uliingia baadae katika TANU? na kisha CCM? Kwa sasa Maaskofu na Mapadre wamekua na nguvu sana kiasi cha kupeleka Kanisani mambo ya Nchi wanapata wapi mamlaka haya!?
MOJA; KUKEMEA SIO KWAMBA KULIKATAZWA -TENA JKN AMESEMA KABISA KAMA TUNAKOSEA KATIKA KUTETEA WANAONYONYWA MTWAMBIE - MSIKAE KIMYA
Hata katika hii Hotuba anasema sababu ya Makanisa kupoteza Sifa yake nzuri huko Ulaya ni sababu ya Makanisa Ku-side na Wanyonyaji na kuwa Wanyonyaji hivyo watu kuona kwamba Hawafai......
NANUKUU KUTOKA KWENYE NUKUUU
Kuna Mataifa mawili Sasa". Katika nchi ile ile ? moja kuna mataifa mawili — kuna kataifa kadôgo ka mabwana kanashiba, kanatakata, kana jeuri, na taifa kubwa la wafanyakazi hawana kitu maskini, hali yao inazidi kuwa dhalili.
Manung'uniko lazima yaanze. Yakaanza. Yakaanza. Dhahiri katika nchi zile, imegawanyika sehemu moja inaonea, dhahiri inaonea, na sehemu moja inaonewa. Wafanyakazi lakini jasho lao linapotea hivi hivi. Manung'uniko yalikuwaya ? Lazima. Lazima. Mtu hakubali akae ananyonywa hivi hivi. Halafu anyamaze tu asiseme. Kwa hiyo, dhahiri watu walianza kunung'unika? Watu walianzaz kunungunika kwa sababu wafanyakazi dhahiri wanadhulumiwa na matajiri wao. Nasema kelele hizi Ulaya zikawa nyingi sana katika karne mwisho wa karne iliyopita. Nyingi sana!
Sasa, watu wanazungumza juu ya . dhuluma; watu wanazungumza juu ya dhuluma. Watu wengi wananung'unika wanasema wanadhulumiwa na wachache. Dhuluma jambo baya.
Waelezaji wa mema na mabaya duniani, waliotumwa waeleze mema na mabaya duniani angalao wenyewe ndivyo wanavyotuambia — ni wakubwa wa dini. Wasimamizi: "Msifanye hivi — hivi ni vibaya; msifanye hivi hivi -ni vibaya. Fanyeni hivi hivi ndivyo vizuri.. Inafika wakati ambapo taifa limegawanyika katika sehemu mbili: watu fulani wananungunika - tena wengi wananung'unika kwamba wanaonewa, na wachache wanawaonea. Kilio kikubwa si kidogo hicho.
Inapofika hapo Watu wa dini — nyinyi mnatazamiwa sauti yenu iwe ya wazi wazi. Si ya mashaka mashaka, Kama ni mazungumzo kati ya haki na dhuluma, wakubwa wa dini hawatazamiwi kunongona; au kuwa na mashaka mashaka; lazima waseme dhahiri: "Mnaonea nyinyi; mnawadhulumu hawa" Lakini jamaa wanaojua historia hii ya Ujamaa Ulaya wanajua kwamba kauli ya Makanisa haikuwa ya wazi wazi, Makanisa yalibabaika. Makanisa. ya Kikristo yalibabaika babaika katika jambo hili. Makanisa ya Ulaya yalibabaika kidogo katika jambo hili la dhuluma Kwa nini yalibabaika, wanajua wenyewe.
Lakini wengine tunadhani kwamba ingawa dini ni ya Mungu; anawapa Mitume wake: "Kawafundisheni binadamu kadha kadha". Lakini' hao Mitume wanaotumwa, hao ni binadamu hao. Kwahiyo pamoja na kueleza dini yenyewe kama walivyotumwa na ubinadamu hupitapita hümo! Na wakati mwingine vitamaa tamaa vya kibinadamu hupita pita humo vikawapata watu. Wakati mwingine dini, Uislamu na Ukristo, hupakwa matope na ubinadamu — ubinadamu! Dini zilizotazamiwa zisimamie haki tu hujikuta zimeambatana kidogo — kidogo, kidogo ----- kidogo, kidogo — kidogo; Zimepakwa pakwa matope; na matope yale yanafifisha sauti yake!
Katika hili: Ardhi ni ya Mungu. Ardhi anatoa Mungu anawapa binadamu wote— Sisi wapangaji tu. Tunakuja tunapanga tunakwenda; tunakwenda; hakuna mtu aliyetengeneza ardhi. Tunapanga tunakwenda. Tunakuja hivi hivi — tunakuja hivi hivi. Ardhi ipo kwa binadamu wote; Sio kwa baadhi ya binadamu; kwa binadamu wote. Leo Julius na Mheshimiwa hapa wanasema, "Hii yetu", yaani tunachukua haki katika ardhi ya kumnyima huyu, kumnyima huyu, kumnyima huyu! haki hii tunaipata wapi? Wanyamwezi — tuseme — sasa Wanyamwezi mkitaka ardhi niombeni mimi na "Area Commissioner", ni mali yetu; na "Regional Commissioner" ni mali yetu. Maana yake ninil Hii haki tuliipata wapi? Kwa sababu ardhi anatoa Mungu; kulima nalima mimi; kufyeka nafyeka mimi. Naweza kusema, "Hapa nimefyeka jama, nimefyeka mimi; usiniingilie nimefyeka mwenyewe hapa; Aa Aa". Lakini ardhi yenyewe ni ya Mungu.
Sasa tunaanza kugawana; mimi nachukua. huyu anachukua, na Kanisa nalo linachukua! Mimi nimepata pande langu, Mheshimiwa amepata pande lake, Kanisa nalo limepata pande lake, na Maimamu nao wamechukua mapande yao ya ardhi; wanasema wakfu! Vema. Watu wanaanza kunung'unika sasa: ''Jamani hatuna pa kulima!" Tunawatoza. Mimi nawatoza; bwana anawatoza; na Mheshimiwa wa Wakfu na wewe unawatoza. Wote tunawatoza. Wanapiga kelele: "Jamani ardhi ni ya wote imekwenda kwendaje ardhi imekuwa ya mtu" Mimi nasema: ''Nani anasema watu wote sawa'?" Mimi nasema, "Nani kasema watu wote sawa. Watu wanaweza kuwa sawa bwana. Watu tuko tofauti; wengine wanawatumikia wengine. Wote mnawezaje kuwa sawa; mbona hata vidole haviwi sawa?" Mimi nasema hivyo. Na Imamu naye anaanza kusema hivyo hivyo; anachukua na Msahafu. Anapata aya fulani inayosema hayo anayoyataka yeye anakwenda Msikitini anasema:" Nani anasema watu wote ni sawa?" Na Padri anaanza kutetea jambo la kumiliki ardhi binafsi!
Tuonyeshe katika Msahafu: Ardhi tunavyojua. Mungu kawaumbia wote hakuigawanya. Wewe Padri. binadamu wamegawana-gawana na wewe umetumbukia ndani!? Sasa Padri akishatumbukia ndani akagawana, na yeye ana-pande Iake Ia ardhi, hawezi kuwatetea maskini.; Hawezi kuwatetea maskini. Anatetea wenzake wenye ardhi. Kadhalika Misikiti na Makanisa mkianza kuwa na nyinyi mña viwanda.-
Badala ya kuhubiri Neno Ia Mungu, mnahubiri viwanda vycnu. Mnategemea mali ya kutokana na viwanda. Sasa nyinyi. wafanyakazi na matajiri wanapozungumza juu ya dhuluma, nyinyi lazima mtakuwa huku pamoja na matajiri. Na wafanyakazi wako upande mwingine — wanawanung'unikia matajiri wao pamoja na nyinyi vile Vile.
Kwa hiyo kelele ya dhuluma itakapoanza: "Jama tunadhulumiwa na Matajiri Misikiti kimya; haisemi kitu; Makanisa kimya; hayasemi kitu. Yanasema: "Wana fujo hao". Na hasa- kama wanaodhulumu ni Serikali: haya makubwa, haya yenye mali ndiyo vile vile huwa matawala ya Serikali vile Vile. Basi Mapadri mara wanasimama katika Makanisa wanasema: "Mpeni Kaisari kilicho chake!" "Chake! hata ardhi ya Mungu vile vile yake! Hata ardhi ya Mungu nimpe Kaisari, mali yake ile? Ardhi — Kaisari na mimi kwa Ardhi wote sisi ni sawasawa. Kaisari anakula na mimi nakula. Kwa nini Kaisari yeye awe na ardhi mimi sina Ardhi' Padri kusema: Mpeni Kaisari chake"; ”Chake nini "Chake, Ardhi?" ”Chake, Ardhi? Kaisari ana matumbo mangapi. huyu mnamtetea yeye awe na ardhi? Na sisi wote sawa ! Kaisari anânionea mimi nyinyi mnasema Mpe Kaisari chake ” ' 'Chake", ni kipi cha Kaisari hasa?”
Kaisari kwamba awe na viwanda. Anasema: Hawa wafanyakazi wangu! Kaisari amepata — ana viwanda chungu mzima amevipata wapi viwanda hivyo Kaisari? Kaisari naye si alikuja duniani hivi hivi, naye mtupu hivi kama Sisi? Leo ana viwanda, ana watu wake wanamfanyia kazi, ana mamali ya ajabu!”' Mashekhe tunapiga kelele Sisi: ”Huyu Kaisari anatuumiza jamani tazameni ana mali huyu; kaambatana na matajiri venzake, tunabanwa- tu; sasa Polisi na majeshi ya kutuonea Sisi?' ' Badala ya kuja na kututetea Sisi, Mapadri na Mashekhe mnatwambia: 'Lazima mtii wakubwa”. ''Tuwatii wakubwa, hawa wanyonyaji!” Mnatujibu "Unyonyaji si kitu”.
Mahubiri mengine kwa sababu Sheikh, na lmamu, na Padri na Askofu mmekwisha ambatana mna ma Ardhi, mna viwanda, mna ma mali', kwa sabâbu mmekwisha fitia huku azima mtumie Kuruani na Injili kutetea mali yenu. Hamwezi kuitumia Kuruani na Injili kutetea maskini, hata! Na, inadhaniwa, Ulaya ilifika kiasi hicho. Wanadhani watu Ulaya ilifika kiasi hiëho. Ilifika kiasi hicho! Dhuluma ni ya dhahiri kabisa kabisa, lakini Makanisa kimya! Wanababaika katika jambo la haki kana kwamba Kanisa nalo linababaikal Kanisa kama halijui kama hii ni dhuluma au si dhuluma! Kanisa haliwezi kuwa na mashaka juu ya dhuluma! Kanisa haliwezi kuwa na mashaka liseme: "Hatujui kama hii ni dhuluma au si dhuluma!"
Kanisa wakati wote linajua: Hii ni dhuluma na hii ni haki. Haliwezi kuwa na mashaka mashaka. Haiwezi kuwa imegawanyika kabisa kabisa, kundi kubwa linasema. "Hii dhuluma", halafu Kanisa lasema "Sisi hatujui". Kanisa hamjui! kwamba hii ni dhuluma au si dhuluma?•
Sasa likinyamaza Kanisa, sio kwamba mambo yenyewe basi watu wanyamaze. Kanisa laweza likababaika: inaweza ikababaika; lakini Watu hawawezi kunyamaza Wataendelea. Wataendelea kupigania haki yao. Na Ulaya ilifika kiasi hicho. Ulaya ilifika kiasi hicho; jamaa wakaendelea, Nadhani walifika wakati 'wakasema Ala, kumbe Makanisa yenyewe ndiyo hivyo — lo! potelea mbali"! Wakajikatalia. Wakajikatalia wengine wakakataa dini. "Kumbe dini- zenyewe ndiyo hivyo bwana: dini inaona watu wanaonewa wengine hivi hivi dini haisemi....