Unajua ingawa naweza ku-sound kama an idealist am a pragmatist..., Hizi theory / idelogies ni kama guidelines wala sio Msahafu tukichukulia Socialism na Capitalism (na hapa sitaki kusema Ujamaa) theory inaweza ikakwambia kwamba moja ni opposite ya nyingine lakini realistically hakuna nchi ambayo ni 100 sociliast wala 100 percent capitalist..., Nchi kama USA pomoja na kujinasibu kama ya Kibepari lakini kuna Social welfare ya kufa mtu..... Now Je Ujamaa tunaongelea nini kama ni Commanding Heights za Economy kuwa kwenye State Ownership that is good, kama ni planned economy ya kupangiana Bei (kama sasa hivi sukari n.k. sijui bei elekezi n.k.) hio will never work and meddling will make it worse....
Tukija kwenye vijiji vya Ujamaa it was badly planned and could never work, huwezi kuwa-force watu waache mali zao na kuwapeleka kama mifugo (people have free will) LAKINI naweza kukwambia modern cities of today they are nothing more than vijiji (watu wakiwepo karibu ni rahisi kuwapelekea huduma)..., Lakini kumbuka Israel na kibbutz walifanya hili jambo na kwenda to such an extreme hadi kuingilia haki za individual to me that was an utopian idea... Kwa ufupi ndio maana sitaki sana kujikita kwenye hizi theories sababu kama nilivyosema haya mambo sio msahafu ni mixture ya hapa na pale na kinachoweza kufanya kazi hapa huenda kwenye jumuia nyingine kisifanye
Unajua kwanini tuongelee kuwalinda hawa au kuwaonea hawa ? Kwanini wote wasiishi no matter wingi wao au uchache wao ? Point unayotaka kusema kwamba Ujamaa ni kulinda baadhi ya watu sikubaliani nayo unless hao watu ni so called wanaonyonywa (sikatai kwamba practically Ujamaa mwingi ulikuwa ni Ubepari kwenye ngozi za Kijamaa ambapo wachache waligeuza kula Keki wakati wengine wanashangaa) ila hio sio Misingi.... Na tatizo la kuangalia hizi theory ni kuchanganyana.... Mfano niki-qoute Hotuba....
Karne ya kumi na tisa. Wakati ambapo Ubepari Ulaya. Ubepari Ulaya, umekomaa sana. Ubepari: hapa wakati mwingine lazima ueleze maana ya Ubepari maneno haya maneno mapya yote haya: maana ya Ukabaila ni nini? Maana ya Ubepari nini. Ulaya si lazima kueleza hii. Wanajua kabisa Ukitamka tu wanajua maana yake. Ukisema Feudalism, Ulaya wanajua kabisa unasema nini. Huna haja ueleze-eleze. Mnyamwezi ukisema Ukabaila, anakuuliza: "Ukabaila ndio nini?” Ueleze taratibu, anauliza tena: 'Makabaila hao wako wapi?” Maana Unyamwezini hawapo. Hawapo 'hao wamiliki wa ardhi. Hao wanaomiliki ardhi, na nyinyi wengine mnakaa katika ardhi ya watu mnawatumikia tu; hawapo hao. Mnyamwezi hajui habari hiyo. Ulaya wanajua sana habari hiyo ya kwamba ardhi kama hii ya Tabora yote inaweza ikawa ni ya miamba miwili tu na wengine wote mnakaa katika ardhi ambayo ni yao hao miamba mkabaila wakubwa hao. Na mnakaa kwa ruhsa yao. Wanaweza kusema: "Toka katika arthi yangu; nenda zako”
Mnyamwezi hajui habari hiyo; hajui habari hiyo. Ulaya wanajua habari hiyo. Wanajua taabu ya kuwa huna ardhi. Ardhi ukitaka unamwomba mtu. Hakuna ardhi ya Ummal Unamwomba mtu,.binadamu, akupe ardhi.” Akupe kwa ruhusa yake; na akupe masharti yake. Waswahili Tanzania hamjui habari hii hata kidogo. Na uchungu wake hamuujui. Kwani tunapolieleza hili, wakati mwingine tunakinga hatari iko mbali. Waswahili hawana habari na hatari hiyo.
Hio ni sababu ya Kijamaa ? (kwamba tunachagua rangi) au ilikuwa sababu ya kijamaa kwamba most companies ni state owned hivyo automatically hawa sio kwamba walitengwa bali walijitenga; Vilevile sitaki kujikita kwenye theory sababu practically kilichotokea na utendaji mbovu sio necessarily what the theory / ideology says na hapa unaongelea Ujamaa versus Liberalism na Sio Ujamaa vs Capitalism of the time Kitu ambacho the Socialist at the time were fighting against....
Kwamba uwepo wa Sheria mbovu au uonevu wa baadhi ya watu ni sababu ya watu kufuata Ujamaa, Ubepari au hata Imani fulani ? Hivi unajua hadi watu kuamua Separation of Church and State ilikuwa kuondoa Uonevu kwa watu ambao sio wa Imani hio ? Na unaweza vipi kuepusha Imani moja au kutokuwa na Imani moja kuonea wengine zaidi ya kusema kwamba wewe kama nchi / serikali huwapangii watu cha kuamini wala huwatungii sheria ya Kuamini au kutokuamini bali wajipangie wenyewe ?
Mkuu hapa tu JF watu kumi tunashindwa kuelewana mambo ya Imani sasa hapo unataka iundwe Serikali ambayo inajumuisha watu accoarding to Imani zao, sasa Imani ipi itashika hatamu na kama zikikinzana what then ? Unaona kweli muda wa kuulizana kuhusu ugawanaji wa keki ya taifa (elimu, chakula, barabara, matibabu) hautoshi sasa tuongezeane muda wa kujadili Imani kitaifa ?
Na wakishinda watu ambao Imani yao inasema labda hata Huduma za Ki-afya maybe blood transfusion inakwenda against Mungu na kuacha kuwekeza kwenye Mahospitali what then... Kikishinda Chama cha
Serikali inakusanya Kodi kwa watu wote no matter Imani zao tukianza kupangia Kodi yangu ifanye nini kulingana na Imani ya fulani hatutafika hakuna mtu atatoa Kodi...., Na hata leo unaweza ukalaumu kwanini Kodi yangu inatumika kuwekeza kwenye vilezi unless Kiwanda cha kilevi kinazalisha zaidi na kuleta faida hata ya kumletea maji huyo Mpemba....
Unapoongelea majimbo kwa muktadha huu ni kama kuongelea jambo lile lile microscopically..., kama jimbo langu mimi mkristo wengi ni waislamu what then ? Kwamba serikali na Sheria zinihukumu mimi kama Muislamu sababu ni minority ? Which is better kufanya hivyo au kuachana kabisa na mambo kuunganisha Imani na Serikali ?
Ni kama vile hatuelewani.
Nadhani ni kwasababu si mwathirika wa itikadi hii.
Lakini msingi wa hoja zangu inakubalika na tafiti zinazoheshimika.
Kwa mfano upo utafiti kutoka taasisi yenye kuheshimika ukithibitisha kuwa nchi nyingi zinazojipambanua hazina dini hupendelea (hulinda) dini moja na kudhibiti (kubagua ) nyingine.
Many Countries Favor Specific Religions, Officially or Unofficially
Pili nadhani pia hatutoelewana kwa kuwa tuna baadhi ya maneno tunatumia kila mmoja ana maana tofauti na mwengine
Mfano neno
1. SERIKALI – Ni wananchi walio na mamlaka kupitia
uchaguzi/kura. Na mamlaka hayo kuyakasimu
kwa Watendaji wa Serikali ili wasimamie
maamuzi, mahitaji na matakwa yao.
2. Dini.
Neno dini kina maana mbili hadi tatu ambazo zote zinakubalika.
Dini yako ni utamaduni wako.
Dini ni mahusiano kati ya muumba na waumbwa
Dini ni imani
Dini ni mfumo wa maisha.
Mara zote napotaja neno dini lkn kwa upande wangu mi nanamaanisha tafsiri yenye nguvu ni hii ya tatu.
Na kwamba Ujamaa ni imani hivyo Ujamaa ni dini. Na kwamba hata upagani nayo ni dini. Kwa kuwa dini ni mfumo wa maisha, hivyo hakuna mtu anaweza kuishi bila ya mfumo wa maisha.
Kama tunakubaliana nani basi weka tafsiri moja wapo kila ulipoandika neno dini.
Uislam kwa mfano nao ni mfumo wa maisha. Kwa kwamujibu wa reference zilizopo ndani ya mwongozo wao, uislam haujaa haujaacha kipengele chchte cha maisha.
Bali ktk mfumo wa utawala hasa utawala wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamuliaambo yao wenyewe, ni kura ya maoni ndio itakayoamua iwapo kundi hili kinataka kujiongozwa kwa kumtanguliza Mungu basi ajiongoze bila kumlazimisha asiyeamini hilo.
Kwa mfano kama hijab imeruhusiwa kwa binti wa kiislam wa kike mwanafunzi, sheria hiyo hiyo inawaruhusu wa kada nyengine. Yakiwemo majeshi.
Kwa nchi kama SA, UK zinawapa ruhusa hiyo masingasinga, wayahudi na waislam. Pamoja wote wanaamini ktk Usekyula lkn UK na SA hulinda makundi yote kwa kuwa wao ni waliberali.
Lkn Usekyula wa wajamaa unadhani ndio maana utaona pamoja na uwingi wa waislam tz lkn wajeshi wa kike ambao mavazi ya stara ni ibada kwao lkn hunyimwa uhuru huo wa kuabudu kwa kuwa kazi ya itikadi ya Usekyula ktk nchi hizi ni kudhibiti baadhi ya makundi ingawa hawaleti madhara yyt ktk umoja wa kitaifa. Na wala hawalazimshi watz wote.
Kwa tz tunapaswa kuwapatia uhuru huo wamasai pia.
3. Unapouzungumzia ujamaa unajielekeza kwa kanuni za kiuchumi pekee. Wakati kama Ujamaa ni kanuni za uchumi hata uislam una kanuni zake za uchumi. In fact uchumi wa kijamaa na wa uislam tunatumia kanuni moja. Uchumi utamilikiwa na umma.
Lkn huraki kuizungumzia theology ya Ujamaa au usekyula. Jambo ambalo ndio moja ya msingi wa kujua iwapo Ujamaa ni dini au laa.
Wakati theology ya uislam ni kuamini uwepo wa Mungu na kuogopa kufanya ufisadi, uhuni na kuingizwa na uadilifu na wema.
Ukomonist/ujamaa uliongozwa na theologian ya kukana uwepo wa Mungu. Hivyo kuondoa hofu ya kushutumu, ufisadi nk. Muhimu kwao ni kuabudu viongozi wakuu tu yatosha.
Hivyo ni vizuri uelewe kuwa uislam si dini kwa maana ya kurukaruka barabani na kufanya miujiza.
Bali uislam ni mfumo wa maisha kama ilivyo ubepari, ujamaa nk.
But princial za uislam zinaongozwa na kumtanguliza mungu.
Na tunaposema tunataka Utawala wa dini zote inamaana kuwepo na utawala utakaolinda wenye dini na kudhibiti wasio na dini (waasherati) kama ambavyo serikali usio na dini unavyodhibiti baadhi ya dini na kulinda matendo ya kiesherati. Waathirika wanatambua hili.
Na kwamba Itikadi hizi mbili zishindanishwe, na ni wajibu wa wananchi kuamua itikadi gani wanayoitaka.
Lkn mfumo wa serikali za majimbo yenye nguvu zaidi za kujiamulia mambo yake wenyewe ni suluhisho la pili kuondokana na mfumo wa sasa wa dini moja kuhodhi madaraka na kuwa maamuzi mipango ya nchi.
Niishie hapa na shukran kwa wasaa wako