Ujambazi wa polisi liwe fundisho kwa Serikali ya Rais Samia

Ujambazi wa polisi liwe fundisho kwa Serikali ya Rais Samia

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Baada ya vitendo vya kijambazi vinavyofanywa na polisi kushamiri katika siku za karibuni, sasa imefika wakati serikali ijithathmini namna ya kuwachuja polisi wanaofaa kuajiriwa. Madhara ya kung’ang’ania form four failures (Divison 4 & 0) ndiyo yametufikisha hapa tulipo. Sasa serikali ianze mara moja kuajiri wahitimu waliofaulu vizuri (Divisheni 1 & 2) ili kulinda heshima ya jeshi la polisi. Polisi wenye ufaulu mdogo wana kiwango kidogo cha kufikiri na pia wana upeo mdogo wa kudadavua mambo.

Na pia imeonyesha hawa polisi ambao ni form four failures, wana tamaa ya pesa na inawezekana wanatokea familia masikini jambo linalopelekea kuwa na mitindio ya ubongo ama kwa kukosa lishe nzuri au kulelewa malezi ya ajabuajabu. Mtu aliyelelewa vema akili zake hukuwa vema na huwaza vema. Polisi wa sasa hivi ni zaidi ya vichaa. Ukitazma matukio wanayofanya na sababu wanazotoa unaona kabisa kwamba wana hililafu fulani vichwani mwao. Polisi mwenye akili zilizotimia hawezi kuondoa uhai wa raia kwa sababu tu ya fedha.

Michezo hii ya polisi ilianza wakati ule wa akina Zombe walipompora mamilioni ya fedha mfanyabishara wa madini kutoka Morogoro na kisha kumuua. Laana ilianzia hapa. Kabla machozi hayajakauka, wamekuja tena kumuua mfanyabishara mwingine wa madini kutoka Mtwara. Inauma sana. Ina maana polisi hawataki watu wachimbe au wajihusishe na biashara ya madini katika nchi hii? Polisi wamekuwa kama fisi wenye njaa wanaomfuata mtu nyuma wakitamani mkono mmoja udondoke wafanye kitoweo. Lakini polisi wetu hawa wameenda mbali zaidi. Wanalazimisha kumuua mtu ili wachukue mikono wale kisha kukimbilia vichakani kujificha.

Pamoja na ujambazi wote huu unaofanywa na polisi, tangu kuuliwa kwa Daudi Mwasngosi hadi mfanyabishara wa madini wa Mtwara, siajwahi kusikia Waziri au kiongozi yeyote wa polisi au serikali akiwajibika kwa kujizuru. Tukumbuke miaka ya nyuma Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzuru uwaziri baada ya polisi kuhusika kwenye uhalifu kama huu unaofanyika siku hizi. Natoa wito kwa Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Sirro kujiuzuru nyadhifa zao mara moja ili kuonyesha uwajibikaji wao kwa haya matukio ya kijambazi yanayofaywa na polisi mchana kweupe.​
 
Shida sio wasomi tena hao wasomi wenyewe ndio wanaoisumbua serikali maana kwa elimu zao anaona anachelewa kupata maendeleo akifikiria elimu yake.

Mbona zamani kulikuwa na wa elimu ndogo hadi la saba b lakini weledi ulikuwepo? Tatizo hapo ni tamaa ya mali haraka haraka ebu wapewe mshahara wa kutosha uone kama kazi haijafanywa vizuri hata na rushwa yaweza pungua.

Ni bora wawe polisi wachache posho kubwa
 
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata sababu wanazotoa baada ya kumuua polisi mwenzao ni za kitoto sana. Polisi mwelewa mwenye divisheni wani au twu hawezi kutoa sababu ya kiqumer kama hii waliyotoa hawa failures 😳 😳 😳
 
1643556199102.png
 
Mkuu pamoja na Mama Rais wetu kuyasema haya Ila tatizo naliona katika kuchagua viongozi wa kuwasimia hao wa chini, naona Kuna chain of command ambayo sio nzuri na ndiyo inayowachafua
 
Mkuu pamoja na Mama Rais wetu kuyasema haya Ila tatizo nakuona katika kuchagua viongozi wa kuwasimia hao wa chini, naona Kuna chain of command ambayo sio nzuri na ndiyo inayoeachafua
Ndio maana nimeagiza Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Ziro wajiudhuru nyadhifa zao ili kuonyesha uwajibikaji binafsi. Wasimtwishe Rais Samia lawama zote hizi na kupelekea chuki dhidi ya serikali kutoka kwa wananchi wanyonge wanauliwa na polisi kama kuku kila kukicha.
 
Maadamu mshahara hautoshi hata Wiki mbili hakuna kitu kitafanyika kubadilisha chochote I mean, mtu analipwa laki 3 kwa mwezi unategemea aishi vipi ? Hapo sijaongelea vitendea kazi kama uniform, viatu, gloves na vinginevyo, Polisi pia kama walivyo Watanzania wa profession nyingine wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana hapo hapo wanasikia Raisi wa nchi akiwaruhusu Mawaziri ambao tayari wanalipwa vizuri kuiba mali ya umma halafu unategemea Polisi awe Malaika ?

Shida ya kubwa Tanzania ni INJUSTICE, maadamu hakuna haki wala usawa Polisi mnawaonea tu, kwani Walimu wana shida, Madaktari wana shida, Manesi wana vilio wote hao wanatakiwa wawe waaminifu lakini Waziri kuiba ruksa, huwezi kujenga jamii yenye heshima na hofu ya Mungu kama kuna injustice kuanzia kwa Raisi mwenyewe .
 
Maadamu mshahara hautoshi hata Wiki mbili hakuna kitu kitafanyika kubadilisha chochote, I mean mtu analipwa laki 3 kwa mwezi unategemea aishi vipi ? Hapo sijaongelea vitendea kazi kama uniform, viatu, gloves na vinginevyo, Polisi pia kama walivyo Watanzania wa kada nyingine wanafanya mazingira magumu sana hapo hapo wanasikia Raisi w nchi akiwaruhusu Mawaziri ambao tayari wanalipwa vizuri kuiba mali ya umma halafu unategemea Polisi awe Malaika ?
Sasa walipoambiwa wale kulingana na urefu wa KAMBA yao maana yake waue raia na kupora mali zao? Kama wanaona mshahara ni mdogo si waache kazi, kwani kuna mtu kawalazimisha kubaki kazini? Mkuu usiseme hivyo kuna watu wamepoteza wapendwa wao kwa sababu ya ujambazi wa polisi. Usiwatoneshe vidonda.
 
Hata sababu wanazotoa baada ya kumuua polisi mwenzao ni za kitoto sana. Polisi mwelewa mwenye divisheni wani au twu hawezi kutoa sababu ya kiqumer kama hii waliyotoa hawa failures 😳 😳 😳
Ndugu Walio faulu vyema hawataweza kuuza roho zao kirahisi... Kazi ya Police ngumu broo... Kule shule ndogo moyo mgumu ndo unahitajika.
Kazi ile sio ya kushika karatasi na kalam nakuanza kuandika essay ya Literature.
Au kuchambua vitabu vya Ngoswe.
Ama kuchora mchoro wa battery yenye posv na Negv.

Elimu yako inabaki kabatini kule nikushika mtutu kujilinda na kulinda mali za raia.
Sasa kama ukiamini dvn 1 itakaa na mtutu na kulinda usiku kucha basi sawaaa.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana nimeagiza Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Ziro wajiudhuru nyadhifa zao ili kuonyesha uwajibikaji binafsi. Wasimtwishe Rais Samia lawama zote hizi na kupelekea chuki dhidi ya serikali kutoka kwa wananchi wanyonge wanauliwa na polisi kama kuku kila kukicha.
Ni matumaini yangu kwa mawazo ya wananchi watafanya tathimini ya kujiboresha zaidi
 
Elimu yako inabaki kabatini kule nikushika mtutu kujilinda na kulinda mali za raia.
Sasa wanapowaua raia na kuchukua mali zao ndizo kazi walizotumwa kufanya mkuu? Hawa polisi wetu ni wa ovyo sana. Mbona huko Ulaya na Marekani wanachukua divisheni wani na twu lakini wanapiga kazi kama kawaida? Hawa polisi wetu bange wanazovuta zinawaharibu vichwa.
 
Sasa walipoambiwa wale kulingana na urefu wa KAMBA yao maana yake waue raia na kupora mali zao? Kama wanaona mshahara ni mdogo si waache kazi, kwani kuna mtu kawalazimisha kubaki kazini? Mkuu usiseme hivyo kuna watu wamepoteza wapendwa wao kwa sababu ya ujambazi wa polisi. Usiwatoneshe vidonda.

Ukisharuhusu injustice huwezi kukontrol how far injustice can go, ni ukweli wa maisha huo, ndiyo maana nchi za Kidini zilizostaarbika zote za Kikristu na Kiislamu Viongozi wanahakikisha kila raia anapata stahiki yake kwa wakati na inayomtosheleza kuishi maisha ya heshima.

Wakati mwingine ni stress tu zinafanya Binadamu awe mnyama, wewe unamwambia Polisi akalinde amani akapambane na Majambazi ambapo uwezekano wa kufa wa kulemaa upo wakati huo huo ana njaa tumboni au mtoto hana karo ya Shule, uniform imetoboka, viatu vimechanika na kavaa smg unategemea nini ?
 
Kwani hawo polisi wamelazimishwa kufanya kazi wakiwa na njaa na mzongo wa mawazo? Kama wanaona kazi ya upolisi hailipi si waachane nayo wakafanye kitu kingine? Udogo wa mishahara ya polisi na mazingira magumu hayawezi kujustify ujambazi wanaofanya bila soni kwa kupora mali na kuua raia hadharani. Sidhani kama unanielewa.
 
Mtafukuza wote na kuajiri upya lkn maadamu kila kitu kinabakia kama kilivyo hakuna kitakachobadilila, kufanya kazi katika mazingira magumu kiasi hicho halafu hapo hapo utake awe muaminifu wakati wewe mwenyewe siyo mwaminifu, hilo haliwezekani.

Hii ni man eat man society, na kila mahali ni hivyo!
 
Shida sio wasomi tena hao wasomi wenyewe ndio wanaoisumbua serikali maana kwa elimu zao anaona anachelewa kupata maendeleo akifikiria elimu yake.
Mbona zamani kulikuwa na wa elimu ndogo hadi la saba b lakini weledi ulikuwepo? Tatizo hapo ni tamaa ya mali haraka haraka ebu wapewe mshahara wa kutosha uone kama kazi haijafanywa vizuri hata na rushwa yaweza pungua.
Ni bora wawe polisi wachache posho kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemaliza mkuu.
 
Mtafukuza wote na kuajiri upya lkn maadamu kila kitu kinabakia kama kilivyo hakuna kitakachobadilila, kufanya kazi katika mazingira magumu kiasi hicho halafu hapo hapo utake awe muaminifu wakati wewe mwenyewe siyo mwaminifu, hilo haliwezekani.

Hii ni man eat man society, na kila mahali ni hivyo!
Kwa hiyo wewe unakubaliana na UJAMBAZI huu wa polisi au msimamo wako ni upi? Nini kifanyike?
 
Back
Top Bottom