sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Huwa nawaonea huruma sana vijana wadogo wanaochora tattoo kuona ni ujanja ama kufuata mkumbo... kwa nchi kama ulaya na marekani tattoo sio shida hata kidogo, ila kwa hapa bongo hali ni tofauti kabisa.
kwa mitazamo ya jamii zetu, mtu akisha chora tatoo basi heshima yake inapungua pakubwa mno kwenye jamii zetu, jamii itamuweka kundi moja na wavuta bangi ambao huonekana ni wahuni, yes! ndivyo jamii zetu zilivyo, kuna vitu ukivifanya hata kama havina madhara utaonekana ni muhuni tu.
itakufanya uonekane ni mhalifu mbele ya vyombo vya usalama, upo hatarini kuwa mtuhumiwa namba moja endapo kuna uhalifu umetokea kwa sababu tu jamii imejenga dhana kwamba mtu mwente tatoo ni muhalifu. ni rahisi sana hata kusingiziwa wewe ni jambazi, muuza madawa, n.k.
inakuwa shida zaidi ukiwa ni binti, itakuharibia sana kwenye swala la kupata mume, wanaume wengi tuna dhana ya kwamba mwanamke aliechora tattoo ni malaya aliekubuhu. hata utapoenda kutambulishwa kwa familia ya mwanaume basi tegemea wakuone huna maadili na humfai mtoto wao.
kwa ulaya na marekani kuna wanajeshi, mahakimu, madaktari wana tattoo na maisha yana kwenda ila kwa hapa bongo ukiwa na tattoo hupati kazi serikalini hata kama una connection ama una vyeti vizuri. ponea yako labda utafte kazi makampuni binafsi au N.G.O za wazungu hapa bongo.
kadiri miaka inavyoenda mambo hubadilika, umechora tattoo ya mpenzi wako mkaja kuachana inakuwa vp ? umechora tattoo ya msanii flani havumi tena huko mbele itakuwaje ? ulichora tatoo ya nyota shingoni kuendana na fasheni za miaka ya 2010, leo hii unajisikiaje hii fashen imeshachuja ?
Pia jua ya kwamba kwa hapa bongo ukichora tattoo hurusiwi kuchangia damu kwasababu tattoo huwa inachorwa na sindano inayoingiza wino kwenye ngozi ila huwa inafika kwenye damu, huu wino ukishaingia kwenye damu ni hatari kiafya kuchangia damu.