View attachment 2243436
View attachment 2243438
Huwa nawaonea huruma sana vijana wadogo wanaochora tattoo kuona ni ujanja ama kufuata mkumbo... kwa nchi kama ulaya na marekani tattoo sio shida hata kidogo, ila kwa hapa bongo hali tofauti sana
wanajeshi,mahakimu,wacheza mpira,wasanii,madaktari wanatattoo na maisha yana kwenda
Mosi, kwa mitazamo ya jamii zetu, mtu akisha chora tatoo basi kwa kaisi fulani heshima yake inapungua pakubwa mno kwenye jamii zetu, jamii itamuweka kundi moja na wavuta bangi amba huonekana ni wahuni, yes! ndivyo jamii zetu zilivyo, kuna vitu ukivianya utaonekana ni muhuni tu.
itakufanya uonekane ni mhalifu mbele ya vyombo vya usalama, upo hatarini kuwa mtuhumiwa namba moja endapo kuna uhalifu umetokea kwa sababu tu jamii imejenga dhana kwamba mtu mwente tatoo ni muhalifu.
inakuwa shida zaidi ukiwa ni binti, itakuharibia sana kwenye swala la kupata mume, wanaume wengi tuna dhana ya kwamba mwanamke aliechora tattoo ni malaya. hata utapoenda kutambulishwa kwa familia ya mwanaume basi tegemea wakuone huna maadili na humfai mtoto wao.
kwa ulaya na marekani kuna wanajeshi,mahakimu,madaktari wana tattoo na maisha yana kwenda ila kwa hapa bongo ukiwa na tattoo hupati kazi serikalini hata kama una connection ama una vyeti vizuri. ponea yako labda utafte kazi makampuni binafsi au ngo za wazungu hapa bongo.
kadiri miaka inavyoenda mambo hubadilika, umechora tattoo ya mpenzi wako mkaja kuachana inakuwa vp ? umechora tattoo ya msanii flani havumi tena huko mbele itakuwaje ? umechora tatoo ya nyota shingoni kuendana na fasheni, ghafla imeshachuja, inakuwaje ?
Pia jua ya kwamba kwa hapa bongo ukichora tattoo hurusiwi kuchangia damu kwasababu tattoo huwa inachorwa na sindano, vitu kama hivi yenye ncha kali endapo havibadilishwi husambaza magonjwa kama ukimwi , Home ya Ini B, n.k. ila pia hata ule wino unaweza ukawa umechafua damu yako.