Ujana haudumu, kuchora tattoo kunaweza kukugharimu sana maisha yako ukubwani

Namfahamu kijana, babu na babake wote walikuwa jeda waheshima!
Yeye bright akapelekwa China kusoma, karudi na degree Kali!
Finance & Chinese. Anajua lugha 4, Kiswahili, English, French na Chinese.

Kumuingiza jeshi CV ikagoma, kisa tattoo!
Wakajaribu aende sijui wanyama Pori, nako kukabuma! Kisa tattoo!
Sikuwahi kuwaza kibongobongo, mtu aweza kosa kazi!

He is frustrated, anakunywa mipombe na mabangi, anashinda na bodaboda Tu vijiweni!
Wamemfanyia counseling, haamini hawezi kuitwa GENERAL!

He is lost, kwa sababu aliamini yeye kazi ni moja tu, jeshi!
Kazi za ukalimani wapo masela wengi mitaani wanajua lugha.
 
labda kwa tanzania na africa.ila kwa wenzetu hakuna hayo kuna wanajeshi,mahakimu,wacheza mpira,wasanii,madaktari wanatattoo na maisha yana kwenda
 
Usipangiane maisha watu..hivyo vizazi vya kuona tatoo uhuni vimeanza kutoweka..soon wazazi nao watakua na tatoo.

Halafu mbona wamakonde, wanyaturu n.k walikua wanajichora zamani..hao mbona huwaongelei.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bado ni changamoto sana hakika, kama mtu hakuna ulazima sana achana na tatoo ni mbaya sana haswa baadaye kama alivyo eleza mtoa mada
 
Ebu toa madhara ya Tatoo na usitageti katika .... Kuajiriwa tu.
Achana na kuajiriwa athari kubwa ni mitazamo ya jamii zetu....mtu akisha chora tatoo basi kwa kaisi fulani heshima yake inapungua pakubwa mno kwenye jamii zetu, hata kuaminika hawezi kuaminika sana
 
Miaka ijayo itakuwa kitu cha kawaida na hii Taboo itaondoka tu.
Itachukua muda mrefu sana labda huko mijini lakini huku kwetu vijijini itachukua muda mrefu sana, pia unapaswa ukumbuke uwepo wa tatoo umeanza miaka mingi sana imepita lakini hadi sasa bado ni changamoto
 
Muwe mnaweka na picha mazejooo hili kuchangamsha uzi
 

Attachments

  • FB_IMG_1650807588706.jpg
    43.4 KB · Views: 28
Usipangiane maisha watu..hivyo vizazi vya kuona tatoo uhuni vimeanza kutoweka..soon wazazi nao watakua na tatoo.

Halafu mbona wamakonde, wanyaturu n.k walikua wanajichora zamani..hao mbona huwaongelei.

#MaendeleoHayanaChama
Ndonya za wamakonde ndiyo kwa upande mwingine ni kweli ndizo tatoo zenyewe lakini hiki ni kitu tofauti sana na hizi za kisasa haswa katika mitazamo na fikra za watu...hebu jaribu kufikiria wanaume wa Kimasai wanasuka nywele na jamii haina shida na hilo...lakini hebu niambie mwanaume wa Kichaga/Kihaya akisuka jamii itamtazamaje?
 
Sawa mkuu
 
Acha kutisha watu..kwa illusion zako.

#MaendeleoHayanaChama
Haman mtu anamtiaha mtu mzima. Tunaandika kutokana na uhalisia kama unadhan natisha na iwe hivyo. Binadamu tunapenda kusikia tunachokiamini
 
Familia lazima ilie na kujua kijana wao tayarii kashaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…