Ujana haudumu, kuchora tattoo kunaweza kukugharimu sana maisha yako ukubwani

Mzee baba.....hivi Kuna uhusiano gani Kati ya kuchangia damu vs mtu aliechora tatoo........coz hili Jambo nalisikia sana
Wana-assume vitu vyenye ncha kali havikuwa salama na vinaweza kusambaza magonjwa yasababishwayo na virusi kama UKIMWI, Home ya Ini B, n.k.
 
Chora na wewe ukaajiliwe huko ubalozini,unaonywa lakini hutaki kusikia wewe vipi lakini
 
Mimi huwa naona msichana aliyechora tattoo ni kama jini tu
 
Kuna msela nilipiga nae kazi kipind nipo intership na alikuwa afisa mkubwa analipwa vizuri taasisi nyeti kachora tattoos kweny bega havai nguo za mikono mifupi hata t shirt za kiofisi anavaa na t shirt ya mikono mirefu ndani mtu mzima miaka 42 anafika yuko poa ila ukingulia unajua huyu mafia kabisa then alisoma nje unaonyesha

Siku moja natoka sina hela nilikuwa na buku vya hiace akaniambia unaelekea wapi nikamwambia sinza anakaniambia panda mi naenda huko huko ila kwangu kimara .nikapanda Ana vanguard kali mpya safari inaanza tu kweny redio zile za smart kaingia YouTube kaweka ngoma ya kodak sielewi naona bangi tu jamaa mbinafsi akaweka earphone masikioni mpaka tunafika na niliona karatasi za zig pembeni
 
nilipataga bonge la pisi kabla ya kufanya yetu ilichukua miez 2 nkasema mke ndo huyu kila anayetambulishwa napewa sifa kama zote.

siku nakula vyangu chumba namuweka chuma mboga lahaula tatoo hyo ya rose kiunoni dah mzuka ote ulikata,na tulipotakaga pale hatukuonan tena na kila kitu nili cancel
 
Izo sifa zote ni kwa wale wasio na hela,,ukiwa na kibunda hata ukiwa na tatoo usoni utapewa tu heshima
 
Binafsi siwezi kuchafua ngozi yangu kwa maswala ya kipuuzi kama haya
 
Unajua sisi vijana huwa tunafanya mengi sana yanayo haribu uelekeo mzuri wa maisha kwa kuiga, ukimuona Sergio Ramos anacheza mpira kachafuka tattoo unaona ujanja si ndo huu sasa kumbe yule tayari kashatoboa maisha mtu kwa wiki analipwa zaidi ya million 500 za ki Tz alafu unamuiga

kwa life la kibongo tattoo ni sumu hasa kwa sisi wa familia maskin tattoo itakuachia njia nyembamba sana ya kufanikiwa na njia nyingi itakuzibia, ukizingatia unakuta wazee wanalala njaa ili wakusomeshe uajiriwe maana mtaji wa kukupa hawana
 
maamuzi ya udogoni hayaondoagi madhara ykubwani....

ukiona umepita miaka ya 15 hadi 25 salama mshukuru Mungu wako, wengi sana huwa wanavuruga hapa
 
Binafsi siwezi kuchafua ngozi yangu kwa maswala ya kipuuzi kama haya
ukiona umepita miaka ya 15 hadi 25 salama mshukuru Mungu wako, wengi sana huwa wanavuruga hapa
 
Upo sahihi. Hawajui kuhusu hilo, mikumbo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…