Gobole Lenye Risasi
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,519
- 23,693
Hii Inatufundisha Usiamini Mtu hata kama Atakuonyesha upendo wa hali ya juu
Kati ya mwaka 2013 hadi 2015 mwanadada Catherine perez shakdam raia wa Ufaransa aliingia nchini Iran kutokana na kuvutiwa sana na siasa za Iran za kutokubali kushindwa mbele ya nchi zenye nguvu pamoja na Israel, Catherine ambae alibadili dini akiwa Ufaransa na kuwa muislamu wa dhehebu la kishia alianza kuandika makala nyingi za kuisifia serikali ya Iran na uongozi wa Ayatollah Khamenei kwa ujumla , kutokana na maandiko yake kwenye kurasa za kimataifa kuhusu Iran Catherine alipata kazi kwenye idara ya habari ya taifa ya Iran na kuwa mwandishi wa habari tegemezi na wakuaminika sana nchini Iran
Catherine aliweza kufanya mahojiano na wakuu mbalimbali wa Iran na wa kijeshi wa Iran , ikiwemo raisi wa Iran aliyepita Ibrahim raisi
Kutokana na uaminifu huo Iran ilimteua Catherine kuwa mmoja wa washauri wa serikali ya Iran hivyo akawa anatembea sehemu mbalimbali na kuwa na ukaribu na washauri wa Ayatollah Khamenei , Catherine alikuwa na tabia ya kusoma sana Quran usiku kitendo ambacho kilimvutia mshauri wa Ayatollah Khamenei bwana Murtadha alavi na kuwafanya wawili hao kuwa pamoja sana, kutokana na taaluma yake ya habari Catherine alijikuta akimhoji bwana alavi vitu vingi vya siri na alavi akawa anampa ushirikiano mzuri kwenye maongezi yao, alavi alimwambia Catherine Kila kitu kuhusu Hezbollah, Syria na namna Iran inavyotoa silaha na fedha kwa vikundi hivyo pamoja na vikundi vya iraq, ushawishi wake nchini Syria na malengo mengi ya Iran huko mashariki ya kati
Catherine pia akaja kufanya mazungumzo na Kiongozi mmoja wa jeshi ambae nae akamwambia Kila kitu kuhusu vinu vya nyuklia vya Iran pamoja na kipya cha natanz, Kila kilichokuwa kinaendelea kwenye kambi za kijeshi na vituo vya nyuklia Catherine alikuwa anajua.
Mwaka 2019 mwishoni ( kumbuka aliingia Iran kwenye miaka ya 2013-15) Kamera za ulinzi za makao makuu ya shirika la utangazaji la Iran zilimuona akitembea usiku sana akiwa peke yake huku akiwa na begi dogo, taratibu ikaanza minong'ono kuhusu tabia zake , idara ya ujasusi ya Iran ikaanza kumchunguza kwa karibu Catherine , mmoja wa washauri wa raisi wa kipindi hicho wa Iran alimpa taarifa namna timu ya usalama wa Taifa ilivyoanza kumfatilia
Mmoja wa washauri wa raisi wa wakazi huo alimpa taarifa namna timu ya usalama wa Taifa ilivyoanza kumfatilia
Kwanza alitambulishwa kwa kijana wa kiiran aitwae Abbas Lotfi ambae nae ni mtafiti wa dini na siasa pia Abbas hupenda sana kufanya mazungumzo na wanahabari wa kigeni wanaojihusisha na siasa za Iran na dini kama ilivyoyeye Catherine , Moja kati ya maswali ya Abbas kwa Catherine ilikuwa ni kipi kilichomfanya Catherine kuzipenda siasa za Iran na kuamua kwenda kufanya kazi zake za uandishi kuliko kwenda kwenye nchi nyingine za kiislamu duniani? Pia Abbas alimuuliza namna Catherine alivyosomea elimu ya kiislamu nchini Yemen ( ndivyo wasifu wa Catherine unavyosema) na ni kiongozi gani wa dini wa Yemen anavutiwa nae zaidi? Hayo yalikuwa
ni maswali yaliyotaka majibu ya hapo kwa hapo, Catherine aliweza kumjibu vizuri Abbas na kisha kuondoka, nyumbani alikutana na ujumbe " tunakutazama"
Kisha likaja katazo dhidi yake la kutoruhusiwa kutoka nje ya Iran
Hata hivyo zikaja taarifa za kuwa Catherine amefanikiwa kutoroka nchini Iran, waliomuona mwishoni wanasema alivaa vaji la abaya na kwenda kupanda ndege ya shirika la Qatar akiwa na begi dogo lililokuwa na peni pekee
Baadae ikajakufahamika kuwa Catherine perez shakdam alikuwa ni jasusi wa idara ya usalama ya Israel MOSSAD na alikuwa anarekodi kila mahojiano aliyokuwa anayafanya kupitia peni yake, huku kila jioni akiandaa ripoti zote za ujasusi na kuzituma nchini Israel kila mwisho wa wiki, Catherine alikuwa na VPN maalumu inayotumiwa na Mossad ili kufungua mitandao akiwa kwenye maeneo ambayo mitandao ilikuwa imedhibitiwa na serikali ya Iran pamoja na kunasa mawasiliano ya sehemu husika.
Baadhi ya taarifa muhimu ambazo Catherine alizituma kwa Israel ni
*Njia inayotumiwa na Iran kufanya ufadhili kwa Hezbollah
*Majina ya maofisa wa Lebanon wanaopokea fedha kwa Iran kwaajili ya Hezbollah
*Idadi ya askari wa Hezbollah
*Mipango ya Iran kwa Hezbollah
*Namna Iran inavyojiimarisha nchini Syria
- Vikosi vya Iran nchini Syria
- Ufadhili wa Iran kwa wahouthi
- Ufadhili wa Iran kwenye vikundi vya wanamgambo wa Iraq
Baada ya kutokea vita vya siku 12 kati ya Iran na Israel imefahamika kuwa Catherine ndie aliyetoa ramani zote na taarifa zote muhimu kuhusu vituo vya nyuklia vya Iran
- Majina mengi ya wanasayansi wa nyuklia wa Iran
- Makazi ya viongozi wakubwa wa jeshi na usalama wa Iran
- Catherine ndie aliyekuwa ana funga gps kwenye vituo vya nyuklia (ama alikuwa anategesha) vilivyolipuliwa na Israel
- Taarifa zake ndizo zilizotumika kwenye kifo cha mkuu wa majeshi wa Iran
- Mashambulizi mengi ya Israel kwenye vita na Iran yametokana na ujasusi wa Catherine
Inaaminika Catherine huenda alikuwa anatumia tendo la ngono kuwahadaa baadhi ya maofisa wa serikali na jeshi kiasi cha kufanikiwa kuzipata taarifa nyingi na nyeti , kwa mfano wakati imeanza minong'ono kuhusu yeye afisa mmoja mkubwa kwenye shirika la utangazaji la Taifa alimtetea sana
Kwa sasa Catherine yupo nchini Israel.
View: https://youtu.be/EN9DA5Kx7YU?feature=shared
Cn P