Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #41
Nzuri Sana
🙏🏾🙏🏾
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nzuri Sana
kuna uzi niliandika 2021 kuhusu namna ya ku behave ktk eneo lako la makazi.umegusa mulemule nilimogusa.Ujasusi kwenye Makazi[/I][/B]
Elewa eneo unapoishi na wakazi wake vizuri Kabisa. Usipende watu wakujue Sana na wakuzoee Sana. Nawe usiwazoee Sana Ila jitahidi uwajue Kwa namna ya Akili. Zingatia adui WA Mtu hatoki Mbali. Hivyo vyovyote utakavyofanya jua kuwa adui wako yupo katika mzunguko wako. Hivyo usiwe mtu wa kuji-expose Kwa watu.
Shida zako au mafanikio yako. Jua nani ni mke wa Mtu Nani siye kama bado haujaoa. Kamwe usiingize Demu WA hapo mtaani chumbani kwako. Kama utaweza usidate na warembo wa mtaani ulipopangisha,
Hakikisha unajua wahuni wote wa mtaa. Hii itakusaidia kiusalama. Kama ni kijana hakikisha hata kama unauwezo na unafanya kazi yenye kipato cha Kati. Hakikisha unajua vichochoro vyote vya mtaa wenu, siku za wikiend toka zurura Kwa mguu unanyoosha miguu ukipita kwenye njia na vichochoro vyote vya mtaa. Sio kwa siku moja. Bali wikiend hii unapita kichochoro Hilo, wikiendi hii kichochoro kile. Ujue vinatokea wapi.
Elewa jina la mtaa na majina ya watu maarufu
Usipende kuomba omba vitu, wala usipende watu wakusogelee kukuombaomba vitu. Mazoea mazoea Epuka Sana. Kama umepanga usipende vitoto vidogo vya jirani kuingia ingia chumbani au kwako. Usipende watu majirani kuingia ingia kwako. Acha uswahili Swahili. Halikadhalika usipende kuingia kwenye majumba ya watu.
Usipende kukopesha kopesha watu unaoishi nao. Kiufupi usipokuwa na mazoea Sana na watu ni ngumu watu kuja kuwakopa. Ila pia uwe mtu wa kutoa misaada Kwa wanaohitaji misaada.
4. Ujasusi Eneo la kazi
Hakikisha unajifunza Saikolojia ya binadamu, body language, maana ya sauti ya matamshi ya watu wanapozungumza. Ni rahisi mtu kujua utafukuzwa kazi lini kama utakuwa makini na mambo hayo. Ni nadra Sana mtu atukuzwe kazi ghafla kabla Boss au mkurugenzi hajaandaa mpango wa kumfukuza kazi. Nadra Sana.
Taarifa nyeti zinazohusu Future za Ofisi unazofanyia kazi ni muhimu kwako Kama mfanyakazi, Usiishi Kama Kuku asiyejua kesho kitatokea nini. Ingawaje tumia akili Sana kuzipata hizo taarifa. Na hata ukizipata usizitoe Kwa watu. Ujasusi Una kanuni muhimu ya usiri.
Mambo ya nyumbani usilete Ofisini. Na mambo ya Kazini usilete nyumbani. Wewe Kama ni Boss mahali unapofanyia kazi usilete Uboss wako Mtaani, utakwama. Sifa mojawapo ya ujasusi ni kuwa Normal, isipokuwa kama inawezekana kuwa Low-key.
Ukileta Uboss wako mahali unapoishi utakwama Maeneo mengi mno. Hasa kiuchumi, hautakuwa huru. Ukipata shida labda ya kutengenezewa kitu fulani sio ajabu ukalipishwa pesa nyingi kutokana na kuletaleta uboss wako wa kijinga. Ni Kheri utoe Pesa Kwa moyo mmoja lakini sio Kwa kupigwa. Ukileta uboss mtaani itakufanya usiwatambue wanaokuzunguka Kwa usahihi kabisa yaani kuna hatari ya kupata taarifa za uongo. Wengi watakuigizia au ku-pretend kama sio kuwa Wanafiki.
Ukileta Uboss au usomi wako mahali unapoishi utajikuta unakuwa mtumwa na haupo huru hata kuongea Pumba au mambo ya kipuuzi. Unajua sio muda wote unapaswa uongee mambo ya maana.
Mtibelii
kuna uzi niliandika 2021 kuhusu namna ya ku behave ktk eneo lako la makazi.umegusa mulemule nilimogusa.
unaweza kuupitia:
'Street codes' za kukusaidia uishi vizuri na watu mtaani kwako katika mji wowote Tanzania
lazima niwe jasusi aisee
Kuna uzi wako nautafuta unazungumzia tabia ya watu (vijana)kuendekeza utoto! Unakuta kijanaa ana miaka 20, 21 n k anashindwa kufanya na kupuuza vitu vya maana akitumiia utoto kama scapegoat.Naam Mkuu
Barikiwa sanaUzi mzuri sana