Rihanna Kwa sasa ana umri wa miaka 34, baada ya kufanya kazi ya kutafuta pesa Kwa bidii na kwa muda mrefu mpaka kufikia kuwa bilionea, nadhani sasa amejiandaa kulea
Rihanna amechagua wa kuzaa nae, amechagua muda wa kuzaa, na anaenjoy Mimba yake,yote afanyayo Kwa sasa ni Kwa sababu anafurahia kuja kuitwa Mama
Turudi kwetu, wadada wengi wanapata mimba wakiwa hawana mbele wala nyuma,wanazaa na watu wasio chaguo Lao,wanapata mimba wakiwa ktk umri mdogo, hivo ni ngumu kukuta mdada anafurahia Mimba yake zaidi ya malalamiko Tu
Ukikuta mtu amepata Mimba ktk wakati sahihi na mtu sahihi lazima utamuona Tu vile anaenjoy kuwa na Mimba, tofauti ni kwamba hawezi kutembea tumbo wazi km Rihanna kutokana na mila zetu ila ukimuona tu unajua huyu anaenjoy, kwahiyo Mleta mada we achana nae tu huyo kwani anafanya kwa Raha zake