Ujenzi Barabara ya Segerea-Bonyokwa-Kimara waanza baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu

Ujenzi Barabara ya Segerea-Bonyokwa-Kimara waanza baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Habari wakuu,

Hii barabara kuanzia Segerea-Bonyokwa mpaka Kimara kwa sisi wakazi wa maeneo hayo ilikuwa kero kubwa sana sababu kutokana na ubovu wake hasa kipindi cha mvua. Hii barabara imekuwa ikilalamikiwa miaka na miaka lakini serikali ilikuwa imeziba masikio lakini sasa kilio kimewafikia. Hii barabara ni muhimu sana kutokana na kwamba inaunganisha Tabata Segerea na Kimara.

Juzi nimepita Bonyokwa nikakuta mkandarasi yupo site pale mwisho wa lami, nilifarijika sana. Eneo lile kuanzia kibao cha Shule ya Msingi Macedonia mpaka stendi ya Bonyokwa ilikuwa korofi sana kutokana na kukosa mifereji hivyo maji yalikuwa yakijitafutia njia. Nakumbuka kijana wangu aliachwa pale na school bus kisa ubovu wa barabara akaambiwa atembee kwenda nyumbani umbali kama kilometa 2.

Ujenzi huo utachochea sana maendeleo ya eneo lile na hatimaye tutaachwa kuchekwa watu wa Bonyokwa.

Pia soma

B1.jpg
B4.jpg
 
Utakua mgeni huku Bonyokwa kwetu [emoji23]

Yaani kuna mtu Ana ulaji wake pale kila baada ya muda anapita kulima barabara Kama Shamba la viazi..inaharibika analima tena .
 
Wanarekebishaa tuu kuzuga mzee hakuna ujenzi hapooo..
 
Utakua mgeni huku Bonyokwa kwetu [emoji23]

Yaani kuna mtu Ana ulaji wake pale kila baada ya muda anapita kulima barabara Kama Shamba la viazi..inaharibika analima tena .
itakuwa dalali aliempangishaa alimletaa kipindi hiki jamaa akaenda kwa kichwaa sasa subiri mvua inyesheee atajuaa hajuii 😀 😀 😀 😀 😀 atajua HAISHI DAR
 
itakuwa dalali aliempangishaa alimletaa kipindi hiki jamaa akaenda kwa kichwaa sasa subiri mvua inyesheee atajuaa hajuii 😀 😀 😀 😀 😀 atajua HAISHI DAR

Leo nimetoka huko G7
Hamna Ujenzi pale ni zuga tu
 
Na hii ya kutoka mbezi stend ya magufuli kwenda mpiji mpaka Bunju B lini wataanza
 
Back
Top Bottom