Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Naanza kumaizi kuwa upo umuhimu wa jamii yetu kujifunza maarifa ya ujenzi wa hoja ili kupunguza mitindinganyo ya hoja inayoendelea jambo linalowapa nafasi wachache wanaojua kujenga na kubomoa hoja hata kama wakisimamia hoja dhaifu.
Nimefuatilia majibizano mengi ya hoja na nilichoweza kubaini ni ukweli kuwa viongozi wengi wanapenda kuvuta utayari wa Umma " public attention" ila hawana uwezo wa kujenga hoja imara au kubomoa hoja kinzani.
Kuna hoja nyingi zenye nguvu zinazoibuliwa na watu mbalimbali na nyingine zipo katika mkao wa tuhuma ila majibu yanayotolewa na wenye nyadhifa husika yanazipa hoja hizi uhalali wa kujadiliwa zaidi.
Siyo kila hoja au tuhuma inayotolewa inapaswa kujibiwa kwa wakati huohuo, na siyo kila jibu linalokuja linapaswa kutolewa waziwazi kwa Umma.
Ikumbukwe jamii yetu ya kileo ina uelewa mpana sana wa masuala mbalimbali, teknolojia, maarifa na ufambaaji wa taarifa mbalimbali kwa Kasi ya mwanga ni mambo yanayoifanya jamii kuwa hai kuliko wengi wanavyodhani.