Ujenzi rahisi kwa kutumia interlock blocks, jenga popote, jenga sasa

Ujenzi rahisi kwa kutumia interlock blocks, jenga popote, jenga sasa

Hizi tofali huwa zina momonyoka sana..hasa zilizochini kwenye msingi..hasa zikinyeshewa mvua ama unyevu nyevu kwa muda mrefu.

Mleta uzi toa solution kwa tatizo hilo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hizi tofali huwa zina momonyoka sana..hasa zilizochini kwenye msingi..hasa zikinyeshewa mvua ama unyevu nyevu kwa muda mrefu.

Mleta uzi toa solution kwa tatizo hilo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Msingi unaoigwa na za kawaida na inapigwa matitio fulani maji hayapenyi
 
20220831_130411.jpg
 
IMG_20220713_141801.jpg
kanuni zile zile za ujenzi ila tu unafuu tofauti. Hakuna haja ya jukwaa.
 
Interlock blocks au bricks ni aina ya tofali zinazofungamana kwenye ujenzi bila kutumia zege(motor) kuziunganisha,zinapigwa kwa saruji na udongo wenye mfinyazi kiasi. Tofali hizi zinatumia saruji kidogo sana(10%) tu ya udongo. Hizi tofali zipo miundo mingi sana lakini nitazungumzia aina ya Hydraform.
View attachment 2303148
Hydraform ndio waasisi wa teknolojia hii ya tofali lakini kulingana na soko kila sehemu wanatengeneza mashine.

Aina hii ni maarufu sana Tanzania
Mashine ya kupiga Hydraform inatumia hydrolic ambayo ina uwezo wa kupiga tofali zaidi ya 2000 kwa siku kwa kinu kimoja.

View attachment 2303149
Kuna mashine za mkono pia ambazo kwa kinu kimoja kinapiga tofali 400.
Uzuri wa Hydraform unapiga size unazotaka za urefu wa tofali na vipande vyake bila kuja kukata wakati wa ujenzi.
Urefu wa tofali huanzia nchi 18-24 na upana ni nchi 9 na 6 na kimo ni nchi 5.
Mfuko mmoja wa saruji unaweza kupiga tofali 80 mpaka 100 ikitegemea na aina ya udongo uliopo eneo lako.

URAHISI WA UJENZI WAKE HUU
1.Baada ya kuwa na tofali kinachofuata ni ujenzi au kupandisha boma lako. Tofali ya kwanza baada ya msingi ni kuset boma. Ujenzi wake ni rahisi kwa sababu hakuna haja ya motor kwenye kupandisha boma lako,utapachika tu ila utazingatia kanuni zote za ujenzi.

2.Hakuna haja ya plasta na skim baada ya ujenzi wako,hapo utaokoa saruji,mchanga,maji na gharama za fundi.

3.Kuhimili mitikisiko na vishindo hivyo si rahisi kuona nyumba hizi zikiwa na ufa sababu tofali zinapumua. Kama itatokea tetemeko au bomoa bomoa unaweza kuhama na tofali zako.

Faida ziko nyingi na kitaalamu ujenzi wa tofali za kufungamana unapunguza 40% ya gharama za ujenzi, mfano kama ulipanga kujenga kwa milioni 10 basi huenda ukatumia milioni 6 tu.

Karibu kwa mnaotaka kujenga,iwe ni kwa awamu kulingana na uwezo wako au kwa pamoja pia. Gharama zetu ni rafiki kabisa.

Kama una fundi wako karibu tukuuzie tofali. Kuna option mbili za kupata tofali.
1.Tofali moja tutakuuzia Tsh.650 kwa ndani ya Dar na maeneo ya jirani mikoani tutaelewana tu.
2. Tunaweza kukupigia tofali kwa Tsh. 250 ikiwa utanunua matirio yote mwenyewe.


View attachment 2303152

Kama una maoni au swali karibu uulize na utajibiwa iwezekanavyo.

MAWASILIANO YETU
Tupigie simu au WhatsApp 0625547181
Telegram t.me/ujenzirahisi
Facebook @ujenzirahisi
Instagram @ujenzirahisi
Tiktok @ujenzirahisi
KARIBU UJENZIRAHISI TUKUJENGEE UTAKAVYO,IWE NI KIDOGO KIDOGO AU KWA PAMOJA
Mkuu hongera kwa tangazo zuri. Hebu pia waeleze wadau changamoto za kutumia huu mfumo (interlocking) hasa ikitokea unataka kubadilisha mpangilio wa vyumba au kufanya partition au kubadili mfumo wa maji taka baada ya ujenzi kukamilika.
Ahsante
 
Mkuu hongera kwa tangazo zuri. Hebu pia waeleze wadau changamoto za kutumia huu mfumo (interlocking) hasa ikitokea unataka kubadilisha mpangilio wa vyumba au kufanya partition au kubadili mfumo wa maji taka baada ya ujenzi kukamilika.
Ahsante
Changamoto mkuu ni kupata tofali tu zote, kama mashine itatumika hydraform basi wateja wengi huona ni gharama sababu unatakiwa kuwa na matirio yote site, wengine wanataka kupiga kidogo kidogo jambo ambalo wanakata tamaa...bila kukumbuka ukishapata tofali zako swala la kujenga ni haraka na nafuu zaidi.

Kuhusu kugawa parttion ni rahisi haswa sababu unapagua tofali zako na kuzipanga utakavyo tu kulinga na jinsi unayoona inafaa tena kwa wenye ghorofa ni rahisi sana kugawa ofisi.
 
Back
Top Bottom