SoC04 Ujenzi/upanuzi wa madarasa mapya ya shule za kata kila mwaka na kubana maeneo ya michezo

SoC04 Ujenzi/upanuzi wa madarasa mapya ya shule za kata kila mwaka na kubana maeneo ya michezo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Martin Mwamba

New Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Naipongeza serikali kwa ujenzi wa shule za kata kwa nchi yetu ya Tanzania kila wilaya kwasasa wanafunzi wetu wanapofaulu wanauhakika wa kuendelea na kidato cha kwanza pia na ukaribu wa sehemu wanazoishi. Hii imeondoa adha ya ukatili wa kijinsia na kuwajengea weledi watoto.

Hoja yangu ni Hii; Kila mwaka Serikali inajenga shule ya kata au kupanua shule kwenye eneo moja ambalo kuna shule ya kwanza. Kwasasa maeneo mengi ya shule yamepimwa yakiwa na viwanja vya michezo mbalimbali vinavotumika na wanafunzi pia jamii inayowazunguka.

Sasa upanuzi wa shule mpya au madarasa mapya kwenye shule hizi yamepelekea kuondoa viwanja vya michezo au kuvifinya na kuwa vidogo ambavyo avikidhi kwa michezo na eneo kubwa kujaa madalasa mapya.

Sasa ujenzi huu hufanyika kila mwaka kulingana na matokeo ya ufaulu ya dalasa la saba yanapoongezeka kila mwaka.sasa atuwezi kila mwaka tukajenga au kupanua madalasa mapya kwenye eneo moja na kujenga kwenye maeneo ya michezo yaliyobakia.

Sasa hatuwezi kuwa na kiwanja kimoja ambacho pia hakina mita za mraba sahihi kitumike kwa michezo yote ya shule riadha,mpira na netboll kwa wakati mmoja.

Shule nyingi za jijini Dar es Salaam kwasasa viwanja vyake vya michezo vimebaki vinyu yani vidogo kutokana na ujenzi wa kila mwaka wa maadalasa na watoto wanakosa haki yao ya michezo mfano Nguvu Mpya iliyopo Chanika Dar es Salaam.

Ushauri wangu; kwanini tusiwe na mpango mkakati wa miaka 10 ijayo kwa watoto wetu tukijua kuna ongezeko la watu na ufaulu yani shule zote mpya tujenge mfumo wa ghorofa ili kuchukua nafasi ndogo pia sio radhima iwe na floor 2 au 3.

Tunaweza kuanza floor moja ukiwa msingi wetu wa jengo ambao kila mwaka ufaulu unapoongezeka na ujenzi wa madarasa mengine yanafanyika juu ya ujenzi ule wa ghorofa.tunajikuta tunaweza kutengeneza madarasa ya maghorofa na tukachukua ardhi ndogo na tukawa na vyumba vingi kwenda juu.

Hii itaondoa mlundikao wa shule kwenye kata moja ambao pia unabana au kuchukua nafasi ya viwanja. Mfano shule ya Minazi Mirefu ipo Ukonga, Banana hii kwasasa inajengwa kwa mfumo wa ghorofa na imechukua nafasi ndogo hata wakitaka kupanua madarasa juu kuna muendelezo.

Naona kuna haja kila shule mpya ikijengwa iwe na msingi wa ghorofa ili kuruhusu upanuzi wa madarasa kila mwaka kuendana na kasi ya ufaulu na kuondoa mrundikano wa shule na kubana maeneo ya michezo.
 
Upvote 2
Ushauri wangu; kwanini tusiwe na mpango mkakati wa miaka 10 ijayo kwa watoto wetu tukijua kuna ongezeko la watu na ufaulu yani shule zote mpya tujenge mfumo wa ghorofa ili kuchukua nafasi ndogo pia sio radhima iwe na floor 2 au 3.
Bonge la idea lipo hapa.

Halafu ukiangalia huko ndiko tulikoanzia, ila sasa ndio tunarudi nyuma. Shule zote zilikuwa zinajengwa maghorofa. Kibaha, Kilosa, Kigonsera, Kilakara, pote tu shule ni ghorofa.

Kuna haja turejee kwenye ujenzi wa namna hiyo tena
Naona kuna haja kila shule mpya ikijengwa iwe na msingi wa ghorofa ili kuruhusu upanuzi wa madarasa kila mwaka kuendana na kasi ya ufaulu na kuondoa mrundikano wa shule na kubana maeneo ya michezo.
Nakubali, tuwasubiri mainjinia na maplanner sasa watujibu.

Ila wazo la taasisi kuwa za ghorofa. Asee li.esimama saana
 
Sio kwa CCM hii ya akina Nape!
 
Back
Top Bottom