Ujenzi huu wa Bandari ya Bagamoyo unakiua wosia wa mwendazake !!
My take: CCM haina consistence ya ujenzi wa Taifa letu, kila awamu unakuja na mambo yake namna hii tunaumia ni sisi wananchi. Kwa mfano JK alianzisha bomba la Gesi mtwara, Magu alivyoingia haikuwa priority yake yeye akaachana na umeme wa gesi anageukia umeme wa maji, Maza naye kaugeukia mradi wa Bagamoyo ambao Magu aliupinga vikali.
Hii si sawa, tunaoumia kwa maamuzi haya ni sisi wananchi, kama Magu angeendelea kuongeza capacity ya Gesi ya mtwala kutoka 6% aliyoishia JK nafikiri kwa sasa tungekuwa 50% na kusingekuwa na mgawo huu.
Kuisimamia Serikali kwenye maamuzi yenye tija kwa Taifa ni kazi ya Bunge, sasa Bunge nalo ndugu zangu kama mnavyojua - imeshakuwa kikao cha kupitisha miswaada ya serikali kwa justification tu, hakuna kuuliza why & how - unapataje maendeleo katika nchi kwa mwenendo huu.
Sasa tukisema tuna tatizo kubwa la KATIBA yetu, mnabisha - mnaona sasa mambo yalivyo sasa !!