Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi 2023

Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi 2023

Upotevu wa pesa za bure kuwafurahisha wakina kikwete. Bandari ya Tanga ambayo tayari kuna mafuta ya uganda yanakuja tusijenge pale tutumie pesa kujenga bandari ya pili Dar. Hii ni miradi binafsi
Hata ya mtwara wangeiboresha nako kule uchumi ukue na kupunguza msongamano Mana hii Moro road Ni balaa kwa magari.
 
Hivi mradi wa bandali ya kwale umeushia wapi?
Mwaka 2019 tuliona mpaka makontena yanaletwa na wakasema bado barabara.sasa barabara ndio ukwamishe huo mradi.
 
Huu utapeli wa kijinga, hatuna uwezo wa kujenga bandari itakayogharimu $10b, reli na bwawa lenyewe ni mwendo wa kinyonga, ndio itakuwa bandari ya $10b? Sana sana waseme watasafisha eneo linalotarajiwa bandari kujengwa.

Wawekezaji wamekimbia?
 
Ukweli ya pale dar ni ndogo sana. Eneo lilotengwa kuhifadhi mizigo nalo pia ni changamoto halitupi kilichosahihi.

Tujenge bagamoyo kubwa na yenye ukubwa stahiki tuchochoe soko letu na nchi za karibu. Pia tutazame mifumo yetu ya kodi bandali

Ile ya dar tunaweza itumia kwa ajili usafirishaji kwenda maeneo karibu mfano Comoro
 
Wenyewe hatuwezi ni pesa ndefu sana.

Ndio maana wameongelea issue ya wawekezaji kuungana nasi wakati bandari inaendelea kujengwa.

Hakuna cha kuungana ndugu, hao wanatafuta kiki tu. Kuungana inatakiwa sisi wangalau tutoe $3b ambazo hatuna, na nyingine watoe hao wawekezaji. Sasa ufyeke vichaka kisha useme kuna muwekezaji anakuja kujiunga na ww?!
 
Hivi hawa wanaofanya ufisadi wa kutisha namna hii hawajui kuwa hawataondoka na hata senti moja??
 
Hakuna cha kuungana ndugu, hao wanatafuta kiki tu. Kuungana inatakiwa sisi wangalau tutoe $3b ambazo hatuna, na nyingine watoe hao wawekezaji. Sasa ufyeke vichaka kisha useme kuna muwekezaji anakuja kujiunga na ww?!
Mimi nadhani kuna jambo nyuma ya pazia serikali inalijua ila inatuficha.

Wawekezaji wenyewe tumefichwa kwa kuwa wapo kwenye hatua za awali za majadiliano.

Kwani kuwataja wawekezaji mnaojadiliana nao ni kosa?

Yote kwa yote huu mradi serikali iache utani iweke pesa ya kutosha ili tuwe na share ya kueleweka.
 
Hivi hawa wanaofanya ufisadi wa kutisha namna hii hawajui kuwa hawataondoka na hata senti moja??
Kibaya zaidi.

Wengi kama si wote wanaofanya ufisadi ni wanachama wa chama chako pendwa cha CCM.
 
Hii miradi ya watu kutokana na masharti waliyokwisha jifunga, hivyo juhudi mahususi zinafanyika ili kutimiza adhima hiyo ambayo hakika kama nchi itakuwa ni mzigo mkubwa kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom