Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi 2023

Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi 2023

Mimi nadhani kuna jambo nyuma ya pazia serikali inalijua ila inatuficha.

Wawekezaji wenyewe tumefichwa kwa kuwa wapo kwenye hatua za awali za majadiliano.

Kwani kuwataja wawekezaji mnaojadiliana nao ni kosa?

Yote kwa yote huu mradi serikali iache utani iweke pesa ya kutosha ili tuwe na share ya kueleweka.
Kitu ambacho nashindwa kuelewa ni hii kuficha ficha mambo , Mbona nchi za wenzetu utakuta wanafanya maongezi ya kufanya biashara Kwa pamoja lakini wananchi wanaambiwa kabisa kuwa tunafanya maongezi na kampuni hii na hii, Sijajua mwananchi Kwa tanzania tunachukuliawaje na serikali yetu wenyewe? Sisi raia wa Tanzania serikali yetu wanatuchkulia kama vile hatuna umuhimu wowote wakati nchi ni raia na siyo nchi ni viongozi , kila kitu wanatuficha ficha na pale wakimaliza wanakuja tu na kusema tayari kampuni hii inafanya Hivi na vile na hakuna mtanzania hata mmoja anaweza hata kupinga yaani wakishaamua wao Basi
 
Nimeshangaa kwa kweli.

Muwekezaji kafichwa sababu majadiliano yapo hatua za awali.
 
Hivi ukiulizwa sababu hasa inayofanya bandari za Tanga, Dar na Mtwara zionekane haifai ila suluhisho ni kuanza kujenga mpya unajua?
Kiukweli hiyo sababu haipo. Aliyekuwa mkurugenzi wa TPA aliwahi kuhoji hayo mwisho wa siku alisingiziwa mambo mengi akafukuzwa kazi akawekwa rumande kwa zaidi ya mwaka juzi nasikia walimfikisha mahakamani. Yeye hakuona sababu ya kuanzisha bandari ya Bagamoyo wakati za Dar, Mtwara na Tanga zipo. Pia alihoji kuwa wale wachina kama ilikuwa ni lazima wapewe wajenge halafu warudishe pesa yao kwa kuimiliki hiyo bandari ya Bagamoyo basi chini ya miaka 10 wangerudish pesa yao yote na sio miaka 99 iliyokuwa kwenye mkataba alioshtukia rais wa awamu ya 5. Matokeo yake yanafahamika. Ila naona Mungu ametupigania mno kama zinakuja hoja za TPA au serikali kuijenga badala ya wale wachina
 
Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo katika mwaka ujao wa fedha. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa alibainisha jana kuwa hawatalazimika kusubiri zaidi wawekezaji kuanza ujenzi wa bandari hiyo.

"Wawekezaji wataungana nasi njiani," Bw Mbossa alisema wakati wa mkutano na bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) uliofanyika hapa katika Makao Makuu ya TPA. Alikariri kuwa kampuni kadhaa za kimataifa zimeonyesha nia ya kuendeleza na kuendesha mradi wa bandari ya Bagamoyo wenye thamani ya dola bilioni 10 (takriban Sh23 trilioni).

Bw Mbossa hakutaja majina ya kampuni hizo kwa madai kuwa bado ziko katika hatua ya awali ya ushiriki. "Tumejitolea kujenga bandari ya Bagamoyo katika jitihada za kupunguza msongamano wa bandari ya Dar es Salaam na kuvutia wateja wetu," alisisitiza.

Takwimu rasmi zinasema kuwa bandari ya Dar inahudumia tani milioni 17.025 za mizigo kwa mwaka na mpango wa sasa ni kuongezeka hadi tani milioni 30 ifikapo 2030. "Tuko hapa kusaidia mkoa. Bado tuna changamoto kama vile msongamano, lakini tunafanya kila tuwezalo kuzitatua,” alikiri Bw Mbossa.

TPA, alisema inaangalia mfumo wake wa kisheria ili kutatua changamoto zinazokwamisha utendaji kazi wa bandari ya Dar. Alisema wanafanya kazi na mashirika kadhaa ambayo ni pamoja na, lakini sio tu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).

"Kama nchi, tunajitahidi tuwezavyo kuboresha usafiri wa aina mbalimbali ili kutoa fursa kwa wateja wetu kutumia vifaa kwa gharama ya chini," alisimulia Bw Mbossa. "Pia tunafanya kazi ili kuunda uwezekano wa kutabirika linapokuja suala la malipo yanayohusiana na uhifadhi na uondoaji," alisema.

Pia alisema walikuwa wakiimarisha na kuongeza kina cha gati ili kukidhi meli kubwa zaidi. Kwa sasa, bandari ya Dar inaweza kubeba meli zinazoshughulikia vitengo 6,000 hadi 8,000 sawa na futi ishirini (TEUs), uboreshaji ikilinganishwa na TEU 2,000 zilizopita.

"Tukiwa na meli kubwa zaidi, wateja wetu watapata nafasi ya kufurahia uchumi wa hali ya juu. Tunafanya haya yote (maboresho) ili kupata ufanisi unaohitajika na wateja wetu," bosi huyo wa TPA alisema. Katika mwaka huu wa fedha, alisema, Sh10 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa.

Akizungumza awali, Mwenyekiti wa EABC, Bi Angelina Ngalula, alisema sekta binafsi katika mkoa huo imedhamiria kutumia bandari ya Dar. Alisema ili bandari ya Dar ivutie watumiaji wengi, kunapaswa kuwepo na uratibu mzuri na taasisi nyingine zinazotoa huduma bandarini ili matatizo yasiyo ya lazima yaweze kutatuliwa.

“TPA imesafisha nyumba yake. Lakini biashara zinapokabiliana na changamoto bandarini, ni (TPA) ndiyo iliyonyooshewa kidole cha lawama,” aliona Bi Ngalula. "Unahitaji kukuza utaratibu bora wa uratibu."
Hii inahusiana na ile waliyotaka kujenga wachina enzi za jiwe au tofauti?
 
Kiukweli hiyo sababu haipo. Aliyekuwa mkurugenzi wa TPA aliwahi kuhoji hayo mwisho wa siku alisingiziwa mambo mengi akafukuzwa kazi akawekwa rumande kwa zaidi ya mwaka juzi nasikia walimfikisha mahakamani. Yeye hakuona sababu ya kuanzisha bandari ya Bagamoyo wakati za Dar, Mtwara na Tanga zipo. Pia alihoji kuwa wale wachina kama ilikuwa ni lazima wapewe wajenge halafu warudishe pesa yao kwa kuimiliki hiyo bandari ya Bagamoyo basi chini ya miaka 10 wangerudish pesa yao yote na sio miaka 99 iliyokuwa kwenye mkataba alioshtukia rais wa awamu ya 5. Matokeo yake yanafahamika. Ila naona Mungu ametupigania mno kama zinakuja hoja za TPA au serikali kuijenga badala ya wale wachina
Siyo changa la macho kweli? Naona kuna namna. Ile sehemu kuna watu wanaimezea mate sana. Kusema TPA au serikali ndiyo itajenga pale mimi nitakuwa wa mwisho kuamini. Hebu tusubiri tuone.
 
Siyo changa la macho kweli? Naona kuna namna. Ile sehemu kuna watu wanaimezea mate sana. Kusema TPA au serikali ndiyo itajenga pale mimi nitakuwa wa mwisho kuamini. Hebu tusubiri tuone.
tusubiri wote ila tuendelee kuiombea hii nchi kwa Mungu wa Mbinguni
 
Naisubiri kwa hamu hii bandari nipihe pesa. Nina kiwanja changu huko Bagamoyo karibu kabisa na eneo itakapojengwa bandari
 
Hivi mradi wa bandali ya kwale umeushia wapi?
Mwaka 2019 tuliona mpaka makontena yanaletwa na wakasema bado barabara.sasa barabara ndio ukwamishe huo mradi.
Hili nalo la Banadari kavu ya Kwala tulilitizama kwenye kikao cha kamati kuu na Mimi Kama Mwenyekiti niliona ni bora lile eneo nimkabidhi Mwanangu Ridhiwan ajenge Godown na Sheli.
 
Hivi mradi wa bandali ya kwale umeushia wapi?
Mwaka 2019 tuliona mpaka makontena yanaletwa na wakasema bado barabara.sasa barabara ndio ukwamishe huo mradi.
Kwala dryport inakaribia kuisha...ile barabara nayo bado kilometer 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom