Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi 2023

Kitu ambacho nashindwa kuelewa ni hii kuficha ficha mambo , Mbona nchi za wenzetu utakuta wanafanya maongezi ya kufanya biashara Kwa pamoja lakini wananchi wanaambiwa kabisa kuwa tunafanya maongezi na kampuni hii na hii, Sijajua mwananchi Kwa tanzania tunachukuliawaje na serikali yetu wenyewe? Sisi raia wa Tanzania serikali yetu wanatuchkulia kama vile hatuna umuhimu wowote wakati nchi ni raia na siyo nchi ni viongozi , kila kitu wanatuficha ficha na pale wakimaliza wanakuja tu na kusema tayari kampuni hii inafanya Hivi na vile na hakuna mtanzania hata mmoja anaweza hata kupinga yaani wakishaamua wao Basi
 
Nimeshangaa kwa kweli.

Muwekezaji kafichwa sababu majadiliano yapo hatua za awali.
 
Hivi ukiulizwa sababu hasa inayofanya bandari za Tanga, Dar na Mtwara zionekane haifai ila suluhisho ni kuanza kujenga mpya unajua?
Kiukweli hiyo sababu haipo. Aliyekuwa mkurugenzi wa TPA aliwahi kuhoji hayo mwisho wa siku alisingiziwa mambo mengi akafukuzwa kazi akawekwa rumande kwa zaidi ya mwaka juzi nasikia walimfikisha mahakamani. Yeye hakuona sababu ya kuanzisha bandari ya Bagamoyo wakati za Dar, Mtwara na Tanga zipo. Pia alihoji kuwa wale wachina kama ilikuwa ni lazima wapewe wajenge halafu warudishe pesa yao kwa kuimiliki hiyo bandari ya Bagamoyo basi chini ya miaka 10 wangerudish pesa yao yote na sio miaka 99 iliyokuwa kwenye mkataba alioshtukia rais wa awamu ya 5. Matokeo yake yanafahamika. Ila naona Mungu ametupigania mno kama zinakuja hoja za TPA au serikali kuijenga badala ya wale wachina
 
Hii inahusiana na ile waliyotaka kujenga wachina enzi za jiwe au tofauti?
 
Siyo changa la macho kweli? Naona kuna namna. Ile sehemu kuna watu wanaimezea mate sana. Kusema TPA au serikali ndiyo itajenga pale mimi nitakuwa wa mwisho kuamini. Hebu tusubiri tuone.
 
Siyo changa la macho kweli? Naona kuna namna. Ile sehemu kuna watu wanaimezea mate sana. Kusema TPA au serikali ndiyo itajenga pale mimi nitakuwa wa mwisho kuamini. Hebu tusubiri tuone.
tusubiri wote ila tuendelee kuiombea hii nchi kwa Mungu wa Mbinguni
 
Naisubiri kwa hamu hii bandari nipihe pesa. Nina kiwanja changu huko Bagamoyo karibu kabisa na eneo itakapojengwa bandari
 
Hivi mradi wa bandali ya kwale umeushia wapi?
Mwaka 2019 tuliona mpaka makontena yanaletwa na wakasema bado barabara.sasa barabara ndio ukwamishe huo mradi.
Hili nalo la Banadari kavu ya Kwala tulilitizama kwenye kikao cha kamati kuu na Mimi Kama Mwenyekiti niliona ni bora lile eneo nimkabidhi Mwanangu Ridhiwan ajenge Godown na Sheli.
 
Hivi mradi wa bandali ya kwale umeushia wapi?
Mwaka 2019 tuliona mpaka makontena yanaletwa na wakasema bado barabara.sasa barabara ndio ukwamishe huo mradi.
Kwala dryport inakaribia kuisha...ile barabara nayo bado kilometer 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…