Ujenzi wa Barabara ya Kwanza ya Njia 6 Waanza Zanzibar

Ujenzi wa Barabara ya Kwanza ya Njia 6 Waanza Zanzibar

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take

Safi sana Wazanzibari Kwa kuamua kujitegemea na kuonesha mfano.

Mzanzibari hajawahi kuwa na sifa ya ubianafsi Wala ufisadi kama ule upande wa watu wenye mdomo sana.

===========================

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Said Bakari amesema Serikali imeanza rasmi utekelezaji wa ujenzi wa Barabara ya Kisauni Fumba kuelekea katika Uwanja wa AFCON unaojengwa eneo la Fumba.

Amesema barabara hiyo itakuwa ya kwanza Zanzibar kuwa na njia sita, ambapo njia nne zitatumika kwa magari ya kawaida na njia mbili maalum zitatengwa kwa ajili ya magari ya umeme.

Katibu Said amesema utekelezaji wa mradi huo unalenga kuimarisha miundombinu ya usafiri na kurahisisha huduma za usafiri kuelekea katika uwanja huo mkubwa wa michezo unaotarajiwa kutumika wakati wa mashindano ya AFCON.

Aidha, amesema ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Serikali kuhakikisha Zanzibar inakuwa na miundombinu ya kisasa inayokidhi mahitaji ya maendeleo pamoja na ongezeko la shughuli za kiuchumi na kijamii.

👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/DYDTPdwuLrc/?igsh=MWcyZXVicjdwdGZmNg==
 
Back
Top Bottom