Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Museveni ametembelea tanzania Kikazi

1600015208652.png


===

Rais John Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania

Rais Magufuli: Tumeshuhudia uwekaji wa saini wa ujenzi wa Bomba hili la Mafuta lenye km 1,445. Hii ni hatua muhimu sana kuelekea utekelezaji wa mradi huu. Ni mradi wa takribani USD 3.5 Billion

Rais Magufuli: Km 330 za bomba hili zipo Uganda. Kwa Tanzania, bomba litapita kwenye mikoa 8, wilaya 24 na kata 132. Tathmini kwa Tanzania, watu zaidi ya 90,000 watalipwa fidia; ni takribani bilioni 21
1600015240819.png


Rais Magufuli: Nampongeza Rais Museveni, amefanya mambo yasiyowezekana! Haya mafuta yasingepatikana Uganda, sisi tusingenufaika. Yawezekana kuna waganda wanaomtukana pamoja na kazi hii nzuri anayofanya!

Rais Magufuli: Mradi huu ulichelewa! Coronavirus ilichelewesha huu mradi, ishindwe kabisa! Jana Mzee Museveni alinipigia simu, akasema Corona isiwe sababu ya mradi kuchelewesha mradi. Alisema atakuja na barakoa, nikamwambia hata uje na blanketi, njoo tu!

Rais Magufuli: Mradi huu wa Bomba la Mafuta ni ushindi wa Pili baada ya Vita vya Kagera. Tulichelewa kidogo katika hili juu ya kugawana faida. Tumekaa chemba dakika 5 chemba tu, nikamwambia Tanzania tupate 60% na 40% iende Uganda - Rais Museveni akakubali

Rais Magufuli: Tunaendelea na utafiti wa mafuta hapa Tanzania, endapo yatapatikana, tutayapitisha kwenye hili bomba. Endapo gesi itaanza kupatikana Tanzania, tutaipeleka Uganda sambamba na hili Bomba la Mafuta
1600015264061.png


Rais Museveni: Nilitumia wataalamu wetu tangu mwanzo hadi mwisho, watu wa nje walikuwa wanatuchezea. Baadhi ya waganda waliokuwa wamesomea masuala haya niliwapeleka kuongeza utaalam, waliporudi wakagundua mafuta haya mwaka 2006

Rais Museveni: Nataka watanzania na raia wa Afrika Mashariki tuamke! Huwa nafuatilia TBC1... Nitafanya mazungumzo na Rais Magufuli na CCM tuangalie jinsi ya kuimarisha masoko baina ya nchi zetu na kuimarisha undugu wetu

Rais Museveni: Hivi karibuni tutarudi Tanzania kuzungumzia masuala ya Gesi. Uganda ina uhitaji mkubwa wa gesi, namshukuru Rais Magufuli kwa utayari wa kupitisha bomba la gesi sambamba na bomba la mafuta! Huo ndo undugu
1600015289468.png
 
Mbona Total na Serikali ya UG wamesaini huo Mkataba jana , Sasa naona uliobaki ni wa Tz na UG
Total wanatakiwa wasaini mkataba na Tanzania vile vile kama sikosei. JPM lazima aridhie maana Uganda wanataka waondokane na umasikini wao as soon as possible. Huu ni mradi mkubwa sana utawavusha Uganda pamoja na Tanzania kwa asilimia kubwa fursa na ajira pamoja na kununua mafuta hapa hapa karibu kwa bei ya chini kidogo.
 
Wote wawili hao . Wanafanana kwa kuwatesa washindani wao . Bahati mbaya kila mateso yanapokuwa makubwa wananchi wanajawa hasira.
Kwa hiyo unapinga kuwa halina manufaa kwa Tanzani?
Mateso gani unayoyasema? Wananchi wanapigwa virungu na risasi barabarani?
 
Rais Museveni ametembelea tanzania Kikazi

Vile vile anakwenda kum update Mheshiwa Rais wetu juu ya bomba la mafuta baada ya Rais Museveni kukutana na CEO wa Total Patrick Pouyane na kuwezeshwa kusainiwa document muhimu kwa ajili ya kufikia Final Investment Decision (FID) ya uwekezaji katika bomba hilo.

Halafu yule mgombea wa Mbowe anasema Total inaondoka Tanzania ! Aibuuu ! No research no right to speak !
 
Mkuu Anatafuta kiki mpya .
lakuvunda halina Ubani,
Mwaka Huu Magu Out.
CCM OUT.
Ramli zinasema hivyo
labda Muahirishe uchaguzi kwa kukwepesha ile tarehe na siku.
labda kama unaongelea OUT inayoandikwa kwenye vituo vikubwa vya mabasi ya mikoani
 
Back
Top Bottom