Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Museveni kaja kumpa mbinu za utawala wa kidikteta.
 
Aisee, ina maana mtu anagombea huku anaendelea kufanya kazi kama rais?
 
Watanzania jamani hapa ndio tutie akili, haya mambo ya Chato kufanyika ziara hizi si dalili nzuri. Huyu kweli ataweza kuruhusu akili yake ikubali kuwa haya hayatakuwepo tena huko Chato akishindwa kwenye sanduku la kura?? Si atakomaa na kiti mpaka kufa kwake ili haya yaendelee! Chato sasa ndio Ikulu ya nchi.
 
Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi..... ndio Maana hata ccm wakilazimisha kuwa wengi bungeni bado mbunge mmoja wa Chadema anauwezo wa sawa na wabunge 50 wa ccm
Uwezo wa nini hebu fafanua.
 
Mkuu Anatafuta kiki mpya .
lakuvunda halina Ubani,
Mwaka Huu Magu Out.
CCM OUT.
Ramli zinasema hivyo
labda Muahirishe uchaguzi kwa kukwepesha ile tarehe na siku.
Mkuu Umemaliza kuota?,huyu anayesema ana risasi kumi kiunoni unadhani anaweza chukua nchi hii kweli?
 
Gorge Bush alipotembelea Arusha utalii uliongezeka sana
Obama alipotembelea Serengeti utalii uliongezeka
Kenyatta na mseven walipotembelea chato utalii umeanza kuimarika
Huna akili,usifanabishe marais wa dunia na hizo takataka
 
Bomba la mafuta litalipatia taifa letu mapato na ajira lukuki kwa watanzania wote.
Ni uwendawazimu kufikiria kuwa bomba la mafuta linalopita nchini mwako litakuwa na faida kubwa zaidi kushinda mapato ambayo yangepatilana kutokana na gas.

Hii ni sawa uwe na ng'ombe halafu umwue, baadaye jirani yako akaamua kufuga mbuzi. Kisha akakuambia kuwa anaomba awe anakata nyasi kwenye shamba lako kwaajili ya kulishia mbuzi wake. Halafu wewe kwa uwendawazimu ukabaki umekenua meno kwa kusema utafaidika sana kwa mauzo ya nyasi za kumlishia mbuzi wa jirani, na huku ulikuwa na ng'ombe, ukamwua.

Kutokana na upumbavu wetu, tumewafukuza wawekezaji wa mradi mkubwa wa gas, uwekezaji wa zaidi ya dola bilioni 30. Leo wanajenga Mozambique. Na 2019/2020, Mozambique inakuwa nchi ya pili kwa uwekezaji mkubwa wa gas Duniani.

Sheria za uvunaji mafuta za Uganda hazina tofauti na Sheria tulizokuwa nazo Tanzania. Sheria hiyo hiyo inapotumika Uganda, hawaibiwi, ikitumika Tanzania, tunaibiwa!!

Watanzania tusiwe wajinga wa kulishwa maneno ya wanasiasa wasiojua chochote kuhusiana na uwekezaji kwenye sekta ya mafuta/gas. Kwenye uwekezaji wa gas, awamu hii imeliangamiza Taifa. Nchi inayoongoza kwa pato la mwananchi Duniani ni Qatar. Mapato yake kwa zaidi ya 90% yanatokana na gas. Sheria ya uvunaji wa gas Qatar ni sawa na sheria ya gas tuliyokuwa nayo Tanzania kabla Kabudi hajaja na ile sheria ya hovyo ambayo haitaleta mwekezaji yeyote wa maana kwenye sejta ya madini na gas.

Tumeondoa wawekezaji kwenye gas kwa kulishwa maneno ya kijinga na watawala, leo imekuwa ngumu sana kumpata mwekezaji mwenye uwezo kuja kuwekeza kwenye gas ya Tanzania. Nani mwenye haja na Tanzania tena, wakati sasa Mozambique, kwa utafiti wa kina uliofanyika, tayari ina gas mara 2 ya ile ya Tanzania? Na bado utafiti unaendelea huko Mozambique, huku kwa upande wa Tanzania, hakuna mwenye haja ya kufanya utafiti wowote.

Sasa utafiti wa gas kwa Mozambique umeelekezwa zaidi upande wa bonde la Ruvuma, ambako gas hata ile iliyopo upande wa Tanzania, kwa sababu aquifer ni ile ile moja, itavunwa kwa kupitia upande wa Mozambique.

Kupata kiongozi asiye na uelewa ni hasara kubwa, lakini kuwa na wananchi wajinga wanaomshabikia kiongozi asiye na uelewa, anayefanya makosa makubwa ya kuwaletea hasara, ni laana kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hakika TUNDU LISSU ni jawabu la watanzania.


Baada ya kumchachafya sanaaa magufuli kwenye kampeni juu ya kuharibu mahusiano na majiran, kujenga kiwanja chato ambacho hakina faida


JAMAA WAMEHANGAIKA SANAA, NASIKIA M7 KAJA KWA MAKUBALIANO [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee, ina maana mtu anagombea huku anaendelea kufanya kazi kama rais?
Kazi ya rais haikomi hadi mwingine aapishwe nenda kasome katiba kabla ya kuja kulalamika. Ukasuku pelekeni kwenye chama cha ukoo kule uchagani.

$12.77 kwa kupitisha kila pipa la mafuta kwa kuanzia mapipa 1047 then up to 200,000 later ... .... .. patamu hapo ..... Ding ....Dong.
 
Itakuwa anakuja kumtembelea na kumjulia hali,Polepole na Bashiru kuongoza kampeni.
 
Back
Top Bottom