Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Hayo mafuta moja Sio yetu pili wanaingia gharama za kuchimba na kiwanda sisi kote huko hatupo

Deal liko fair
 
Mahesabu ya kibiashara huwa yananiwacha pembeni, Fikiria kampuni ya Twiga kwenye madini. Tanzania ina hisa 16% lakini faida tunagawana 50/50 na wenye hisa 84%😃😃
Madini ya kwetu yako ardhi yetu mafuta Sio yetu Ni ya waganda deal liko fair Sana tu
 
Hayo mafuta moja Sio yetu pili wanaingia gharama za kuchimba na kiwanda sisi kote huko hatupo

Deal liko fair
Unajua gharama za matunzo ya hilo bomba na umeme wa kuchemshia hayo mafuta? Kwanini a give up hiyo 20 percent
 
Mimi nimeelewa tofauti na wengi mnavyotafsiri. Nichoelewa ni kuwa umiliki wa hiyo miundo mbinu ya kusafarisha mafuta Tanzania itamilki 60% na Uganda 40%. Maana yake ni hii; kama mradi unagharamiwa kwa mkopo, Tanzania tutawajibika kulipa 60% na Uganda watalipa 40%.

Miundo mbinu kama "entity" utakuwa na mapato na matumizi; kama mapato yakizidi matumizi Tanzania na Uganda kama wabia watagawana kwa uwiano wa 3:2
 
Madini ya kwetu yako ardhi yetu mafuta Sio yetu Ni ya waganda deal liko fair Sana tu
Kwa hiyo hayo mafuta yanachimbwa kwenye ardhi Tanzania? Leo mnakubali kuwa hiyo inawezekana na Mnafuta zile kelele za 50/50 haiwezekani John ni muongo? Mgao wa mapato ktk Biashara na uwekezaji haiendeshwi kwa amri za Bunge bali kwa makubaliano ya kimkataba.
 
Yeye achape tuuu..ila aangalie asije akachapika october28
Haiwezi kutokea
8b8772af65a848b2211cc750a1e7211b.jpg
 
Rais Museveni ametembelea tanzania Kikazi

Rais Magufuli: Km 330 za bomba hili zipo Uganda. Kwa Tanzania, bomba litapita kwenye mikoa 8, wilaya 24 na kata 132. Tathmini kwa Tanzania, watu zaidi ya 90,000 watalipwa fidia; ni takribani bilioni 21

21Bil gawa kwa watu 90,000 ni 233,333/=
Fidia gani hii?
 
Nakumbuka huu mradi ulizinduliwa 2016 Kwa mbwembwe sana na mikataba ikasainiwa hadharani na tukajulishwa kuwa mradi utakamilika mwezi wa nne Mwaka 2019 nashangaaa tena leo eti unazinduliwa na katika uzinduzi huo nimesikia maneno kuwa tunataka mazungumzo yafanyike mapema ili michakato ianze haraka, sijaelewa?

Au ni Lissu ndio anafanya watu warudie hadi mikataba? Huyu Lissu huyu atasababisha hadi ule mradi wa Umeme usainiwe upya haki Ya MUNGU, sijawahi ona kitu kama hiki na hii inaitwaje wakuu?

Mzeee wetu anazungumia ajira kuwa mradi utaajiri watu 13,000 anasahau kuwa Kikwete kila Mwaka Alikuwa anaajiri watu 60,000 kwa mwaka, yeye kazuia halafu anapigia upatu ajira Ya mafuta ya Uganda.
Huu mradi wa bomba unazinduliwa kila baada ya miezi mitatu kiasi kwamba tumechoka kuusikia. Kwani lazima uzinduliwe kila mara? Kuna shida gani?
 
Back
Top Bottom