Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Pole sana mkuu. Kwani unaamini kuwa Museveni kafunga Safari kutoka Kampala kwa ajili ya kuifanyia kampeni CCM.

Kumbe kitu gani kama sio hicho...
IMG-20200914-WA0000.jpg
 
Rais Museveni ametembelea tanzania Kikazi

View attachment 1568899

===

Rais John Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wamesaini makubaliano ya kuanza ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania...

Ni ushirikiano wa aina hii Mwalimu Nyerere, na wenzake wengine walioasisi kinachojulikana kama South-South Commission, walikuwa wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa nchi zinazoendelea badala ya kila siku kukodoa macho kwa mataifa ya magharibi (nchi zilizoendelea) kama suluhisho la changamoto zao.

Tukio kama hili haliwezi kupendeza kambi ya nchi hizo kwani wanatamani siku zote kuuchukulia mustakabali wetu kama hisani itokanayo kwao.

Viongozi wetu wameamua kuyaishi kwa vitendo mawazo ya waasisi wetu kwa kuimarisha ushirikiano na uhusiano kwa kuanzisha mradi mkubwa kama huu kwani utachochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi zetu.

Kwa sasa hivi wanapaswa kuziba masikio kutosikiliza makelele ya mawakala waaminifu wa magharibi ambao wangetamani kuona waasisi wa wazo kama hili wakiwa Wamarekani, Waingereza au Wajerumani.

Historia itawakumbuka.
 
Kodi ya kupitisha mafuta ya Uganda nchini iliamuliwa na bunge yaani kila pipa ambalo kodi yake itakuwa USD 12 basi Tanzania ilitakiwa kupata asilimia 80 kwani bomba hilo lipo katika ardhi ya Tanzania kwa zaidi ya asilimia 80.

Sasa cha ajabu jana ili Rais Magufuli kumharakisha rafiki yake Rais Museven akaona ampunguzie tena asilimia 20 huku akienda kinyume na yaliyopitishwa na bunge.

Kwa kupata kodi ya asilimia 60 kwa kila pipa huku ukizingatia mkataba kuwa matengenezo yote ya bomba hilo, kulilinda pamoja na kutumia umeme mkubwa kuchemsha mafuta hayo muda wote kwa asilimia 80 ya bomba hilo itakuwa gharama za Tanzania. Je tunavuna nini?

Hivi hatukujifunza kutoka kwa wataalam wa Uganda waliokuwa wakimkatalia Rais wao kuhusu kujirahisisha kwa hao Total waliotaka kujipatia faida kubwa kutokana n uuzwaji wa mafuta hayo? Hadi ikafikia hatua eti Rais Magufuli akamshauri Museven awafukuze kazi kisa wanamchelewesha? Kwanini sisi watanzania tumekubali kuamuliwa na mtu mmoja ambaye alitaka hata kuingilia yaliyokuwa yakiendelea huko Uganda? Kama Museven angekuwa na hulka hiyo basi bomba lilitakiwa liwe linapitisha mafuta sasa ila aliona umuhimu wa kuwasikiliza wataalamu wake kuhusu maslahi ya Uganda.

Yeye Museven auze mafuta, halafu asilimia 20 tu ya bomba ipo Uganda kisha kodi ya kusafirisha mafuta anafaidi asilimia 40! Na sisi tunasema ndiyo mzee!

Kiasi kioichopotezwa
USD 12 × 0.2= 2.4 USD Per drum
USD 2.4 × Drums 6,500,000,000 = USD 15,600,000,000
Yaani kwa mapipa yote bilioni 6.5 Tumepoteza USD bilioni 15.6 kwa muda wote wa mradi! We are not serious!
 
Hayo mambo ya kusaini yanaendelea kufanyika kila baada ya miezi mitatu. Magufuli kamwita ile asaidiwe kampeni. Hilo Museveni kalisema live! Bomba limeshasainiwa zaidi ya mara sita.

Acheni kuwadanganya watanzania. Magufuli ameshakuwa muongo kupita kiasi.
 
Kodi ya kupitisha mafuta ya Uganda nchini iliamuliwa na bunge yaani kila pipa ambalo kodi yake itakuwa USD 12 basi Tanzania ilitakiwa kupata asilimia 80 kwani bomba hilo lipo katika ardhi ya Tanzania kwa zaidi ya asilimia 80...
Mbona unaeleza kwa kutetemeka?

Tulia bwashee uandike vizuri tena kwa ushahidi!
 
Bunge la Taifa linapogeuzwa kuwa kikao cha chama tawala haya ndiyo madhara yake..

Ni kamati ipi ya Bunge itasubutu kuhoji hilo...huyo Mwenyekiti wa kamati hajipendi?

Hapo ndipo tulipofikia watanzania.
 
Kodi ya kupitisha mafuta ya Uganda nchini iliamuliwa na bunge yaani kila pipa ambalo kodi yake itakuwa USD 12 basi Tanzania ilitakiwa kupata asilimia 80 kwani bomba hilo lipo katika ardhi ya Tanzania kwa zaidi ya asilimia 80...
Mahesabu ya kibiashara huwa yananiwacha pembeni, Fikiria kampuni ya Twiga kwenye madini. Tanzania ina hisa 16% lakini faida tunagawana 50/50 na wenye hisa 84%😃😃
 
hahaha !Tanzania nibMali ya ccm na rais wao hilo hujui,kwani akiamua kuwasamehe kodi utamfanya nini?
mlikaata katiba ya warioba sasa mtakiona
 
MLETA MADA!
ELEWA SOURCE YA MRADI HUU NI MAFUTA.

MAFUTA SIO YETU BALI YA WAGANDA, WEWE HUJUI NI KIASI GANI CHA JITIHADA, ZILIZOTUMIKA HADI KUISHAWISHI UGANDA KUBADILI UAMUZI WAKE WA AWALI. ILIKOKUWA AWALI LIPITIE BANDARI YA MOMBASA.

UNASEMA TUTATUMIA UMEME WETU KULIPASHA BOMBA JOTO. UMEME HUO WATALIPIA NA SIO BURE KAMA UNAVYOTAKA KUPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA.

SASA NIKUTAARIFU KWAMBA ULE MRADI WA STIEGLES GORGE UNA MANUFAA KWA UCHUMI WA NCHI HII.

RAIS AMENUKULIWA KWEMYE HOTUBA YAKE, YA KWAMBA KUNA MIKATABA MIDOGO MIDOGO AMBAYO BILA SHAKA NI YA KITAALAMU ZAIDI, AMBAYO BADO INAFANYIWA KAZI.

WEWE UNAKURUPUKA KUTOKA HUKO ULIKOTOKA NA KULETA HOJA YAKO YA KI LISU LISU HUMU.

JE ULITAKA UGANDA WAURUDISHE KENYA ILI KESHO MJE NA HOJA ZA KIJINGA ZA KIDIPLOMASIA MFU HUMU?

ACHENI NCHI ISONGE MBELE..
 
Kwanini Magufuli afanye maamuzi ya % yeye kama yeye bila kulipeleka suala hilo bungeni. Huu ni udikteta kamili.
 
MLETA MADA!
ELEWA SOURCE YA MRADI HUU NI MAFUTA.

MAFUTA SIO YETU BALI YA WAGANDA ,WEWE HUJUI NI KIASI GANI CHA JITIHADA, ZILIZOTUMIKA HADI KUISHAWISHI UGANDA KUBADILI UAMUZI WAKE WA AWALI. ILIKOKUWA AWALI LIPITIE BANDARI YA MOMBASA....
Gharama ya huo umeme, maintenance costs kuwalipa wafanyakazi na walinzi ni kutoka katika hiyo asilimia 60 ambayo ni USD 7.2 kwa kila pipa litakalo safirishwa. Usibishane na mtu aliyekuzidi maarifa kwa mbali mno!
 
Back
Top Bottom