Kodi ya kupitisha mafuta ya Uganda nchini iliamuliwa na bunge yaani kila pipa ambalo kodi yake itakuwa USD 12 basi Tanzania ilitakiwa kupata asilimia 80 kwani bomba hilo lipo katika ardhi ya Tanzania kwa zaidi ya asilimia 80.
Sasa cha ajabu jana ili Rais Magufuli kumharakisha rafiki yake Rais Museven akaona ampunguzie tena asilimia 20 huku akienda kinyume na yaliyopitishwa na bunge.
Kwa kupata kodi ya asilimia 60 kwa kila pipa huku ukizingatia mkataba kuwa matengenezo yote ya bomba hilo, kulilinda pamoja na kutumia umeme mkubwa kuchemsha mafuta hayo muda wote kwa asilimia 80 ya bomba hilo itakuwa gharama za Tanzania. Je tunavuna nini?
Hivi hatukujifunza kutoka kwa wataalam wa Uganda waliokuwa wakimkatalia Rais wao kuhusu kujirahisisha kwa hao Total waliotaka kujipatia faida kubwa kutokana n uuzwaji wa mafuta hayo? Hadi ikafikia hatua eti Rais Magufuli akamshauri Museven awafukuze kazi kisa wanamchelewesha? Kwanini sisi watanzania tumekubali kuamuliwa na mtu mmoja ambaye alitaka hata kuingilia yaliyokuwa yakiendelea huko Uganda? Kama Museven angekuwa na hulka hiyo basi bomba lilitakiwa liwe linapitisha mafuta sasa ila aliona umuhimu wa kuwasikiliza wataalamu wake kuhusu maslahi ya Uganda.
Yeye Museven auze mafuta, halafu asilimia 20 tu ya bomba ipo Uganda kisha kodi ya kusafirisha mafuta anafaidi asilimia 40! Na sisi tunasema ndiyo mzee!
Kiasi kioichopotezwa
USD 12 × 0.2= 2.4 USD Per drum
USD 2.4 × Drums 6,500,000,000 = USD 15,600,000,000
Yaani kwa mapipa yote bilioni 6.5 Tumepoteza USD bilioni 15.6 kwa muda wote wa mradi! We are not serious!