Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Pinga pinga katika ubora wako.
 
Mahame ya kijiji cha Mobutu Sese Seko Ngebu wa Zabanga Zaire Congo DRC

22 Dec 2018
Katika mji wa Gbadolite alikotoka, Rais Mobutu Sese Seko alijenga kasri kubwa la kifahari na uwanja wa ndege ambao ndege za kusafirisha bidhaa za anasa kama vile mvinyo ghali kutoka Ulaya zilitua na kupaa. Njia ya kutumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja huo ilikuwa kubwa kiasi cha kuweza kutumiwa na ndege kubwa ya wakati huo Concorde - ambayo aliikodi mara kwa mara. Lakini alipotimuliwa madarakani mwaka 1997, kila kitu kilisimama. Sasa ni mahame.
 
Hakuna majibu, na huyo Museveni kaishia kumuombea Magufuli kura, maana ndio kilichomleta. Hilo la uzinduzi wa mradi ni utapeli tu.

Museveni kasoma chuo kikuu mlimani nadhani unalijua hilo.

Hawezi kuja kumuombea kura Tundu Lissu asiyemheshimu Hayati Nyerere.
 
Watanzania ni wajinga kuanzia viongozi wetu hadi maCCM yanafurahia miradi ya watu wengine ya kwetu ikidolora kama Haina wenyewe. Hilo Bomba la mafuta ni mradi wa Uganda kwa asilimia 100% hapa kwetu Bomba na mafuta ghafi yatakuwa yanapita tu kwenda kwa wateja wa Uganda na watumishi muhimu wote watakuwa Waganda, Watanzania labda watakuwa wafagiaji. Kuna TAZAMA Pipeline kwenda Zambia sasa lina miaka zaidi ya 50 lakini Watanzania wengi hawajui kuwepo kwa Bomba hilo wala faida yake kwa nchi yetu. Kama TAZARA, Miradi hii inaanzishwa kisiasa inaishia kutokuwa na faida kwa nchi kiuchumi na hata kuwa mizigo. Miradi ya kisiasa ni balaa, tutaona mingi tu!
 
Nakumbuka huu mradi ulizinduliwa 2016 Kwa mbwembwe sana na mikataba ikasainiwa hadharani na tukajulishwa kuwa mradi utakamilika mwezi wa nne Mwaka 2019 nashangaaa tena leo eti unazinduliwa na katika uzinduzi huo nimesikia maneno kuwa tunataka mazungumzo yafanyike mapema ili michakato ianze haraka, sijaelewa?

Au ni Lissu ndio anafanya watu warudie hadi mikataba? Huyu Lissu huyu atasababisha hadi ule mradi wa Umeme usainiwe upya haki Ya MUNGU, sijawahi ona kitu kama hiki na hii inaitwaje wakuu?

Mzeee wetu anazungumia ajira kuwa mradi utaajiri watu 13,000 anasahau kuwa Kikwete kila Mwaka Alikuwa anaajiri watu 60,000 kwa mwaka, yeye kazuia halafu anapigia upatu ajira Ya mafuta ya Uganda.
 
Anayejua bei ya V8 anijuze nayaona yapo mengi mno kwenye msafara. Naomba kufahamu hilo wakuu.
 
Mkataba wa kuanza ujenzi ndo umeingiwa sasa.
 
Mwambie ameshafeli kabla hajaanza
 
Vijana ndiyo tatizo la tawala za kidikteta. Hapa ni “you rub my back, and I rub yours”. Wanakubaliana kushirikiana ili kuzima sauti za vijana?

Ninavyofahamu, Uganda ni nchi ya pili Africa kwa kuwa na vijana wadogo. Boby Wine anawapa shida kweli kweli. Siwezi kushangaa dikteta akiombea kura nchi jirani ili na yeye aendelee kupata msaada wa kubakia madarakani.
 
The project should be non-political. It should be seen purely as an EAC economic integration project for the benefit of its citizens.
 
umeongea kwa uchungu sana dah,lakin ndio hivyo project inaanza
 
Kilichotangazwa hapo ni CIA (Chato International Airport) na siyo mbuga ya Burigi - Chato.

Kama hata TBC umewasikia wakisemi neno hifadhi ya Burigi - Chato, simama ukiwa umenyosha mkono ujibu swali. Binafsi nimesikia tu maneno, mkataba huu unasainiwa hapa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Chato, na hata Rais JPM kpiga kijembe kuhusu CIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…