Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Isijekuwa Jiwe ameshaingia mfukoni maana hachelewi. Nimemsikia Mu7akisma hiyo bilioni 14 ni kurumure...Yani wanaanza kulima shamba so wanaingia mfukoni. Kama ulimsikiliza vizuri hadi yule mhaya akatafsiri maana ya kirumure
Na bilioni 14 siyo Shs. Ni madolari

Bwaahaaa bwahaaa yaani nimecheka kwa nguvu ile mbaya. Magufuli ana miradi mikubwa miwili huku ndani, inakadiriwa kuwa ni 15t+ ikikamilika kwa 100% yote. Mpaka sasa hakuna mradi wowote umefanyika hata robo, na hajafikisha hata nusu ya hela yaani 7t, amebakisha miaka mitano iwapo tume ya uchaguzi itamtangaza mshindi, haifahamiki ni wapi atapata 7-10t ili kukamilisha hiyo miradi achia mbali shughuli nyingine, saa hii wanaongea na Museveni Njozi za $14b!? Halafu hao wanaccm waliosombwa na malori, wanashangilia hilo igizo kuwa wako na visionary leaders, wakati hata sarafu ya pamoja ya EA imewashinda. Shubamiit.
 
119178995_198652328282550_2480959954329160437_o.jpg
 
Kasoma mlimani so what? Kwanza alichokifanya Museveni ni kosa kidiplomasia. Hairuhusiwi mtu kutoka nje ya nchi kuja kuingilia siasa za ndani ya nchi nyingine. Nilijua lazima utatepeta tu kwenye hii hoja. Na sio ww peke yako ni wanaccm wote mmeshapanick. Kwasasa wapinzani waanze kutegemea ushindani wa kikatili, maana tayari ccm imekata pumzi mpaka wanamuita rais wa nchi nyingine kuja kuwaombea kura.
Hizi imani zenu za CCM kukata pumzi ndio huwa zinawapelekea kusema mnaibiwa kura!!.

Muibiwe kura kwa substance ipi mliyonayo mbele ya jamii!!.

Siasa za jamii forum na twitter ni tofauti kabisa na zile za field na huwa hamjifunzi chochote.

Huwezi kumpangia mkuu wa nchi lipo aongee na kipi asiongee yule ni rais sio admin wa kundi la whatsapp.
 
Nimemsikia Rais Mseveni akimuombea Kura Rais Magufuli na ccm kuwa itapatapa ushindi.

Hili linaweza kuchukuliwa vibaya na wafuasi wa vyama pinzani japo ziara yake ilikuwa ya kikazi na yenye faida kubwa kwa Tanzania lakini hili la uchama litaondoa mazuri yote aliyo kuja nayo.

Lakini pia ni dhahiri Rais Museveni kuwa mwana ccm halisi baada ya kuomba nyimbo za zamani za Tanu enzi hizo akiwa Tanzania.
Birds of the same feather fly together.
 
umeongea kwa uchungu sana dah,lakin ndio hivyo project inaanza

Ni kweli, ule mradi mliosaini kuanza 2017 na kukamilika 2020 mmeuza mapipa mangapi mpaka sasa? Nasikia huu mradi wa sasa ndio mtapiga faida ya ajabu, 60% ya Ccm, na 40% ya waganda!
 
Sina tatizo na kuahirishwa na ninakubaliana na hilo kabisa. Je kuna haja gani ya kukusanya kundi lile lile la viongozi, kuweka mkataba ambao ulikuwa umeahirishwa? Shaka yangu ni hii, wakati ule Tanga wazungu wa Total walikuwepo, na mradi haukwenda kama tulivyoaminishwa, ila leo igizo ni lile lile bila hao wazungu. Ninachoona hapo ni wanaccm ambao hawana hata kumi ya kutoa kwenye huo mradi, huku wazungu wenye pesa hawako kwenye hizo hii episode II. Naona ni kampeni zaidi.

Ninasema hivyo maana nina uzoefu na huyo Museveni. Aliwahi kupewa sehemu ya bandari ya Tanga aendeleze lakini hakufanya hivyo, hilo bomba alishakubali kulipitisha Kenya lakini kabidili porojo kalileta Tanzania! Kuna mengi ila leo sio mada, lakini huyo Museveni ni tapeli kama matapeli wengine, na ndio maana naona kwa sasa ni kampeni zaidi kuliko kinachoongelewa.
Wewe mpuuzi, sikiliza ijumaa M7 alisema nini kuhusu kumuomba JPM? Endelea hapa
 
Back
Top Bottom