Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Ujenzi wa Bomba la Mafuta: Ziara ya Rais Museveni nchini Tanzania - Septemba 13, 2020

Kutoka Kwa mama Maria Nyerere Hadi yoweri museven?
Uchaguzi huu umekufunza abadu magufuli na hapo bado tukiuanza mwezi October ndiyo itakuwa balaa zaidi
 
Nimemsikia Rais Mseveni akimuombea Kura Rais Magufuli na ccm kuwa itapatapa ushindi.

Hili linaweza kuchukuliwa vibaya na wafuasi wa vyama pinzani japo ziara yake ilikuwa ya kikazi na yenye faida kubwa kwa Tanzania lakini hili la uchama litaondoa mazuri yote aliyo kuja nayo.

Lakini pia ni dhahiri Rais Museveni kuwa mwana ccm halisi baada ya kuomba nyimbo za zamani za Tanu enzi hizo akiwa Tanzania.
Na bado Raila Odinga na yeye atakuja kumuimbea kura JPM ndo mjue kwamba JPM ni mfano wa kuigwa Afrika
 
Hizi imani zenu za CCM kukata pumzi ndio huwa zinawapelekea kusema mnaibiwa kura!!.

Muibiwe kura kwa substance ipi mliyonayo mbele ya jamii!!.

Siasa za jamii forum na twitter ni tofauti kabisa na zile za field na huwa hamjifunzi chochote.

Huwezi kumpangia mkuu wa nchi lipo aongee na kipi asiongee yule ni rais sio admin wa kundi la whatsapp.

Kwani huko kwenye box la kura kura huwa mnashinda au mnatangazwa washindi? Mngekuwa mnashinda mngelazimisha kupita bila kupingwa? Jamii ipi, hii inayoshurutishwa kuikubali ccm?

Huku mitandaoni ndio sehemu watu wanafunguka ukweli ambao ni hatari kuuzungumza huko mitaani. Huko mtaani mnajivunia watu wengi wenye ufinyu wa taarifa nothing else. Kwani huyo mkuu wa nchi anapangiwa cha kuzungumza kwa utashi wetu, au ni sheria za kimataifa zinaagiza hivyo?

Wakati ww unajivunia ccm kutangazwa washindi, sisi tunajua kabisa kuwa ccm huwa haishindi bali umiliki wa vyombo vya dola ndio huwabeba. Na udhibitisho kuwa ccm imekata pumzi, ni ww kuzunguka hapa bila kujibu hoja ya tofauti ya hii episode ya leo, na ile ya 2017.
 
Wewe mpuuzi, sikiliza ijumaa M7 alisema nini kuhusu kumuomba JPM? Endelea hapa


Nishike lipi? Hilo ombi la Ijumaa la Museveni au yale makubaliano ya 2017 kuwa hilo bomba litakuwa tayari 2020? Halafu kuna jipya lipi la kufuatilia hapo kuwa eti Tanzania itapata 60% na Uganda 40%, mkuu mbona mimi sina akili hizo za kushikiwa.
 
Viongozi wanaojifahamu wanajiepusha sana na siasa za ndani ya nchi nyingine, lakini hii ndio Africa. Yaani huyu mzee ndio wa kumuombea kura JPM?
Idumu EAC ...kudumu chama cha mapinduzi
 
Wataalam, mimi sijaelewa hapo jamaa anaposema na sisi Tanzania tutalitumia hilo hilo bomba kupeleka gesi huko Uganda. Sasa gesi, hata kama ni liquefied natural gas (LNG) na mafuta yatakuwa yanapishanaje kwenye hilo bomba? Yaani gesi inakwenda Uganda na mafuta yanakwenda Tanga! Au watapeana zamu?
Msinicheke, haya mavitu sina utaalamu nayo.
Linaweza kuwa na section mbili, moja ya gesi nyingine mafuta
 
Dogo ungejua wakati nyie wanyonge mnaigia uchumi wa chini Kati mi tayari Niko uchumi wa juu
Upo uchumi wa juu kusafisha vizee vya kizungu khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ujinga mtupu. Siwezi kuwa mtumwa.
 
Kipi kinamshinda? Kwani anatumia gharama gani wakati gharama zote zinabebwa na serikali yetu? Narudia tena maana naona unakwepa hapo. Siku ile Tanga walisaini mkataba kuwa ujenzi unaanza na kukamilika hii 2020, tena mbele ya wazungu wa Total. Iweje leo 2020 mradi haujaanza kisha wanasaini tena mradi kuanza, huku wazungu wa Total hawapo, zaidi ya wanaccm walioko kwenye kampeni mode? Jikite kwenye ufafanuzi huo.
Mkuu jiongeze,vinginevyo watakuita kilaza.
Wewe ulisoma ABC ya mkataba?
Umesahau kuwa wadau wa mkataba ndio wanafanikisha mkataba?
Na hujui katika mkataba kuna wanauza na wanaonunua?
Elimu mkuu achana na porojo.
 
Linaweza kuwa na section mbili, moja ya gesi nyingine mafuta
Mnahangaika na nini? Mbona imeelezwa kuwa wataweka bomba jingine la gesi kwenye njia hiyo kama inawezekana ili hilo bomba jipya lisafirishe gas kwenda Uganda. Wacheni kuzunguka mbuyu.
 
Hivi huyu jamaa aliwaza nn kujenga uwanja huu porini huyu hana mpango wa kuondoka madarakani
 
Hivi huyu jamaa aliwaza nn kujenga uwanja huu porini huyu hana mpango wa kuondoka madarakani
Chato ni porini? Kweli JF imevamiwa! Hili bomba limewaumiza wengi bado majibu kutoka Kenya et al khe khe keh khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Nimemsikia Rais Mseveni akimuombea Kura Rais Magufuli na ccm kuwa itapatapa ushindi.

Hili linaweza kuchukuliwa vibaya na wafuasi wa vyama pinzani japo ziara yake ilikuwa ya kikazi na yenye faida kubwa kwa Tanzania lakini hili la uchama litaondoa mazuri yote aliyo kuja nayo.

Lakini pia ni dhahiri Rais Museveni kuwa mwana ccm halisi baada ya kuomba nyimbo za zamani za Tanu enzi hizo akiwa Tanzania.

Kwa taarifa yako hakuna mazuri yoyote aliyokuja nayo Museveni, na amefanya kosa kubwa kabisa la kidiplomasia kuingilia siasa za ndani za Tanzania. Museveni ni tapeli kama tapeli mwingine yeyote, na kilichomleta ni sababu za kisiasa na kampeni za kichovu. Hilo igizo la leo lilifanyika mwaka 2017 chongoleani huko Tanga, na mkataba ulionyesha mradi kuanza mara moja 2017 na kukamilika 2020. Tena igizo lile la kwanza ambalo halijafanyika mpaka sasa, wazungu wa Total walikuwepo.

Ukitaka kujua hili la leo ni igizo la kisiasa na hakuna lolote jipya, wale wazungu wa Total ambao ndio watoa hela hakuwepo hata mmoja, zaidi ya wanaccm waliovaa sare tayari kwa igizo la kampeni. Mahali nimejua ile ilikuwa ni siasa za ccm za kupanick maana kampeni zimekuwa nzito, Magufuli anasema waliongea dakika tano tu chemba, wakakubaliana Tanzania ipate 60% na Uganda ipate 40%, huku watoa pesa ambao ni Total mgao wao haikutajwa kabisa! Hivi bado karne hii ccm mnacheza hizo siasa za kichovu hivyo?
 
Mzee shule hujaenda soma uzi wa Pascal Mayalla kuhusu CODO, DODO na COCO kukupa summary ni kwamba Total inaachana na biashara ya kuvimiliki vituo vya mafuta na kuwauzia watu binafsi lakini itakua inaoperate kwa kutumia jina la TOTAL
Mkuu Lyamber nadhani wewe ndio unahitaji kuelimishwa maana umesoma uzi wa Pascal juu juu. I know better than you and Pascal ! Nina maanisha.

Total ina encourage franchises yaani DODO (Dealer Owned Dealer Operated) wakati huo huo inaendelea kumiliki vituo yvake under COCO (Company Owned Company Operated) na CODO (Company Owned Dealer Operated). Visit Total Tanzania web site www.total.co.tz ukaelimike huko.
 
Na bado Raila Odinga na yeye atakuja kumuimbea kura JPM ndo mjue kwamba JPM ni mfano wa kuigwa Afrika

Mfano wa kuigwa kwa kukiuka diplomasia ya kimataifa? Unajisifia uvunjifu wa sheria za kimataifa waziwazi?
 
Back
Top Bottom