Nadhani mfumo wa malezi kwa wazazi wa kiafrika hasa Tanzania ndo unafanya vijana wengi wawe tegemezi.Achilia mbali vijana wangu 4, hata ndugu zangu wa tumbo moja wote hakuna alieajiriwa serikalini na maisha yanaenda, Ila ukichunguza mazingira tuliyoanzia kutafuta, naamini ni vijana wachache sana wa leo wanaoweza kufanya. Wengi ni wavivu, aibu nyingi, waoga, wanachukulia maisha kama kitu simple Sana(utawakuta wanajadili kilimo cha mtikiti mitandaoni wakiwa na matarjio makubwa kweli😂),alafu umri wao ukienda wanabaki na kazi ya kuilaumu serikali juu ya Hali mbaya ya mifuko yao.