BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Kwa zaidi ya miezi miwili eneo la Karume ambalo ni maarufu kwa wafanyabiashara wa mitumba kumekuwepo na changamoto ya foleni ambayo inatokana na ujenzi wa njia ya Mwendokasi.
Mkandarasi ameziba njia upande mmoja kwa muda mrefu huku shughuli za ujenzi zikiwa zinafanyika taratibu (slow) jambo ambalo linachangia kero kudumu muda mrefu bila kujali umuhimu wa eneo hilo kibiashara.
Ni muda umepita zaidi ya miezi sita tokea ujenzi huo uanze katika eneo hilo lakini hatuoni jitihada za kuharakisha kipande hicho kukamilika ili kuwezesha shughuli nyingine kuendelea.
Wito wangu kwa mamlaka zifuatilie kwa ukaribu changamoto hiyo, ni muhimu ujenzi katika eneo hilo ukafanyika haraka ili kuwezesha shughuli nyingine katika eneo hilo kuendelea kama kawaida pamoja na kuondoa kero ya foleni.