Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa meli nne za mizigo zinazojengwa katika Bandari ya Karema mkoani Katavi. Waziri Mbarawa yupo mkoani Katavi kwa ziara yake ya siku mbili amekagua ujenzi wa meli nne za mizigo pamoja na utoaji huduma katika Bandari ya Karema.
Meli hizo zinajengwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kushirikia na kampuni binafsi ya Nzenching International Company, na kila meli ina uwezo wa kubeba tani 2,000.
Ujenzi umeanza mwezi Aprili mwaka huu; meli ya kwanza imeshafikia asilimia 90, meli ya pili asilimia 85, meli ya tatu asilimia 75, na meli ya nne asilimia 35.
"Tunaamini meli hizi zitakapokamilika na kuanza kufanya kazi, zitabadilisha kabisa uchumi wa Mkoa wa Katavi na Kigoma. Tutakuwa na wafanyakazi zaidi ya 6,000 hadi 7,000. Huu ni mwendelezo wa maono ya Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kushirikisha sekta binafsi katika miradi mikubwa ya usafirishaji kwa njia ya maji". Alisema Mbarawa
Waziri Mbarawa pia amebainisha kuwa meli hizo zitatumika kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Karemi- Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kwenda Kigoma, Katavi na Bandari ya Dar es salaam, na katika nchi ya Zambia, jambo litakaloongeza biashara na ushawishi wa kiuchumi katika ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Jamila Yusuph, aliipongezea serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwekeza katika mradi huo mkubwa. Amesema hatua hii ni fursa kubwa kwa wakazi wa Katavi na utaongeza ajira na biashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa alisema kuwa ushirikiano kati ya TPA, TASAC, na taasisi nyingine za Serikali ni msingi wa mafanikio ya mradi huo.
"Meli hizi zitakuza shughuli za uchumi kwenye mnyororo wa usafirishaji kutoka Karemi kwenda na Kigoma hadi Bandari ya Dar es Salaam, na kusaidia kuharakisha ujenzi wa reli na barabara kutoka Mpanda kwenda Karema”, Alisema Mbossa.