JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akikagua kuanza kwa kazi ya Ujenzi wa upanuzi wa Barabara hiyo ya njia nne sehemu ya kwanza inayoanzia Round about ya Rwamishenye hadi eneo la Mitaga lenye urefu wa Kilometa 1, alielekeza ujenzi ufanyike kwa mtindo huo hili kukamilika kwa wakati.
Bashungwa alisema Tsh. Bilioni 4.61 zilitolewa kwa ajili ujenzi wa upanuzi sehemu ya kwanza inayoanzia Roundabout ya Rwamishenye hadi Mitaga yenye urefu wa Kilometa 1.
Ambapo katika kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kama ilivyokusudiwa tayari kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ilielezwa zilitengwa kwa ajili ya kulipa fidia.
Kwa mujibu wa TANROADS - Kagera ilielezwa utekelezaji ambao unafanywa na Mkandarasi M/s Abemulo Contractors Ltd utakuwa wa miezi 12 ambapo kazi kuanzia Oktoba 9, 2023.
Mkandarasi alianza na kasi lakini kwa sasa zoezi linaonekana kusuasua tofauti na matarajio yaliyokuwepo awali kwamba kipande hicho kitakamilika kwa wakati ikizingatiwa ilielezwa wazi fedha kwa ajili ya utekelezaji zilikuwa tayari zimeshatolewa.
Kwa sasa ni Desemba 2024, takribani miezi miwili inapita tokea muda wa ujenzi uliotajwa kwamba kipande hicho kikamilike hatuoni hizo dalili na Mkandarasi ni kama ameenda likizo, tunajiuliza kuna changamoto gani ambayo imepelekea ujenzi huo kutokukamilika kwa wakati?
Ujenzi wa barabara hiyo umekuwa ukipelekea baadhi ya shughuli zinazofanyika katikati ya Mji wa Bukoba kutofanyika kama ilivyozoeleka awali, hilo linachngiwa na magari mengi hasa makubwa kushindwa kuingia eneo la Mjini, ikizingatiwa hiyo ndio njia kuu inayotegemewa zaidi kuingia Mjini hasa kwa magari makubwa.
Hata hivyo wasiwasi wangu kama kipande hicho kinakaa kwa muda mrefu hivyo bila kukamilika wakati tayari pesa ipo, je awamu nyingine za uendelezwaji wa ujenzi ambazo zimeshatangazwa zitakamilika lini, hili kurejesha Mji katika hali ya kawaida hususani shughuli za kiuchumi?
Siku Waziri Bashungwa alipotembelea ujenzi wa Barabara hiyo
Pia soma
~ Serikali Kuongeza Bilioni 4 Kukamilisha Upanuzi wa Njia 4 Bukoba Mjini
~ Shilingi Bilioni 45.6 kutumika kukamilisha Miradi ya Dharura Mkoani Kagera